Chadema yatikisa kwa mulugo; mtangaza nia aacha gumzo

dala dala

Senior Member
Nov 16, 2011
106
105
Hatimaye siku za CCM na Mulugo katika Jimbo la Songwe zinazidi kuhesabika mara baada ya Mwl. Frank Mwakitalima kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Songwe Mkoani Mbeya ambalo linaongozwa na Mhe. Philipo Mulugo. Kazi ya kutangaza nia ilifanyika kijijini kwao Saza na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi licha ya kuwepo kwa Mkutano wa Kijiji ambao inasemekana ulilenga kupunguza mahudhulio kwenye mkutano wa Wana CHADEMA. Vile vile, imeripotiwa ilipangwa mechi ya mpira wa miguu ili kuzidi kudhoofisha mwitikio wa jamii katika mkutano wa ndani wa CHADEMA. Hata hivyo pamoja na hila zote bado CDM walipata watu wengi waliofurika katika Ukumbi wa Ayoub Kijijini Saza.
Mara baada ya kutangaza nia wananchi walilazimika kumbeba juu juu mtangaza nia huyo kutokana na hotuba yake ya kihistoria ambayo aliitoa. Nilibahatika kupata nakala ya hotuba ambayo kwa kweli imejaa hoja za msingi na iliandaliwa kiweledi sana. Hotuba ni hii hapa;

HOTUBA YA MWALIMU FRANK PHILIPO MWAKITALIMA WAKATI WA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA SONGWE KWA TIKETI YA CHADEMA, UKUMBI WA AYUBU, SAZA, TAREHE 21/06/2015
Waheshimiwa Viongozi wa Chadema Jimbo la Songwe,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mliohudhulia,
Waheshimiwa Viongozi wa Dini mbalimbali mliohudhulia,
Wageni Waalikwa,
Wananchi wa Jimbo la Songwe,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Bwana Yesu Asifiwe! Tumsifu Yesu Kristo! Asalaam Alyekum.
Peopleeeeeeeeeeeees!!!!!!!!!!

Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na fadhili kunijalia afya njema na ujasiri wa kusimama mbele ya hadhara hii hapa Saza. Kipekee ninapenda kuwashukuru nyote mliohudhulia shughuli hii ambayo kama mlivyoelezwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari ni kuwa ninatarajia kutangaza nia ya kuwania kiti cha uwakilishi katika chombo cha juu cha kutunga Sheria katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu Wananchi,
Pia nina kila sababu kuwashukuru kwa dhati kabisa familia yangu, ndugu zangu na marafiki zangu kwa kuniunga mkono katika kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Jimbo la Songwe. Kipekee sana ninawshukuru wazazi wangu Mzee Philipo Mwakitalima na mama yangu mzazi Bi. Hawa Yassin Mapunda kwa kunipa baraka zao ili niweze kuingia rasmi katika kinyang’anyiro hiki ambacho tuna kila sababu ya kuibuka washindi.

Ndugu Wananchi,
Ninatambua kuwa baadhi yenu ni mara ya kwanza kusikia jina langu napengine ni mara yenu ya kwanza kuonana nami uso kwa uso. Ninaitwa Mwl. Frank Philipo Mwakitalima, mzaliwa wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Wazazi wangu pia ni wazaliwa wa Wilaya hii hii ama kwa maneno mengine mimi ni Mzawa halisi wa Wilaya hii. Babu yangu mzaa baba ameishi maisha yake yote pale Kiwanja na babu upande wa mama ameishi katika mji mdogo wa Makongolosi akifahamika kama Mzee Yassin Mapunda ambaye alikuwa Kiongozi maarufu sana mpaka kifo chake.

Ndugu Wananchi,

Nimesoma elimu ya msingi katika shule ya Msingi Saza na kisha Elimu ya Sekondari katika Shule ya Mkwajuni ambapo baadae nilijiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Sangu. Nilibahatika kufundisha katika shule yetu ya sekondari ya Mkwajuni kwa kipindi cha miaka miwili kisha nikahamia shule ya Sekondari ya Isangawana iliyoko Tarafa ya Kipembawe. Nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 2010 kuanza shahada ya Ualimu ambapo mwaka 2013 nilihitimu. Kwa sasa ninafundisha masomo ya Jiografia, Historia, Kiingereza na Uraia katika shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwerite inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Ndugu Wananchi,

Ninaijua Chunya kwa matamu na machungu yake. Nimeiishi kama mchimbaji wa kawaida; nimeishi kama mfugaji kupitia kwa wazazi wangu na pia nimeishi kama mkulima. Umri wangu wa miaka 36 si haba kuweza kujua undani wa maisha yanayowakabili wananchi wa Wilaya ya Chunya na hususani Jimbo letu pendwa la Songwe.

