Jambo lipo dhahiri, kwamba CHADEMA watalazimika kufanya kazi ya ziada ili waweze kukubalika maeneo ya pwani! Iwe ni matunda ya propaganda au vinginevyo, tayari taswira ya CHADEMA machoni mwa watu wengi haioneshi utaifa kama ilivyo kwa CCM! Inawezekana kabisa kwamba CCM kikaonekana ni very CORRUPT, lakini linapokuja suala la muonekano wa kitaifa, CCM is far better than CHADEMA and even CUF!
Hili, halikuja kwa bahati! Ni dhahiri kwamba, propaganda za CCM zimesaidia kujenga taswira hiyo ya CHADEMA kuonekana enzi zile kwamba ni chama cha Wachaga, ikaja kuwa cha Kikristo na sasa cha kikanda! Kwa bahati mbaya sana, ama kwa makusudi ama kwa ukosefu wa weledi wa kile kinachosemwa "Think All Before You Speak, But Don' Speak All Before You Think", imetokea mara kadhaa kauli za viongozi wa CHADEMA kuleta mshabihiano wa yale yanayosemwa na wapinzani wa CHADEMA!! Mbaya zaidi, kosa ambalo lilitokea kwa CUF limerejea CHADEMA! Wakati CUF kikituhumiwa kwamba ni Chama Cha Waislamu, ikatokea Waislamu wengi wakajiunga na Chama hicho na tangu hapo hata mamo ya CUF yakakaa Kiislamu Islamu! Ilikuwa ni jamo la kawaida kwenda kwenye mikutano ya CUF na kukuta full Barkhashia!! Hivyo hivyo, wapo Watanzania wengi tu hivi sasa ambao wanajikuta wanaiunga mkono CHADEMA kwa ajili tu ya Ukristo wao! Hata hapa JF, ukiangalia Wakristo ambao wamekubuhu kwa udini, utakuta ni watetetzi wakubwa wa CHADEMA! Si hilo, utakuta members wengi humu JF ambao Signatures zao ni vifungu vya Biblia, basi wengi wao kama sio wote ni watetezi wakubwa wa CHADEMA! Mara nyingi member hawa hata michango yao utakuta inaegemea zaidi kwenye udini udini kuliko Siasa za kawaida hata kama hoja inayojadiliwa ni ya kisiasa! Members hawa, wanatia kinyaa na wanachangia kwa kiasi kikubwa kuifanya CHADEMA ionekane dhahiri ni chama cha Wakristo!
Harakati za CHADEMA nazo zinazua mashaka mengine! Hata uendaji wa Kusini hivi sasa unaonekana ni kama tu katika kuzima kelele za wapinzani wao kwamba CHADEMA ni chama cha kikanda na chama cha Wakristo! Mbwembwe za CHADEMA kwenda kusini hazijaanza leo….na hata kama wataenda bado hawana hamasa kiasi hicho! Molemo, ametuletea habari za gazeti la Majira…..CHADEMA tuliowazoea si wa kusuiri Majira waandike stori kisha waje hapa kui-paste! Safari, imekosa hamasa!
Kama ilivyo ugumu kwa CUF kukubalika Bara ndivyo hivyo hivyo CHADEMA watakavyopata ugumu wa kukubalika Pwani ingawaje wapo wapumbavu watakaosema kwamba watu wa pwani hawana uelewa! Yaani leo hii Mmasasi ambae anaishi kwa kuhamahama awe na uelewa kuliko mtu aliye-settle sehemu moja!