CHADEMA yatoa tamko kuhusu msamaha wa Rais makosa ya uhujumu uchumi, ni haki au fedha?

CHADEMA kazi yao ni kupinga tu kila kitu sishangai
Acha ushamba kwani hujui kuwa kazi ya upinzani ni kuikosoa Serikali? Upinzani lazima upinge mapungufu yote pasipo kuyabagua, usitegemee wapinzani kuwafagilia kwa lolote baya
 
Duh hawa Chadema hawa...
P
Mtu amekaa jela miaka minne (4) hakuna ushahidi tuhuma zake haziendani hata na mali anazomiliki na yule aliyembambikia kesi yupo anadunda ofisini, hii imekaaje? wewe Paskal mayala si ni Mwanasheria ifafanue hii mtu akikubambikia kesi kisha ikaja kuonekana huna makosa je? aliyekubambikia kesi unaweza kumshitaki kumdai fidia?
 
Tumaini Makene

MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE TAFADHALI MPENI, Mh. Rais hakuagiza alitoa ushauri with bolded disclaimer ANGALIENI SHERIA INASEMAJE NA PIA SITAKI IONEKANE KWAMBA NAINGILUA MUHIMILI MWINGINE"

Nabii Issa Alllah Salaam alipoletewa ile kesi ya MWANAMKE MWASHERATI AKAAM IWA HUYU MZINIFU TUMPIGE MAWE KWAKUA MUSSA ALITUAGIZA VIVYO ALISEMA" asiyekua na dhambi awe wa Kwanza kumpiga jiwe.

A.HAKUSEMA KWAMBA ALICHOSEMA MUSSA NI KOSA NA

B. Hakusema msimpige kwakua hivyo utata uliopo hapo ni kwamba sheria kama inaruhusu sawa au waangalie kama, kufanya vivyo ni sahihi.

Mr. Makene.
Ni lini mtaacha siasa za kudandia matukio ambayo yanashusha credibility ya chama.

Hivi hata kama ni kupinga si kwa staili yenye kuchusha na kukwaza.

Suala hili nyeti sana; it borders on extortion au uharamia. Rais hakustahili kulizungumzia kwa namna alivyofanya. The intention is evil through and through. Muhimu zaidi ni kwambà mara tu baada ya kauli ya rais DPP wakaanza utekelezaji; suggesting kuwa alishapata hayo maelekezo kabla ya hicho kinachodaiwa ni ushauri au mapendekezo ya rais!
 
Kwanza hoja zenu Batili. Chama Hakuna viongozi. Pili. Rais alishauri. So shut up and fanyeni uchaguzi.

Ushauri? Rais anawezaje kutoa ushauri wa ajabu kiasi hiki? Tunavyojua sisi Rais mwenyewe ni mtu wa kushauriwa all the time; anawezaje yeye kushauri badala ya kushauriwa?
 
CHADEMA na viongozi wao kama Mnyika, Lema et al kutwa walikuwa vinara wakuwaita hao watu wanaodai leo kesi zao ni za kisiasa yakuwa ni mafisadi.

Kukosekana kwa ushahidi wa hizo kesi ni bora kukaa kimya au wasaidie serikari kupata huo ushahidi kuliko kutoa matamko.

Kwa tamko hili wanaonyesha extent ya unafiki wao na kutosimamia kile wanachoamini.

Waswahili wanamsemo ‘njia ya mtu muongo ni fupi’ mara hii washasahau msimamo wao juu ya hao watu.

Nonsense!
 
Mkuu kwa uzoefu wa nchi yetu na matundu ya kikatiba yaliyopo,ushauri wa rais ni maagizo 100% na ukitaka kujua hilo angalia anachoshauri lazma kitekelezwe hata kama ni kinyume na katiba.

Rais hashauri hata siku moja; yeye ndiye hushauriwa. The moment anaanza kushauri badala ya kushauriwa ujue lolote inaweza kutokea.
 