Ndugu Wananchi,

Wilaya ya Chunya ni miongoni mwa Wilaya za mwanzo kabisa kuundwa hapa nchini tena katika enzi za ukoloni. Kwa kumbukumbu nilizonazo ni kuwa ilianzishwa miaka ya 1940 na wakaloni wa Kiingereza. Licha ya ukongwe wake lakini ni kati ya Wilaya za nyuma zaidi kwa upande wa maendeleo hapa nchini katika kila Nyanja ya maendeleo mfano Elimu, Miundombinu, Afya, Maji na hata maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Ni hivi majuzi tu tumebahatika kupata barabara ya lami ambayo inaanzia Jijini Mbeya mpaka Chunya Mjini katika Jimbo la Lupa. Aidha katika miaka ya mwishoni ya 90 ndipo tulipata huduma ya umeme kutoka gridi ya taifa. Ninatambua sana kazi nzuri iliyofanywa na Mbunge wa wakati huo Mhe. Njeru Mlugala Kasaka ambaye katika historia ndefu na pana ya Wilaya yetu alijitokeza kuwa lulu na akafanikiwa kuiweka Chunya iliyosahaulika katika ramani na kipindi hicho mtakumbuka vizuri kuwa tulikuwa tunatembea kifua mbele kwa fahari ya Mbunge wetu.

Ndugu Wananchi,

Ili tuendelee kuna mambo ya msingi yanayohitajika kuchochea maendeleo husika. Nikinukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa, tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora. Kati ya mambo haya manne Jimbo letu linakosa Uongozi Bora. Sisi sote ni mashahidi wa aina ya kiongozi ambaye amekuwepo katika awamu ya nne ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya kuonesha uelewa duni wa masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa lakini pia imetuondolea heshima ya Wanachunya ambayo wazee wetu akina Kasaka waliijenga. Tumeaibishwa ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Ni Jimbo letu pekee ndilo ambalo lina Mbunge ambaye hajui nchi hii imetokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 maana nasikia yeye anasema ni Muungano wa Tanganyika na Zimbabwe. Sina muda wa kutosha kuelezea visa vya kusikitisha ambayo Mheshimiwa huyu kavileta katika awamu yake ya uongozi maana mambo mengine ni aibu na nina ogopa kusema yote msije mkadhani sina adabu lakini ukweli ndio huo.

Ndugu Wananchi,

Chunya ina dhahabu, Chunya ina ardhi nzuri, Chunya ina maporini ya wanyama, Chunya ina hifadhi kubwa ya madini ya Chuma, Chunya inamiliki sehemu kubwa ya Ziwa Rukwa na pia Chunya ni Wilaya kubwa kuliko zote katika Mkoa wa Mbeya lakini katika mizani ya maendeleo tunabuluza mkia. Hatuna sababu nzuri ya kueleza au kujitetea kwanini Wilaya hii na hususani Jimbo hili lisiwe mbele kimaendeleo. Uwezo Tunao, Nia Tunayo na Sababu Tunayo ya kuanza mwanzo mpya kuelekea Chunya yenye neema, Chunya yenye huduma bora za Afya, Maji na Elimu. Mimi ndiye kiongozi anayetakiwa kuleta mabadiliko haya.

