CHADEMA yatoa tamko kuhusu msamaha wa Rais makosa ya uhujumu uchumi, ni haki au fedha?

Mkidakia ya Raisi wenu.. nawapendea jinsi mnajifunzia kuandika magazeti.. ila ikija juu ya haki, ufisadi, ubepari wa vyeo na demokrasia ndani ya chama chenu, hata sentensi ya maneno matatu hakuna kutokeza
Pengine usome tena mada.
Wametoa tamko kwa masilahi ya Taifa.
Siku utakuja tu kugundua kuwa, chama kitakufa na Taifa litaendelea, endelea kuchunguza mambo ya vyama na sinzia kabisa kwenye masuala ya Taifa.
 
Kwani umekuwaje!!!..
Amedakia au hajadakia?
 
N
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwasamehe watuhumiwa wenye makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha watakaokuwa tayari kuomba msamaha na ‘kurejesha’ fedha bila kuwa na hatia, si tu imethibitisha madai ya kuwepo uonevu mkubwa katika kile kilichoitwa vita dhidi ya ufisadi, bali pia inadhihirisha kuwa watuhumiwa hao wanastahili haki, uhuru wao bila masharti na waombwe samahani, badala ya wao kuomba.

Kitendo cha Rais John Magufuli kumuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia siku saba, kuzungumza na watuhumiwa hao ili walio tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha wasamehewe, wakishindwa (watakaoshindwa) waendelee kubanwa na kesi hata kama ni muda mrefu (miaka ishirini), inaibua masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na;

1. Kuthibitisha kauli na madai ya watu na makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo Chadema, ambayo mara kadhaa kupitia majukwaa mbalimbali imetoa kauli kuwa vita iliyokuwa inaendeshwa na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani, kwa jina la mapambano dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, ililenga kuwaonea baadhi ya watu, kuwabambikia makosa makubwa kwa nia ya kuwakamua fedha au hata kuwafilisi kwa hila.

2. Serikali kupitia vyombo vyake imeshindwa kuthibitisha makosa ya watuhumiwa hao, hivyo imeamua kutafuta njia ya kuepukana na aibu hiyo huku ikitaka kupata sifa za kisiasa mbele ya umma kwa gharama za haki na uhuru wa watu ambao wamekaa mahabusu bila hatia yoyote. Serikali yoyote makini, inayopambana na ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na makosa au uovu mwingine katika jamii, kwa kuweka mbele misingi ya haki, sheria na utawala bora, haiwezi kuagiza watuhumiwa waombe msamaha na kurejesha fedha kwa tuhuma ambazo ukweli wake haujathibitishwa na mahakama. Kwa sababu huko ni kuwaadhibu bila kuwa na hatia.

3. Kikatiba na Kisheria, Rais anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa, kwa maana ya watu ambao tuhuma zao zimethibitishwa mahakamani, lakini hana mamlaka ya Kikatiba wala Kisheria kuagiza msamaha au kusamehe watuhumiwa wa makosa yoyote yale.

4. Kesi za watuhumiwa ambao Rais John Magufuli ameagiza wasamehewe au aliowasamehe bado ziko mahakamani, zikifuata utaratibu wa kimahakama na watuhumiwa bado hawajapatikana na hatia. Kitendo cha Rais kuagiza wasamehewe huku akielekeza muda wa mazungumzo ya kuomba msamaha na kurejesha fedha, moja kwa moja kinaingilia uhuru wa Mhimili wa Mahakama, kwa sababu kinaelekeza hadi upangaji wa kesi hizo ili waweze kuachiwa ndani ya siku saba zinazoanza leo. Wakati huo huo mahakama ikielekezwa kutumia ‘muda mrefu’ kumaliza mashauri ya wale wote watakaoshindwa kuomba msamaha au kurudisha fedha.