Chadema itoe kauai kali dhidi ya Mbowe kung'ang'ania Madaraka.
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwasamehe watuhumiwa wenye makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha watakaokuwa tayari kuomba msamaha na ‘kurejesha’ fedha bila kuwa na hatia, si tu imethibitisha madai ya kuwepo uonevu mkubwa katika kile kilichoitwa vita dhidi ya ufisadi, bali pia inadhihirisha kuwa watuhumiwa hao wanastahili haki, uhuru wao bila masharti na waombwe samahani, badala ya wao kuomba.

Kitendo cha Rais John Magufuli kumuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia siku saba, kuzungumza na watuhumiwa hao ili walio tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha wasamehewe, wakishindwa (watakaoshindwa) waendelee kubanwa na kesi hata kama ni muda mrefu (miaka ishirini), inaibua masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na;

1. Kuthibitisha kauli na madai ya watu na makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo Chadema, ambayo mara kadhaa kupitia majukwaa mbalimbali imetoa kauli kuwa vita iliyokuwa inaendeshwa na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani, kwa jina la mapambano dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, ililenga kuwaonea baadhi ya watu, kuwabambikia makosa makubwa kwa nia ya kuwakamua fedha au hata kuwafilisi kwa hila.

2. Serikali kupitia vyombo vyake imeshindwa kuthibitisha makosa ya watuhumiwa hao, hivyo imeamua kutafuta njia ya kuepukana na aibu hiyo huku ikitaka kupata sifa za kisiasa mbele ya umma kwa gharama za haki na uhuru wa watu ambao wamekaa mahabusu bila hatia yoyote. Serikali yoyote makini, inayopambana na ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na makosa au uovu mwingine katika jamii, kwa kuweka mbele misingi ya haki, sheria na utawala bora, haiwezi kuagiza watuhumiwa waombe msamaha na kurejesha fedha kwa tuhuma ambazo ukweli wake haujathibitishwa na mahakama. Kwa sababu huko ni kuwaadhibu bila kuwa na hatia.

3. Kikatiba na Kisheria, Rais anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa, kwa maana ya watu ambao tuhuma zao zimethibitishwa mahakamani, lakini hana mamlaka ya Kikatiba wala Kisheria kuagiza msamaha au kusamehe watuhumiwa wa makosa yoyote yale.

4. Kesi za watuhumiwa ambao Rais John Magufuli ameagiza wasamehewe au aliowasamehe bado ziko mahakamani, zikifuata utaratibu wa kimahakama na watuhumiwa bado hawajapatikana na hatia. Kitendo cha Rais kuagiza wasamehewe huku akielekeza muda wa mazungumzo ya kuomba msamaha na kurejesha fedha, moja kwa moja kinaingilia uhuru wa Mhimili wa Mahakama, kwa sababu kinaelekeza hadi upangaji wa kesi hizo ili waweze kuachiwa ndani ya siku saba zinazoanza leo. Wakati huo huo mahakama ikielekezwa kutumia ‘muda mrefu’ kumaliza mashauri ya wale wote watakaoshindwa kuomba msamaha au kurudisha fedha.

5. Je, utaratibu huo wa Rais John Magufuli utaweza kuwafikia watuhumiwa wa makosa mengine, mathalani tuhuma za mauaji, ubakaji au ugaidi, badala ya sasa kuonekana umeelekezwa kwa watuhumiwa wa makosa yanayohusu uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pekee (yanayohusisha fedha), ili kuondoa dhana kwamba serikali inataka kutumia makosa hayo kufanya mabadilishano (biashara) ya haki na fedha kwa watu ambao wanapaswa kuombwa msamaha baada ya kubambikiwa kesi na kuwekwa mahabusu bila kuwa na hatia.