Ndugu Wananchi,

Ninaomba niwakumbushe japo kidogo mfumo wa huduma za Afya jinsi zilivyokuwa za kutia moyo katika miaka ya nyuma kidogo kabla ya kuingia madarakani Mheshimiwa Mbunge anayemaliza muda wake. Hospitali ya Mkwajuni ilikuwa ni kimbilio na yenye kutoa huduma bora za afya. Japokuwa kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini kwa ujumla hospitali hii iliweza kukidhi mahitaji. Lakini kwa sasa ninyi ni mashahidi kuwa huduma katika hospitali yetu zinaporomoka kila iitwapo leo. Mbunge wetu yupo tu na wala hasitushwi na hali ilivyo sasa. Nimeambiwa kuwa siku moja akiwa Bungeni aliomba hospitali ibadilishiwe mita ya LUKU. Hivi kweli kwa matatizo makubwa yaliyopo katika hospitali yetu, je ni busara kuzungumzia suala dogo kama hilo ambalo kimsingi angeweza kulimaliza baina yake na Meneja wa Tanesco wa Wilaya. Au anataka tuamini kuwa Ofisi ya Tanesco Chunya imefungwa? Je, sisi wananchi tunapokuwa na matatizo ya mita za umeme huwa tunakimbilia Bungeni kulia tubadilishiwe Mita???

Ndugu wananchi,

Elimu ndio msingi wa maisha, wengine walisema elimu ni bahari na vile vile waungwana husema….Ukiona Elimu ni Ghali basi jaribu Ujinga (if You Think Education is Expensive, then, Try Ignorance). Kiwango cha Elimu katika Jimbo letu ni tete. Licha ya kupata fursa ya kuwa na Waziri mwenye dhamana ya Elimu, hakuna jambo lolote la maana ambalo limefanyika achilia mbali kugawa Kompyuta na vitabu vilivyopitwa na wakati. Binafsi ninasikia uchungu sana kuona kwamba Elimu haipewi kipaumbele katika Jimbo letu. Shule za Kidato cha Tano ni chache na zile za sekondari ufaulu wake bado ni umiza kichwa. Nikiwa mdau wa elimu na ambaye nimetoa mchango katika sekta hii katika Wilaya yetu, ninaona tumechelewa sana ukilinganisha na Wilaya nyingine. Huku kwetu watu wenye shahada tunahesabika, shahada ya pili ni wakuokoteza yote haya yameletwa na uongozi mbovu na sera mbovu za Chama kilichopo madarakani.

Ndugu Wananchi,

Nijuavyo mimi ni kuwa Mbunge ana jukumu la kuwasilisha matatizo ya Jimbo lake mbele ya Serikali kwa wakati na muda wowote. Mbunge anaruhusiwa kuwasiliana na Mawaziri, Waziri Mkuu na hata Rais bila kikwazo chochote. Ni fursa ya kipekee sana kuwa Mbunge kwani ni kiungo muhimu kati ya wananchi na Serikali. Kwa bahati mbaya sana, tangu kuanzishwa kwake Jimbo hili limekosa Mbunge makini na machachari amabaye anaweza kuwasilisha hoja za wana Songwe kwa umakini na kwa kuzingatia misingi ya hoja. Nikiuliza miongoni mwenu lini mlipata kumsikia Mbunge wetu akizungumzia suala la Maji, Umeme, Afya, Elimu, Uchumi, Migororo ya ardhi bondeni. Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa shughuli za Bunge lakini sijawahi kusikia akizunguza Bungeni labda kipindi alichokuwa Waziri ambapo alikuwa akisimama kujibu maswali. Ninaomba kusisitiza jambo hapa kuwa sina ugomvi na Mhe. Mbunge wa sasa ila ninaeleza ukweli. Haya yote ni matunda ya CCM na serikali yake ambayo imeshindwa kabisa kujielekeza katika mambo ya msingi ya maendeleo na badala yake kushughulikia masuala yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa taifa letu.

Ndugu wananchi,

Ombwe hili la kimkakati na kiuongozi ni baadhi ya sababu ambazo zimepelekea nianze safari makini ya kuutwaa ubunge kupitia chama makini, mtetezi wa wanyonge, rafiki wa wote CHADEMA. Nipo hapa leo kutangaza mwanzo mpya na mwelekeo mpya na Songwe mpya. Nina nia ya dhati na vile vile uwezo wa kuwaongoza ninao kinachokosekana ni ninyi kuniwezesha kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niweze kuamsha ari ya maendeleo ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu.