5. Je, utaratibu huo wa Rais John Magufuli utaweza kuwafikia watuhumiwa wa makosa mengine, mathalani tuhuma za mauaji, ubakaji au ugaidi, badala ya sasa kuonekana umeelekezwa kwa watuhumiwa wa makosa yanayohusu uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pekee (yanayohusisha fedha), ili kuondoa dhana kwamba serikali inataka kutumia makosa hayo kufanya mabadilishano (biashara) ya haki na fedha kwa watu ambao wanapaswa kuombwa msamaha baada ya kubambikiwa kesi na kuwekwa mahabusu bila kuwa na hatia.

6. Je, huruma hiyo ya Rais John Magufuli inawafikiaje watuhumiwa wa makosa ya kisiasa, ambapo watu wengi mamia kwa mamia, wapinzani wa CCM na utawala wa Rais John Magufuli, kuanzia Viongozi Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa ngazi za chini, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wanaharakati wa masuala ya haki, demokrasia na utawala bora, wasanii na wananchi wa kawaida wanaokosoa au kutoa maoni yao (kupitia njia mbalimbali; mikutano ya hadhara, mikutano ya kampeni, sanaa, vyombo vya habari na mitandaoni) wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kinyume cha sheria na kufunguliwa kesi nyingi (wengine wamefungwa) kwa tuhuma za uchochezi, makosa ya mtandao, maandamano au mikusanyiko inayodaiwa si halali.

7. Uhuru wa Mkurugenzi wa Mashtaka unawekwa kitanzini. Katiba ya Nchi. Ibara ya 59B(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2005, inaweka misingi ya uhuru wa ofisi hiyo inapokuwa inatekeleza kazi zake, kwamba; *_“Katika kutekeleza mamlaka yake, Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki; (b) kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki; na (c) maslahi ya umma.”_* Pamoja na kutambua kuwa ni wajibu wa DPP kufungua au kufuta mashtaka, ni muhimu kuelewa kuwa, kwa mujibu wa ibara hiyo, Rais hana mamlaka ya kumfundisha kazi wala kumwelekeza wala kuingilia majukumu ya DPP, ambaye anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa uhuru akizingatia masharti yaliyowekwa bayana na Katiba ya Nchi.

Kimsingi, Chadema haikubaliani na utaratibu wa Serikali ya CCM wa kuonea watu, kama Rais John Magufuli anataka kuonekana mwenye huruma na nia yake njema isiibue sintofahamu nyingine kuhusu utendekaji wa haki nchini, hatma ya demokrasia na utawala bora, Chadema inashauri ifuatavyo;

1. Kwa kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, kumetungwa sheria zenye makosa mengi yasiyokuwa na dhamana, iwapo Rais ana huruma ya dhati kwa wananchi wote, Serikali yake ifanye mabadiliko ya sheria, ili makosa yote yawe na dhamana na watu wasikilize kesi zao wakiwa uraiani kwa sababu lengo la dhamana ni kumpata mtuhumiwa awepo pale anapohitajika.

2. Viongozi wa Serikali au vyombo vyake, wajiepushe kuvunja misingi ya utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Mojawapo ya msingi muhimu ni dhana ya kila mtu kuchukuliwa hana hatia hadi itakapothibitishwa hivyo na mamlaka zenye wajibu huo kisheria. Kuwataka watu waombe samahani na kurejesha fedha, wakati hawana makosa, ili waachiwe, ni kuondoa dhana hiyo ya *‘presumption of innocence’.*

3. Serikali iimarishe mifumo ya utoaji haki hasa kwa;

(i) Kutunga sheria itakayoelekeza vyombo husika kutomfikisha mtuhumiwa mahakamani na kumfungulia mashtaka kwa kosa ambalo halina dhamana, bila upelelezi kuwa umekamilika. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kesi nyingi, hasa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kuchukua muda mrefu kuanza kusikilizwa kwa kisingizio cha ‘upelelezi’ haujakamilika, huku watuhumiwa wakisota mahabusu.