6. Je, huruma hiyo ya Rais John Magufuli inawafikiaje watuhumiwa wa makosa ya kisiasa, ambapo watu wengi mamia kwa mamia, wapinzani wa CCM na utawala wa Rais John Magufuli, kuanzia Viongozi Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa ngazi za chini, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wanaharakati wa masuala ya haki, demokrasia na utawala bora, wasanii na wananchi wa kawaida wanaokosoa au kutoa maoni yao (kupitia njia mbalimbali; mikutano ya hadhara, mikutano ya kampeni, sanaa, vyombo vya habari na mitandaoni) wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kinyume cha sheria na kufunguliwa kesi nyingi (wengine wamefungwa) kwa tuhuma za uchochezi, makosa ya mtandao, maandamano au mikusanyiko inayodaiwa si halali.

7. Uhuru wa Mkurugenzi wa Mashtaka unawekwa kitanzini. Katiba ya Nchi. Ibara ya 59B(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2005, inaweka misingi ya uhuru wa ofisi hiyo inapokuwa inatekeleza kazi zake, kwamba; *_“Katika kutekeleza mamlaka yake, Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki; (b) kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki; na (c) maslahi ya umma.”_* Pamoja na kutambua kuwa ni wajibu wa DPP kufungua au kufuta mashtaka, ni muhimu kuelewa kuwa, kwa mujibu wa ibara hiyo, Rais hana mamlaka ya kumfundisha kazi wala kumwelekeza wala kuingilia majukumu ya DPP, ambaye anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa uhuru akizingatia masharti yaliyowekwa bayana na Katiba ya Nchi.

Kimsingi, Chadema haikubaliani na utaratibu wa Serikali ya CCM wa kuonea watu, kama Rais John Magufuli anataka kuonekana mwenye huruma na nia yake njema isiibue sintofahamu nyingine kuhusu utendekaji wa haki nchini, hatma ya demokrasia na utawala bora, Chadema inashauri ifuatavyo;

1. Kwa kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, kumetungwa sheria zenye makosa mengi yasiyokuwa na dhamana, iwapo Rais ana huruma ya dhati kwa wananchi wote, Serikali yake ifanye mabadiliko ya sheria, ili makosa yote yawe na dhamana na watu wasikilize kesi zao wakiwa uraiani kwa sababu lengo la dhamana ni kumpata mtuhumiwa awepo pale anapohitajika.

2. Viongozi wa Serikali au vyombo vyake, wajiepushe kuvunja misingi ya utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Mojawapo ya msingi muhimu ni dhana ya kila mtu kuchukuliwa hana hatia hadi itakapothibitishwa hivyo na mamlaka zenye wajibu huo kisheria. Kuwataka watu waombe samahani na kurejesha fedha, wakati hawana makosa, ili waachiwe, ni kuondoa dhana hiyo ya *‘presumption of innocence’.*

3. Serikali iimarishe mifumo ya utoaji haki hasa kwa;

(i) Kutunga sheria itakayoelekeza vyombo husika kutomfikisha mtuhumiwa mahakamani na kumfungulia mashtaka kwa kosa ambalo halina dhamana, bila upelelezi kuwa umekamilika. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kesi nyingi, hasa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kuchukua muda mrefu kuanza kusikilizwa kwa kisingizio cha ‘upelelezi’ haujakamilika, huku watuhumiwa wakisota mahabusu.

(ii) Kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa wa mamlaka za ukamataji na uchunguzi, hususan katika kesi zinazohusishwa na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, ambapo kumekuwa na vyombo vingine, zaidi ya Jeshi la Polisi, vinavyokamata watu (mf; TAKUKURU, TRA, SUMATRA, etc) kisha wanahifadhiwa vituo vya polisi huku jeshi hilo likitoa kauli kuwa halihusiki na watuhumiwa hao (kuwakamata wala kupeleleza kesi zao) isipokuwa limepewa kuwahifadhi tu.

4. Ni vyema na wakati mwafaka sasa, Rais John Magufuli akaagiza uwajibikaji wa watu au vyombo vya kiserikali vilivyohusika kuwakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao ambao Serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma zao. Hii itaondoa utata mwingine ambao umesababishwa na kauli yake ya jana, kwamba watu hao wasiokuwa na hatia wakiomba msamaha, wakarejesha fedha, wakasamehewa, inaishia hapo? Vipi kuhusu wale wote waliohusika katika kuwakamata na kuwafungulia tuhuma za uongo na kuwanyima haki yao ya kuwa raia huru uraiani?