Ndugu Wananchi,

Kabla ya kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CHADEMA ninaomba usikivu wenu niweze kutaja maeneo yangu ya kimkakati ambayo nitayasimamia kwa moyo wangu wote, akili zangu zote na nguvu zangu zote. Maeneo haya ni kama ifuatavyo;
1. Kupiga vita umasikini
Umasikini si kipimo cha utakatifu wala uadilifu bali ni hali ambayo kila mmoja wetu anatakiwa aichukie ili sote tuweze kupiga hatua ya kimaendeleo. Ninatambua kila mmoja wetu kajaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa na nguvu na akili. Nguvu na akili ni furasa ambayo ikitumika ipasavyo huleta maendeleo. Nikipata fursa hii nitahamasisha ushiriki wa jamii katika kuongeza kipato cha kaya kwa kufanya kazi na vile vile kuwatengenezea mazingira wezeshi (Enabling Environment) yatakayochochea maendeleo. Mazingira wezeshi ni pamoja na masoko ya mazao na mifugo, mikopo kwa wachimbaji wadogo wadogo, umiliki wa maeneo ya machimbo kwa wachimbaji wadogo, uvuvi, na shughuli mbalimbali za kujiletea kipato ikiwa ni pamoja na vikundi vya kijamii vya kuweka na kukopa (VICOBA na SACCOS). Aidha, ni dhamira yangu kuhamasisha kilimo chenye manufaa kwa wakulima yaani kulima kwa tija.

2. Kusimamia uboreshaji wa huduma za Kijamii
Huduma za kijamii hususani Afya, Maji na Elimu ni lazima ziwe kwenye kiwango cha ubora unaokubalika ili kuchochea maendeleo. Kwa upande wa afya mkazo utaelekezwa katika kuboresha huduma za tiba kwa kuhakikisha vituo vya afya na hospitali yetu inapata wahudumu wa kutosha, dawa na vifaa tiba vinakuwepo na miundombinu yaani vifaa tiba na majengo yanawekwa katika hali nzuri. Nitaisimamia vilivyo serikali kuhakikisha kuwa huduma za afya kwa wote zinaboreshwa. Pia nitahamasisha jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii yaani Community Health Fund (CHF) ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za afya. Afya ya mama, mtoto na wazee itakuwa ni kipaumbele. Nitahakikisha wazee wanapatiwa matibabu bure kama ambavyo sera ya afya ya mwaka 2007 anavyoelekeza.
Kwa upande wa elimu nitasimamia ubora wa elimu katika Jimbo langu kwa kuhakikisha kuwa shule zote zinakuwa na Walimu, Madawati na Vitabu vya kutosha na vile vile kila mtoto anakwenda shule. Nitahakikisha ninatumia vizuri mfuko wa Jimbo kwa kuhakikisha elimu inapata mgao wa kutosha. Aidha, nitawasimamia watumishi wa Halmashauri yaani Mkurugenzi, Afisa Elimu na Waratibu wa Elimu Kata ili kushughulikia kero ndogo ndogo ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu.

3. Huduma za Maji safi na salama
Maji safi na salama ni muhimu kwa ustawi wa afya bora katika jamii yeyote. Vijiji vingi katika Jimbo letu la Songwe havina huduma ya maji safi na salama. Ni vijiji vichache tu ndivyo vinapata maji safi na salama. Licha ya uwepo wa tatizo hili, serikali ya CCM bado imelala na haina majibu sahihi ya kutatua tatizo hili. Mbaya zaidi ni kuwa hata Mbunge aliyepo sasa hajawahi hata siku moja kuzungumzia tatizo hili Bungeni. Pengine yeye halioni hili kuwa ni tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi. Ninatambua uwepo wa Miradi ya Maji ambayo ipo chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia hata hivyo miradi mingi ipo Jimbo la Lupa, mfano ujenzi wa bwawa la Matwiga na visima katika vijiji vingi upande ule. Hata hivyo huku kwetu hali ni mbaya na hakuna uwezekano wa kulimaliza kwa siku za karibuni na zile za usoni. Nina kila sababu ya kuomba uwakilishi ili nishughulikie tatizo hili. Kwa nini iwezekane Lupa na ishindikane huku Songwe?

4. Miundombinu (Barabara, Umeme na mawasiliano)
Barabara zinazopitika muda wote, uwepo wa umeme wa uhakika na mawasiliano ya simu ni kichocheo cha maendeleo katika jamii. Kama ilivyo kwa upande wa maji, Jimbo la Lupa lina afadhali sana kuliko Jimbo hili la Songwe. Kiini cha tatizo ni kile kile ukosefu wa uongozi bora na wenye maono au vision. Nitapigania uwepo wa barabara ya lami kutoka Mbalizi hadi Makongolosi na ujenzi wa barabara za Changalawe katika maeneo yaliyosalia. Vile vile, kwa vijiji ambavyo umeme kwao ni ndoto nitahakikisha vinafikiwa na umeme wa gridi. Ni wazi sintaweza kufikisha umeme kwenye vijiji vyote lakini ninaahidi kulishughulikia kikamilifu suala hili.