(ii) Kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa wa mamlaka za ukamataji na uchunguzi, hususan katika kesi zinazohusishwa na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, ambapo kumekuwa na vyombo vingine, zaidi ya Jeshi la Polisi, vinavyokamata watu (mf; TAKUKURU, TRA, SUMATRA, etc) kisha wanahifadhiwa vituo vya polisi huku jeshi hilo likitoa kauli kuwa halihusiki na watuhumiwa hao (kuwakamata wala kupeleleza kesi zao) isipokuwa limepewa kuwahifadhi tu.

4. Ni vyema na wakati mwafaka sasa, Rais John Magufuli akaagiza uwajibikaji wa watu au vyombo vya kiserikali vilivyohusika kuwakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao ambao Serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma zao. Hii itaondoa utata mwingine ambao umesababishwa na kauli yake ya jana, kwamba watu hao wasiokuwa na hatia wakiomba msamaha, wakarejesha fedha, wakasamehewa, inaishia hapo? Vipi kuhusu wale wote waliohusika katika kuwakamata na kuwafungulia tuhuma za uongo na kuwanyima haki yao ya kuwa raia huru uraiani?

5. Serikali itoe orodha ya watuhumiwa wote wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inaowashikilia mahabusu za polisi na magereza, kesi wanazoshtakiwa nazo na thamani ya fedha wanazotuhumiwa kuhujumu au kutakatisha. Hii itasaidia kujua kiwango cha huruma iliyotolewa na Rais John Magufuli na ukubwa wa tatizo la uonevu katika mfumo wa utoaji haki na sheria nchini, hasa kwa kutumia kesi za mashtaka hayo.

*Hitimisho*

Chadema inasisitiza kuwa hakuna mbadala wa haki wala uhuru wa mtu pale unapokuwa umepokwa au kuminywa kwa namna yoyote ile, ikiwemo kesi za hila na kubambikiwa. Hivyo si sahihi kutumia unyonge na madhira ya watuhumiwa walioko mahabusu, kufanya nao (biashara) makubaliano ambayo yatajenga msingi kwamba haki yao imepatikana na uhuru wao kurejeshwa kwa sababu wametoa fedha.

Hivyo basi, kwa kuwa Serikali imeonekana kushindwa kuthibitisha tuhuma za watuhumiwa hao na mojawapo ya sababu kubwa ni kuwa tuhuma zinazowakabili wengi wa washtakiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni za kubambikiziwa, na wengi wao wamekaa muda mrefu mahabusu huku kesi zao zikisuasua kwa upelelezi kutokamilika, wasiadhibiwe kwa mtindo wa kupewa masharti kama ilivyoagizwa na Rais, bali DPP atekeleze wajibu wake wa Kikatiba na Kisheria ili watu hao watendewe haki na kuachiwa. Katika misingi ya haki, ubinadamu na utu, wao ndiyo wanastahili kuombwa samahani.

Imetolewa leo Jumatatu, Septemba 23, 2019 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Ndugu zangu wana Chadema tusameheane mda huu tunaenda kwenye uchaguzi nyinyi mnavyobana kwa program yenu yachadema ni msingi sisi Kama CCM mnataka tujinasue vip tuacheni tusake pesa ya kampeni bana
 
Kuna point umeelezea vizuri kuhusu uharakishwaji wa upelelezi wa kesi hizo pamoja na adhabu stahiki za wale wote wanaobainika kubambikia wenzao kesi hizo nzito zisizo na dhamana.

Lakini haujaongelea lolote kuhusu hatua stahiki kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa kweli, wafanywe nini kwa mawazo yako hayo.

Pale kuna kamchanganyikeni ya watuhumiwa, lakini wote umewa include kwenye ubambikiwaji tu wa kesi kisha ukafunga na thread!