5. Serikali itoe orodha ya watuhumiwa wote wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inaowashikilia mahabusu za polisi na magereza, kesi wanazoshtakiwa nazo na thamani ya fedha wanazotuhumiwa kuhujumu au kutakatisha. Hii itasaidia kujua kiwango cha huruma iliyotolewa na Rais John Magufuli na ukubwa wa tatizo la uonevu katika mfumo wa utoaji haki na sheria nchini, hasa kwa kutumia kesi za mashtaka hayo.

*Hitimisho*

Chadema inasisitiza kuwa hakuna mbadala wa haki wala uhuru wa mtu pale unapokuwa umepokwa au kuminywa kwa namna yoyote ile, ikiwemo kesi za hila na kubambikiwa. Hivyo si sahihi kutumia unyonge na madhira ya watuhumiwa walioko mahabusu, kufanya nao (biashara) makubaliano ambayo yatajenga msingi kwamba haki yao imepatikana na uhuru wao kurejeshwa kwa sababu wametoa fedha.

Hivyo basi, kwa kuwa Serikali imeonekana kushindwa kuthibitisha tuhuma za watuhumiwa hao na mojawapo ya sababu kubwa ni kuwa tuhuma zinazowakabili wengi wa washtakiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni za kubambikiziwa, na wengi wao wamekaa muda mrefu mahabusu huku kesi zao zikisuasua kwa upelelezi kutokamilika, wasiadhibiwe kwa mtindo wa kupewa masharti kama ilivyoagizwa na Rais, bali DPP atekeleze wajibu wake wa Kikatiba na Kisheria ili watu hao watendewe haki na kuachiwa. Katika misingi ya haki, ubinadamu na utu, wao ndiyo wanastahili kuombwa samahani.

Imetolewa leo Jumatatu, Septemba 23, 2019 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
 
Huyo kiziwi atawasikia kweli serikali yake imefirisika hana hata fedha za kulipa mishahara wafanyakazi mwezi huu kweli zero ni zero tu
 
Tanesco wameshindwa kesi kule Hongkong Serikali inatakiwa kulipa mabilioni ndiyo wanahaha sasa
 
Namkumbuka lissu na fatma Karume
Message sent!!!

Bahati mbaya, wapinzani hawapewi coverage ya kutosha na media kama bwana yule anavyopewa ila mitandao itasaidia kufikisha ujumbe huyu kadri iwezekanavyo.

Unamtia ndani Seth na Ruge huku waliowapa hela kutoka zilikokuwa zimehifadhiwa wako uaraina wanapeta alafu unataka tuamini eti unapapambana na rushwa na ufisadi!!
 
Serikali imeshindwa kuthibitisha makosa sasa wanataka watuhumiwa wajitie kitanzi wenyewe kujichafulia CV zao! iweje mtu kama Ruge aliyeuza kampuni yake VIP umshitaki kwa kutakatisha pesa au ufisadi wakati walioidhinisha pesa kutoka kwenye escrow account wapo kitaa wanapeta?!
Dhambi ya dhuluma na uonevu haitokaa kamwe iwaache salama! Watanzania sio wajinga.
Wale wa escrow wapo kitaa wote pamoja na King of escrow.. Uwonevu tu
 
CHADEMA na viongozi wao kama Mnyika, Lema et al kutwa walikuwa vinara wakuwaita hao watu wanaodai leo kesi zao ni za kisiasa yakuwa ni mafisadi.

Kukosekana kwa ushahidi wa hizo kesi ni bora kukaa kimya au wasaidie serikari kupata huo ushahidi kuliko kutoa matamko.

Kwa tamko hili wanaonyesha extent ya unafiki wao na kutosimamia kile wanachoamini.

Waswahili wanamsemo ‘njia ya mtu muongo ni fupi’ mara hii washasahau msimamo wao juu ya hao watu.
Mnafiki ni yule anaeweka watu ndani alafu baadae anajidai kuwaonea huruma ili kupata kiki za kisiasa!!
 
ch
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwasamehe watuhumiwa wenye makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha watakaokuwa tayari kuomba msamaha na ‘kurejesha’ fedha bila kuwa na hatia, si tu imethibitisha madai ya kuwepo uonevu mkubwa katika kile kilichoitwa vita dhidi ya ufisadi, bali pia inadhihirisha kuwa watuhumiwa hao wanastahili haki, uhuru wao bila masharti na waombwe samahani, badala ya wao kuomba.

Kitendo cha Rais John Magufuli kumuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia siku saba, kuzungumza na watuhumiwa hao ili walio tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha wasamehewe, wakishindwa (watakaoshindwa) waendelee kubanwa na kesi hata kama ni muda mrefu (miaka ishirini), inaibua masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na;

1. Kuthibitisha kauli na madai ya watu na makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo Chadema, ambayo mara kadhaa kupitia majukwaa mbalimbali imetoa kauli kuwa vita iliyokuwa inaendeshwa na Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani, kwa jina la mapambano dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, ililenga kuwaonea baadhi ya watu, kuwabambikia makosa makubwa kwa nia ya kuwakamua fedha au hata kuwafilisi kwa hila.

2. Serikali kupitia vyombo vyake imeshindwa kuthibitisha makosa ya watuhumiwa hao, hivyo imeamua kutafuta njia ya kuepukana na aibu hiyo huku ikitaka kupata sifa za kisiasa mbele ya umma kwa gharama za haki na uhuru wa watu ambao wamekaa mahabusu bila hatia yoyote. Serikali yoyote makini, inayopambana na ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na makosa au uovu mwingine katika jamii, kwa kuweka mbele misingi ya haki, sheria na utawala bora, haiwezi kuagiza watuhumiwa waombe msamaha na kurejesha fedha kwa tuhuma ambazo ukweli wake haujathibitishwa na mahakama. Kwa sababu huko ni kuwaadhibu bila kuwa na hatia.

3. Kikatiba na Kisheria, Rais anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa, kwa maana ya watu ambao tuhuma zao zimethibitishwa mahakamani, lakini hana mamlaka ya Kikatiba wala Kisheria kuagiza msamaha au kusamehe watuhumiwa wa makosa yoyote yale.

4. Kesi za watuhumiwa ambao Rais John Magufuli ameagiza wasamehewe au aliowasamehe bado ziko mahakamani, zikifuata utaratibu wa kimahakama na watuhumiwa bado hawajapatikana na hatia. Kitendo cha Rais kuagiza wasamehewe huku akielekeza muda wa mazungumzo ya kuomba msamaha na kurejesha fedha, moja kwa moja kinaingilia uhuru wa Mhimili wa Mahakama, kwa sababu kinaelekeza hadi upangaji wa kesi hizo ili waweze kuachiwa ndani ya siku saba zinazoanza leo. Wakati huo huo mahakama ikielekezwa kutumia ‘muda mrefu’ kumaliza mashauri ya wale wote watakaoshindwa kuomba msamaha au kurudisha fedha.

5. Je, utaratibu huo wa Rais John Magufuli utaweza kuwafikia watuhumiwa wa makosa mengine, mathalani tuhuma za mauaji, ubakaji au ugaidi, badala ya sasa kuonekana umeelekezwa kwa watuhumiwa wa makosa yanayohusu uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pekee (yanayohusisha fedha), ili kuondoa dhana kwamba serikali inataka kutumia makosa hayo kufanya mabadilishano (biashara) ya haki na fedha kwa watu ambao wanapaswa kuombwa msamaha baada ya kubambikiwa kesi na kuwekwa mahabusu bila kuwa na hatia.

