Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 13,328
- 7,396
Walinitoa jasho kikao chao kilipoamua kwa pamoja kumwangukia Slaa agombee, jambo ambalo ni nadra kwani vyama vingine huwa na ushindani wa kugombania nafasi hiyo nyeti.
Mkuu Crashwise kwa hiyo habari hapo juu nakubaliana na wewe 100% wala sikubishii. Nisije nikawa kama wabunge wa CCM wanaunga Hoja 100% halafu wanaanza kuipinga tena huko katikatimimi naamini mwaka 2015 tanzania itaongozwa na chadema kwani nimebahatika kuzunguka nchi hii hakika iko tayari kuongozwa na chadema..cha msingi mashambulizi yaendelezwe na tuongeze umakini maana hawa mafisadi wanatafuta pakujishika...
MIKAKATI YA CHADEMAMbowe ametangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 Chadema haitapokea 'maskrepa' yaliyokosa nafasi katika vyama vingine, biashara ya kupokea watu waliokosa nafasi katika vyama vingine ilikuwa 2010.Alisema tabia ya kukimbilia meli dakika za mwisho ilikuwa zamani na kwamba uchaguzi ujao hawatakubali waliokosa fursa kwa vyama vyao kukimbilia Chadema.
Mipango yao ni kupata wabunge na viongozi bora watakaopimwa kwa dhamira, uwezo na uwajibikaji kwa chama."Wafanyakazi wanatishiwa kufukuzwa kazi na wafanyabiashara wanafilisiwa na kubambikiwa kodi kisa wameonekana kushabikia Chadema," alisema.
Baada ya kuhutubia, wanachama wa Chadema vyuoni mkoani Dodoma wameutaka uongozi wa chuo kuondoa bango la CCM lililoko UDOM kwa maelezo kuwa ni kinyume cha Ibara ya 7 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005.
ccm wamechekelea kuruhusu mgombea binafsi akili yao ikiwatuma kwamba wapinzani wanategemea makapi yanayotemwa na ccm, sasa wajue kwamba CDM iko full kwa kila nyanja, ccm itabaki na magamba yao, halafu kutakuwa na tawi lingine la magamba binafsi.
Candid Scope hii thread muda si mrefu itavamiwa na wale wanazi wa CCM waiharibu bado hawaja amka