Ujumla jumla huu wa mawazo, ndiyo unaoleta dhana kuwa 'upinzani wa Tz ni kupinga kila kitu'.
Kama wapo watuhumiwa wenye makosa, kwa nini hayo makosa mpaka leo hayajathibitishwa mahakamani? Serikali kila mara inasema upelelezi haujakamilika, utakamilika lini?

Ameeleza vizuri, sheria zibadilishwe. Watuhumiwa wapewe dhamana, wataenda magerezani au kupewa msamaha wa Rais watakapokuwa wamehukumiwa na mahakama.
 
Kuna point umeelezea vizuri kuhusu uharakishwaji wa upelelezi wa kesi hizo pamoja na adhabu stahiki za wale wote wanaobainika kubambikia wenzao kesi hizo nzito zisizo na dhamana.

Lakini haujaongelea lolote kuhusu hatua stahiki kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa kweli, wafanywe nini kwa mawazo yako hayo.

Pale kuna kamchanganyikeni ya watuhumiwa, lakini wote umewa include kwenye ubambikiwaji tu wa kesi kisha ukafunga na thread!

Ujumla jumla huu wa mawazo, ndiyo unaoleta dhana kuwa 'upinzani wa Tz ni kupinga kila kitu'.
Wahujimu wa kweli wa uchumi adhabu yao c inajulikana pimbi ww
 
Asante CDM neno. Haki daima hailinganishwi ma vipande vya pesa.Zoezi hilo ni biashara haramu na batili,halina uhalali wala sifa kuitwa kodi.
 
tangu mwazo niliamini kuwa hii vita dhidi ya ufisadi ni nguvu ya soda kwani halikuwa la mkakati na hatukuwa na mfumo badala yake ilikuwa ni umaarufu tu unatafutwa.Kibaya zaidi kuna chembe cha za chukikwa baadhi ya watuhumiwa.
 
Kuna point umeelezea vizuri kuhusu uharakishwaji wa upelelezi wa kesi hizo pamoja na adhabu stahiki za wale wote wanaobainika kubambikia wenzao kesi hizo nzito zisizo na dhamana.

Lakini haujaongelea lolote kuhusu hatua stahiki kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa kweli, wafanywe nini kwa mawazo yako hayo.

Pale kuna kamchanganyikeni ya watuhumiwa, lakini wote umewa include kwenye ubambikiwaji tu wa kesi kisha ukafunga na thread!

Ujumla jumla huu wa mawazo, ndiyo unaoleta dhana kuwa 'upinzani wa Tz ni kupinga kila kitu'.
Asante sana Mh. Makene. Imenena vyema. Vipi makosa madogo kama mwizi wa kuku - nae anaweza kuomba msamaha, akalipa ile.kuku halafu akasa
Kwa hiyo uchaguzi wa Mwenyekiti ni uhujumu uchumi?
Hah hah hah! Huwa nafurahi sana kuyasikia maCCM yakiweweseka na Mbowe! Ukisikia yanasema mbona hamfanyi uchaguzi mpate M/Kiti mwingine ujue yanaweweseka! Hah hah hah
 
Kuna point umeelezea vizuri kuhusu uharakishwaji wa upelelezi wa kesi hizo pamoja na adhabu stahiki za wale wote wanaobainika kubambikia wenzao kesi hizo nzito zisizo na dhamana.

Lakini haujaongelea lolote kuhusu hatua stahiki kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa kweli, wafanywe nini kwa mawazo yako hayo.

Pale kuna kamchanganyikeni ya watuhumiwa, lakini wote umewa include kwenye ubambikiwaji tu wa kesi kisha ukafunga na thread!