6. Je, huruma hiyo ya Rais John Magufuli inawafikiaje watuhumiwa wa makosa ya kisiasa, ambapo watu wengi mamia kwa mamia, wapinzani wa CCM na utawala wa Rais John Magufuli, kuanzia Viongozi Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa ngazi za chini, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wanaharakati wa masuala ya haki, demokrasia na utawala bora, wasanii na wananchi wa kawaida wanaokosoa au kutoa maoni yao (kupitia njia mbalimbali; mikutano ya hadhara, mikutano ya kampeni, sanaa, vyombo vya habari na mitandaoni) wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kinyume cha sheria na kufunguliwa kesi nyingi (wengine wamefungwa) kwa tuhuma za uchochezi, makosa ya mtandao, maandamano au mikusanyiko inayodaiwa si halali.

7. Uhuru wa Mkurugenzi wa Mashtaka unawekwa kitanzini. Katiba ya Nchi. Ibara ya 59B(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2005, inaweka misingi ya uhuru wa ofisi hiyo inapokuwa inatekeleza kazi zake, kwamba; *_“Katika kutekeleza mamlaka yake, Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki; (b) kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki; na (c) maslahi ya umma.”_* Pamoja na kutambua kuwa ni wajibu wa DPP kufungua au kufuta mashtaka, ni muhimu kuelewa kuwa, kwa mujibu wa ibara hiyo, Rais hana mamlaka ya kumfundisha kazi wala kumwelekeza wala kuingilia majukumu ya DPP, ambaye anapaswa kutekeleza wajibu wake kwa uhuru akizingatia masharti yaliyowekwa bayana na Katiba ya Nchi.

Kimsingi, Chadema haikubaliani na utaratibu wa Serikali ya CCM wa kuonea watu, kama Rais John Magufuli anataka kuonekana mwenye huruma na nia yake njema isiibue sintofahamu nyingine kuhusu utendekaji wa haki nchini, hatma ya demokrasia na utawala bora, Chadema inashauri ifuatavyo;

1. Kwa kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, kumetungwa sheria zenye makosa mengi yasiyokuwa na dhamana, iwapo Rais ana huruma ya dhati kwa wananchi wote, Serikali yake ifanye mabadiliko ya sheria, ili makosa yote yawe na dhamana na watu wasikilize kesi zao wakiwa uraiani kwa sababu lengo la dhamana ni kumpata mtuhumiwa awepo pale anapohitajika.

2. Viongozi wa Serikali au vyombo vyake, wajiepushe kuvunja misingi ya utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Mojawapo ya msingi muhimu ni dhana ya kila mtu kuchukuliwa hana hatia hadi itakapothibitishwa hivyo na mamlaka zenye wajibu huo kisheria. Kuwataka watu waombe samahani na kurejesha fedha, wakati hawana makosa, ili waachiwe, ni kuondoa dhana hiyo ya *‘presumption of innocence’.*

3. Serikali iimarishe mifumo ya utoaji haki hasa kwa;

(i) Kutunga sheria itakayoelekeza vyombo husika kutomfikisha mtuhumiwa mahakamani na kumfungulia mashtaka kwa kosa ambalo halina dhamana, bila upelelezi kuwa umekamilika. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kesi nyingi, hasa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kuchukua muda mrefu kuanza kusikilizwa kwa kisingizio cha ‘upelelezi’ haujakamilika, huku watuhumiwa wakisota mahabusu.

(ii) Kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa wa mamlaka za ukamataji na uchunguzi, hususan katika kesi zinazohusishwa na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, ambapo kumekuwa na vyombo vingine, zaidi ya Jeshi la Polisi, vinavyokamata watu (mf; TAKUKURU, TRA, SUMATRA, etc) kisha wanahifadhiwa vituo vya polisi huku jeshi hilo likitoa kauli kuwa halihusiki na watuhumiwa hao (kuwakamata wala kupeleleza kesi zao) isipokuwa limepewa kuwahifadhi tu.

4. Ni vyema na wakati mwafaka sasa, Rais John Magufuli akaagiza uwajibikaji wa watu au vyombo vya kiserikali vilivyohusika kuwakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao ambao Serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma zao. Hii itaondoa utata mwingine ambao umesababishwa na kauli yake ya jana, kwamba watu hao wasiokuwa na hatia wakiomba msamaha, wakarejesha fedha, wakasamehewa, inaishia hapo? Vipi kuhusu wale wote waliohusika katika kuwakamata na kuwafungulia tuhuma za uongo na kuwanyima haki yao ya kuwa raia huru uraiani?

5. Serikali itoe orodha ya watuhumiwa wote wenye kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inaowashikilia mahabusu za polisi na magereza, kesi wanazoshtakiwa nazo na thamani ya fedha wanazotuhumiwa kuhujumu au kutakatisha. Hii itasaidia kujua kiwango cha huruma iliyotolewa na Rais John Magufuli na ukubwa wa tatizo la uonevu katika mfumo wa utoaji haki na sheria nchini, hasa kwa kutumia kesi za mashtaka hayo.

*Hitimisho*

Chadema inasisitiza kuwa hakuna mbadala wa haki wala uhuru wa mtu pale unapokuwa umepokwa au kuminywa kwa namna yoyote ile, ikiwemo kesi za hila na kubambikiwa. Hivyo si sahihi kutumia unyonge na madhira ya watuhumiwa walioko mahabusu, kufanya nao (biashara) makubaliano ambayo yatajenga msingi kwamba haki yao imepatikana na uhuru wao kurejeshwa kwa sababu wametoa fedha.

Hivyo basi, kwa kuwa Serikali imeonekana kushindwa kuthibitisha tuhuma za watuhumiwa hao na mojawapo ya sababu kubwa ni kuwa tuhuma zinazowakabili wengi wa washtakiwa wa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni za kubambikiziwa, na wengi wao wamekaa muda mrefu mahabusu huku kesi zao zikisuasua kwa upelelezi kutokamilika, wasiadhibiwe kwa mtindo wa kupewa masharti kama ilivyoagizwa na Rais, bali DPP atekeleze wajibu wake wa Kikatiba na Kisheria ili watu hao watendewe haki na kuachiwa. Katika misingi ya haki, ubinadamu na utu, wao ndiyo wanastahili kuombwa samahani.

Imetolewa leo Jumatatu, Septemba 23, 2019 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Chadema hawajielewi,wamekosa ubunifu sasa hv kazi yao ni kukurupuka tuu na matamko kuhusiana na uchapakazi wa mh Rais.
 
Mnafiki ni yule anaeweka watu ndani alafu baadae anajidai kuwaonea huruma ili kupata kiki za kisiasa!!
Raisi aliemaliza muda wake alisema sio hela za serikari.

Mawaziri na wataalamu wa sheria wa muda ule kwa upande wa serikari waliridhia sio hela za serikari.

Watu wakapelekwa kamati ya maadili wakaonekana hawana hatia, wawili watatu kwa kuonewa wakafungwa kisiasa au sijui walitakiwa warudishe hela.

Viongozi CHADEMA, unafiki wa ofisi ya CAG na kamati ya kipuuzi ya PAC ya muda ule wakaendelea kuaminisha umma ni hela ya serikari.

Kibaya zaidi CDM kama chama wakawa wanatoa political pressure ya hilo sakata watu wachukuliwe hatua.

Serikari kwa kuitikia wito wamefanya ivyo miaka mitatu baadae hakuna ushahidi watu wanataka kujifanya wamesahau msimamo wao wa awali.

Njia ya mwongo ni fupi, kwenye siasa ukiwa na viewpoint fulani mambo yakienda mrama ni bora kukaa kimya kuacha upepo upite, hila kitendo cha kujitokeza kuhamia upande wa pili wa argument kinaonyesha ni watu ambao wapo desperate kutafuta wimbi la kuwanyanyua kwenye jamii na unafiki uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom