CHADEMA yatoa neno juu ya figisu figisu zinazoendelea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

CHADEMA yatoa neno juu ya figisu figisu zinazoendelea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Kufuatia matukio yanayoonyesha mazingira ya kuharibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yaliyojitokeza siku ya kwanza ya kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za uteuzi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, siku ya Jumanne Oktoba 29, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemwandikia barua Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kumtaka achukue hatua za haraka dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi huo.

=====

Kufuatia matukio yanayoonesha mazingira ya kuharibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yaliyojitokeza siku ya kwanza ya kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za uteuzi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, siku ya Jumanne Oktoba 29, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemwandikia barua Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kumtaka achukue hatua za haraka dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi huo.

Katika barua hiyo ambayo imeambatanishwa na taarifa inayoonesha mifano mahsusi kuhusu ukiukwaji huo wa kanuni, Chadema kimemtaka Waziri wa TAMISEMI ambaye kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mamlaka ya rufaa, kutambua kuwa kukithiri kwa vitendo vya dhuluma katika uchaguzi kunajenga na kuchochea hisia mbaya kwa wananchi ambao ndiyo wenye uchaguzi.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Chadema imeainisha mambo tisa yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na wasimamizi wasaidizi, ambayo ni ukiukwaji wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kiashirio cha kuvuruga na kuharibu uchaguzi;
  • Wasimamizi/Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kutoa nakala za fomu ambazo hazina nembo ya Halmashauri husika na mhuri ili kuthibitisha kuwa ni nakala halisi.
  • Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutofungua ofisi kwa ajili ya kutoa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kwa wagombea wa Chadema hata baada ya wagombea hao kufika kwenye ofisi za wasimamizi kabla ya muda wa kuanza kutoa fomu saa 1.30 asubuhi, kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019.
  • Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoa nakala za fomu za kuomba kugombea bila kuambatanisha fomu za maadili ya uchaguzi jambo ambalo linaashiria kuweka mazingira ya kuwaengua wagombea wa Chadema.
  • Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kukataa kutoa fomu kwa sababu ambazo ni kinyume na Kanuni, mathalani kushindwa kumpatia mgombea fomu kwa kigezo cha kutolipia mchango wa Mwenge jambo ambalo halitajwi kwenye Kanuni wala Mwongozo.
  • Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kukataa kutoa nakala ya fomu ya kuomba kugombea baada ya mgombea kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa.
  • Wasimamizi/ Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kudai kwamba katika maeneo yao wapo wagombea wa Chama cha Mapinduzi pekee.
  • Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kukataa kutoa fomu kwa wagombea wa Chadema kwa hoja kuwa kuna watu wengine wameshachukua fomu hizo, mathalani katika maeneo mbalimbali ya Mbozi, Vwawa na Tunduma. Pamoja na ukweli kuwa wagombea wa Chadema walikuwa kwenye ofisi za wasimamizi wasaidizi mapema asubuhi kabla ya muda wa kufungua ofisi, wakiwa na barua za kuwatambulisha kutoka kwa viongozi wa Chadema.
  • Baadhi ya wagombea wa Chadema kunyimwa fomu, mfano katika Wilaya ya Serengeti, Tunduma na Ukerewe kwa hoja kuwa wamejiandikisha mara mbili wakati si kweli na wakienda kutoa ripoti kwa majina yao kughushiwa na kuonekana katika vituo vingine, wananyimwa ushirikiano na Jeshi la Polisi.
  • Jeshi la Polisi, mgambo na viongozi wa Serikali kukamata, kushikilia fomu za wagombea, mfano Kitongoji cha Nyanghali, Kjiji cha Mwamagembe, Kata ya Mwataga, Wilaya ya Kishapu.

  • Katika barua hiyo ya tarehe 29 Oktoba, 2019, yenye Kumb. Na. C/HQ/ADM/MS/11/140, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, Chadema kimeeleza kuwa matukio hayo ni ukiukwaji wa kanuni ambazo zimetungwa kwa mujibu wa Sheria. Pia ni ukiukwaji wa Katiba ya Nchi, ibara ya 146(1)(2)(c) ambapo madhumuni ya uwepo wa Serikali za Mitaa yameelezwa kuwa ni pamoja na kupeleka madaraka kwa wananchi na kuhakikisha demokrasia inaimarishwa katika eneo husika.
  • Imetolewa leo Jumatano, Oktoba 30, 2019

  • na; Tumaini Makene
  • Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano



photo5028337656647493734.jpg
photo5028337656647493735.jpg


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA

 
Toeni tamko uchaguzi mkuu wa CHADEMA unafanyika lini acheni kujificha kwenye Chaka la uchaguzi wa serikali za mitaa.

Huko CHADEMA kumejaa figisu figisu kibao za uchaguzi wenu mnakurupukia kwingine.Toeni tamko la uchaguzi wenu wa CHADEMA kwa waandishi wa habari
 
Kwani toka wameanza kutoa matamko, ni lipi limewahi kuwashtua watesi??
Kama hawawezi kuleta mabadiliko wawaachie watesi waafanye wanayotaka kuliko kuwa na matamko yasiyo na impact.
 
Ccm maji ya shingo dah, yaani wanaviogopa hata vyama vya upinzani kwenye sanduku la kura...
 
Chadema wakati mwingine huwa tunashindwa kuelewa kwanini mpaka leo bado munalia na hawa mataga wakati tunajua nyie ni huge IQ ya kuwazibiti hao hivi kwanini lakini!
 
Chama cha matamko
Sasa wamepata pa kujificha,tako la uchaguzi wa ndani hakuna
 
CDM wataendelea kulialia mpaka siku ya kiama

Haki haipatikani burebure kama pipi

Kama hatua stahiki kimkakati hazitachukuliwa kwa vitendo
 
Ulisema kwenda kwenye uchaguzi sio sahihi, playing field haiku levelled
 
Toeni tamko uchaguzi mkuu wa CHADEMA unafanyika lini acheni kujificha kwenye Chaka la uchaguzi wa serikali za mitaa.

Huko CHADEMA kumejaa figisu figisu kibao za uchaguzi wenu mnakurupukia kwingine.Toeni tamko la uchaguzi wenu wa CHADEMA kwa waandishi wa habari
Haya Bwana. Hivi huwa mnalipwa kwa kupotosha na kupindisha mada za watu?
 
Wewe dada jigeuze uwe dume angalao utakuwa na akili
Toeni tamko uchaguzi mkuu wa CHADEMA unafanyika lini acheni kujificha kwenye Chaka la uchaguzi wa serikali za mitaa.

Huko CHADEMA kumejaa figisu figisu kibao za uchaguzi wenu mnakurupukia kwingine.Toeni tamko la uchaguzi wenu wa CHADEMA kwa waandishi wa habari
 
Back
Top Bottom