Ujumla jumla huu wa mawazo, ndiyo unaoleta dhana kuwa 'upinzani wa Tz ni kupinga kila kitu'.
Wewe ni mjinga soma tena utaelewa!
 
si hawajalazimishwa ama?
kama anadhani ana haki wakomae..
kilichoombwa ni confession kama ulifanya kosa.
Serikali imeshindwa kuthibitisha makosa sasa wanataka watuhumiwa wajitie kitanzi wenyewe kujichafulia CV zao! iweje mtu kama Ruge aliyeuza kampuni yake VIP umshitaki kwa kutakatisha pesa au ufisadi wakati walioidhinisha pesa kutoka kwenye escrow account wapo kitaa wanapeta?!
Dhambi ya dhuluma na uonevu haitokaa kamwe iwaache salama! Watanzania sio wajinga.
 
hata hao utaratibu uko wazi wakiamua ku confess huwa wanapewa hukumu ndogo..
Hakika CHADEMA ni Chama makini...

Itakuwaje msamaha uwe Kwa "watuhumiwa" wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha tu, tena msamaha huo uwe ni baada yakurudisha/kubadilishana na fedha (barter trade)?

Lakini je vipi kwao walotuhimiwa Kwa makosa mengine kama wizi, maandamano, kesi za kisiasa nk? Maana hao nao ni "watuhumiwa" ambao makosa yao bado hayaja thibitishwa na Mahakama, je wanawekwa wapi hawa?

Wema huu si lolote zaidi ya kutafuta huruma za wananchi na mkwamo wa Ukata uliopo serikalini kwasasa !!
 
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwasamehe watuhumiwa wenye makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha watakaokuwa tayari kuomba msamaha na ‘kurejesha’ fedha bila kuwa na hatia, si tu imethibitisha madai ya kuwepo uonevu mkubwa katika kile kilichoitwa vita dhidi ya ufisadi, bali pia inadhihirisha kuwa watuhumiwa hao wanastahili haki, uhuru wao bila masharti na waombwe samahani, badala ya wao kuomba.

Kitendo cha Rais John Magufuli kumuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia siku saba, kuzungumza na watuhumiwa hao ili walio tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha wasamehewe, wakishindwa (watakaoshindwa) waendelee kubanwa na kesi hata kama ni muda mrefu (miaka ishirini), inaibua masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na;

1. Kuthibitisha kauli na madai ya watu na makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo Chadema, ambayo mara kadhaa kupitia majukwaa mbalimbali imetoa kauli kuwa vita iliyokuwa inaendeshwa na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani, kwa jina la mapambano dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, ililenga kuwaonea baadhi ya watu, kuwabambikia makosa makubwa kwa nia ya kuwakamua fedha au hata kuwafilisi kwa hila.

2. Serikali kupitia vyombo vyake imeshindwa kuthibitisha makosa ya watuhumiwa hao, hivyo imeamua kutafuta njia ya kuepukana na aibu hiyo huku ikitaka kupata sifa za kisiasa mbele ya umma kwa gharama za haki na uhuru wa watu ambao wamekaa mahabusu bila hatia yoyote. Serikali yoyote makini, inayopambana na ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na makosa au uovu mwingine katika jamii, kwa kuweka mbele misingi ya haki, sheria na utawala bora, haiwezi kuagiza watuhumiwa waombe msamaha na kurejesha fedha kwa tuhuma ambazo ukweli wake haujathibitishwa na mahakama. Kwa sababu huko ni kuwaadhibu bila kuwa na hatia.

3. Kikatiba na Kisheria, Rais anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa, kwa maana ya watu ambao tuhuma zao zimethibitishwa mahakamani, lakini hana mamlaka ya Kikatiba wala Kisheria kuagiza msamaha au kusamehe watuhumiwa wa makosa yoyote yale.

4. Kesi za watuhumiwa ambao Rais John Magufuli ameagiza wasamehewe au aliowasamehe bado ziko mahakamani, zikifuata utaratibu wa kimahakama na watuhumiwa bado hawajapatikana na hatia. Kitendo cha Rais kuagiza wasamehewe huku akielekeza muda wa mazungumzo ya kuomba msamaha na kurejesha fedha, moja kwa moja kinaingilia uhuru wa Mhimili wa Mahakama, kwa sababu kinaelekeza hadi upangaji wa kesi hizo ili waweze kuachiwa ndani ya siku saba zinazoanza leo. Wakati huo huo mahakama ikielekezwa kutumia ‘muda mrefu’ kumaliza mashauri ya wale wote watakaoshindwa kuomba msamaha au kurudisha fedha.

5. Je, utaratibu huo wa Rais John Magufuli utaweza kuwafikia watuhumiwa wa makosa mengine, mathalani tuhuma za mauaji, ubakaji au ugaidi, badala ya sasa kuonekana umeelekezwa kwa watuhumiwa wa makosa yanayohusu uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pekee (yanayohusisha fedha), ili kuondoa dhana kwamba serikali inataka kutumia makosa hayo kufanya mabadilishano (biashara) ya haki na fedha kwa watu ambao wanapaswa kuombwa msamaha baada ya kubambikiwa kesi na kuwekwa mahabusu bila kuwa na hatia.

6. Je, huruma hiyo ya Rais John Magufuli inawafikiaje watuhumiwa wa makosa ya kisiasa, ambapo watu wengi mamia kwa mamia, wapinzani wa CCM na utawala wa Rais John Magufuli, kuanzia Viongozi Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa ngazi za chini, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wanaharakati wa masuala ya haki, demokrasia na utawala bora, wasanii na wananchi wa kawaida wanaokosoa au kutoa maoni yao (kupitia njia mbalimbali; mikutano ya hadhara, mikutano ya kampeni, sanaa, vyombo vya habari na mitandaoni) wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kinyume cha sheria na kufunguliwa kesi nyingi (wengine wamefungwa) kwa tuhuma za uchochezi, makosa ya mtandao, maandamano au mikusanyiko inayodaiwa si halali.

7. Uhuru wa Mkurugenzi wa Mashtaka unawekwa kitanzini. Katiba ya Nchi. Ibara ya 59B(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2005, inaweka misingi ya uhuru wa ofisi hiyo inapokuwa inatekeleza kazi zake, kwamba; *_“Katika kutekeleza mamlaka yake, Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki; (b) kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki; na (c) maslahi ya umma.”_* Pamoja na kutambua kuwa ni wajibu wa DPP kufungua au kufuta mashtaka, ni muhimu kuelewa kuwa, kwa mujibu wa ibara hiyo, Rais hana mamlaka ya kumfundisha kazi wala kumwelekeza wala kuingilia majukumu ya DPP, ambaye anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa uhuru akizingatia masharti yaliyowekwa bayana na Katiba ya Nchi.

Kimsingi, Chadema haikubaliani na utaratibu wa Serikali ya CCM wa kuonea watu, kama Rais John Magufuli anataka kuonekana mwenye huruma na nia yake njema isiibue sintofahamu nyingine kuhusu utendekaji wa haki nchini, hatma ya demokrasia na utawala bora, Chadema inashauri ifuatavyo;

1. Kwa kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, kumetungwa sheria zenye makosa mengi yasiyokuwa na dhamana, iwapo Rais ana huruma ya dhati kwa wananchi wote, Serikali yake ifanye mabadiliko ya sheria, ili makosa yote yawe na dhamana na watu wasikilize kesi zao wakiwa uraiani kwa sababu lengo la dhamana ni kumpata mtuhumiwa awepo pale anapohitajika.

2. Viongozi wa Serikali au vyombo vyake, wajiepushe kuvunja misingi ya utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Mojawapo ya msingi muhimu ni dhana ya kila mtu kuchukuliwa hana hatia hadi itakapothibitishwa hivyo na mamlaka zenye wajibu huo kisheria. Kuwataka watu waombe samahani na kurejesha fedha, wakati hawana makosa, ili waachiwe, ni kuondoa dhana hiyo ya *‘presumption of innocence’.*

3. Serikali iimarishe mifumo ya utoaji haki hasa kwa;

(i) Kutunga sheria itakayoelekeza vyombo husika kutomfikisha mtuhumiwa mahakamani na kumfungulia mashtaka kwa kosa ambalo halina dhamana, bila upelelezi kuwa umekamilika. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kesi nyingi, hasa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kuchukua muda mrefu kuanza kusikilizwa kwa kisingizio cha ‘upelelezi’ haujakamilika, huku watuhumiwa wakisota mahabusu.

(ii) Kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa wa mamlaka za ukamataji na uchunguzi, hususan katika kesi zinazohusishwa na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, ambapo kumekuwa na vyombo vingine, zaidi ya Jeshi la Polisi, vinavyokamata watu (mf; TAKUKURU, TRA, SUMATRA, etc) kisha wanahifadhiwa vituo vya polisi huku jeshi hilo likitoa kauli kuwa halihusiki na watuhumiwa hao (kuwakamata wala kupeleleza kesi zao) isipokuwa limepewa kuwahifadhi tu.

4. Ni vyema na wakati mwafaka sasa, Rais John Magufuli akaagiza uwajibikaji wa watu au vyombo vya kiserikali vilivyohusika kuwakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao ambao Serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma zao. Hii itaondoa utata mwingine ambao umesababishwa na kauli yake ya jana, kwamba watu hao wasiokuwa na hatia wakiomba msamaha, wakarejesha fedha, wakasamehewa, inaishia hapo? Vipi kuhusu wale wote waliohusika katika kuwakamata na kuwafungulia tuhuma za uongo na kuwanyima haki yao ya kuwa raia huru uraiani?

5. Serikali itoe orodha ya watuhumiwa wote wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inaowashikilia mahabusu za polisi na magereza, kesi wanazoshtakiwa nazo na thamani ya fedha wanazotuhumiwa kuhujumu au kutakatisha. Hii itasaidia kujua kiwango cha huruma iliyotolewa na Rais John Magufuli na ukubwa wa tatizo la uonevu katika mfumo wa utoaji haki na sheria nchini, hasa kwa kutumia kesi za mashtaka hayo.

*Hitimisho*

Chadema inasisitiza kuwa hakuna mbadala wa haki wala uhuru wa mtu pale unapokuwa umepokwa au kuminywa kwa namna yoyote ile, ikiwemo kesi za hila na kubambikiwa. Hivyo si sahihi kutumia unyonge na madhira ya watuhumiwa walioko mahabusu, kufanya nao (biashara) makubaliano ambayo yatajenga msingi kwamba haki yao imepatikana na uhuru wao kurejeshwa kwa sababu wametoa fedha.

Hivyo basi, kwa kuwa Serikali imeonekana kushindwa kuthibitisha tuhuma za watuhumiwa hao na mojawapo ya sababu kubwa ni kuwa tuhuma zinazowakabili wengi wa washtakiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni za kubambikiziwa, na wengi wao wamekaa muda mrefu mahabusu huku kesi zao zikisuasua kwa upelelezi kutokamilika, wasiadhibiwe kwa mtindo wa kupewa masharti kama ilivyoagizwa na Rais, bali DPP atekeleze wajibu wake wa Kikatiba na Kisheria ili watu hao watendewe haki na kuachiwa. Katika misingi ya haki, ubinadamu na utu, wao ndiyo wanastahili kuombwa samahani.

Imetolewa leo Jumatatu, Septemba 23, 2019 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Kuna ile tabia ya kuwabambikia makosa mengi mfano utasikia mtuhumiwa ana makoa 350 au 500 au zaidi, wanaweka idadi kubwa ya mashitaka kwa kosa moja au mawili, utitiri wa kesi tofauti ni sentesi tu, wanawalundikia makosa kibao kwa nia ya kuwachanganya kisakologia
 
Back
Top Bottom