5. Michezo
Kama mnavyofahamu mimi ni mwanamichezo kwahiyo suala la michezo na burudani tegemeeni makubwa. Nitaanzisha ligi ya Jimbo kwa timu za mpira wa miguu, pete bila kusahau riadha ili tuweze kupata wachezaji watakaoshiriki michezo kitaifa na kimataifa.

Ndugu Wananchi,
Ninaomba kuwahakikishia kuwa nina vipaumbele vingi ambavyo kutokana na tatizo la muda sintaweza kuvitaja vyote ila endapo nitapitishwa na chama changu cha CHADEMA nitaeleza kiundani namna ya kufanikisha ndoto yangu ya Songwe yenye neema tele.

Ndugu Wananchi, mabibi na mabwana;
Bila shaka mmeelewa msingi wa mimi kupigania kuteuliwa kugombea kiti cha Ubunge kwa jimbo hili la Songwe. Ninawahakikishia utumishi uliotukuka na utetezi wa haki za raia wote bila kujali kabila, dini wala rangi. Nina msimamo thabiti na ninyi ni mashahidi wa ujasiri na misimamo yangu ambayo siku zote imelenga kutetea masilahi mapana ya nchi na wananchi. Ni matumaini yangu kuwa nikipata nafasi hii wenzetu wa vyama vinavyounda UKAWA vitaniunga mkono ili kwa pamoja tuweze kuipumzisha CCM.

Ndugu Wananchi,
Sasa ninapenda kutangaza rasmi kuwa nina sababu za msingi na nia ya dhati kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA kupitia UKAWA. Niungeni mkono ninawahakikishia kuwa hamtakaa mjutie uamuzi wenu. Kaulimbiu yangu ni Chaguo Jipya, Songwe Mpya, Amka Tuchape mwendo. Kaulimbiu hii inatuhusu sote bila kubagua itikadi ya mtu yeyote. Nilipoitwa nikaitika na sasa ni zamu yenu ndugu zangu kusimama pamoja na mimi ili kwa umoja wetu tufanye maajabu ambayo watu hawajawahi kuyafikiria. Inawezekana kabisa endapo tutatimiza wajibu na kutimiza haki yetu ya kupiga kura.

Ndugu Wananchi,

Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu ya kutangaza nia ninaomba kwa unyenyekevu mkubwa nirudie kuwashukuru nyote kwa kufika hapa kwani hii ndio imani yenu kwangu na ndio nguvu zangu. Tuweke tofauti zetu pembeni tushikamane ili kwa mwaka huu Mbunge wa Jimbo la Songwe atoke katika Kijiji chetu cha Saza.

Ndugu Wananchi,

Baada ya kusema hayo ninaomba kuishia hapa na kukaribisha maswali kutoka miongoni mwetu. Nipo tayari kutoa ufafanuzi katika jambo lolote.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.
 
Kila la kher kamanda! Nyota njema huonekana asubuh! Naona imeanzia kwako na baadae kusambaa nchi nzima! Mwambien murugo kua brn haikuishia wizarani pale ilpo mtoa mkuku sasa imemfuata had jmbon
 
Porojo tupu na uongo mwingi na unajua kabiss kuwa unawadanganya.

Akipata(japo 100% hapati) miaka 5 ijayo atasema haa hiyo sio kazi ya mbunge, kuleta hayo ni kazi ya serikali.
 
Kazana kufanya mikutano mingi vijijini huko .tena andaa kamati kuu kila kata yenye watu 200 wa kufanya kampeni yako kwenye kila kijiji
 
Acha mbwembwe unatuchosha unashindwa kusamariz
 
Ndugu sio kila kitu kinahitaji summary vinginevyo mitihani ingekuwa rahisi sana. Hapa nimeweka hotuba rasmi aliyoitoa Mtangaza nia. Sikutaka kupunguza au kuongeza maneno yangu. Karibu sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom