Usishangae kusikia hivyo; kwani ni kawaida serikali inaposhindwa kutimiza majukumu yake inatafuta chaka la kujifichia. Hizi ni siasa za kutaka kupoteza nini chanzo ili muafaka upatikane na si kwamba hilo gazeti lina ukweli na kile wanachoandika. Wakiambiwa wataje majina ya hao wanafunzi waliowahoji ili waeleze ni ktk mazingira gani chadema imehusika watakosa majibu. Kwani chadema inahusika vipi na mikopo ya wanafunzi? Na chadema inahusika vipi na uongozi wa udsm kufanya maamuzi ya kikatili na kinyama dhidi ya wanafunzi?
Mimi ningeshauri serikali yangu itafute muafaka wa suala hili na si kwa udsm pekee bali ni kwa vyuo vyote na mfumo wa elimu nchini, kwani tuna tatizo kubwa sana. Serikali ijaribu kuangalia chanzo na kutoa solution na si kukimbilia kufukuza wanafunzi wkt wana madai ya msingi. Lkn kwasasa tusitegemee muafaka, kwani serikali yetu ina hali mbaya sana ki-pesa, kwani kwa taarifa nilizonazo, si tu kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchini tanzania ndiyo wenye tatizo la pesa lkn kuna jamaa yangu anasoma nje ya nchi kanifahamisha kwamba wanataabika sana kwani serikali yetu imeshindwa kuwatumia pesa ya matumizi ni ni muda mrefu sasa na kusababisha baadhi yao washindwe kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Mbaya zaidi kuna baadhi yao wameondolewa kwenye nyumba walizokuwa wanaishi kwa kushindwa kulipia, kwani serikali yetu imeshindwa kutimiza sehemu ya mkataba ontime kama walivyokubaliana. Cha ajabu, hiyo pesa ambayo wanatakiwa kuwalipa ilitolewa pia na nchi husika kwa serikali yetu lkn bado serikali imetumia pesa ya mdhamini bila kuwapa wanfunzi kama walivyokubaliana na mdhamini. Na hii hali inaweza kusababisha uhusiano mbaya kati ya tanzania na hiyo nchi hisani, na ukizingatia hiyo nchi ina uchumi imara duniani na inatoa msaada mkubwa sana kwa serikali yetu.
Pia waandishi wa habari badala ya kutafuta habari zenye kuleta muafaka wa tatizo, wao wanafikiria kuhamisha attention za watu kwa kuhusisha chadema na hiyo migogoro. Serikali yetu haioni kwamba kwa maamuzi yake ndiyo maana kundi kubwa sana ya vijana nchini wanaichukia serikali? Hivi serikali ingekuwa na dira na kuto slution kwa mambo ya msingi nchini kama elimu, afya, miundombinu, nishati, n.k ; je hao wapinzani wangepata hoja wapi za kusemea? Haya ndiyo matatizo ya kutokuwa na vision ktk uongozi wa serikali yetu. Yaani serikali ipo tu na wala haijui ni kwanini ipo na inataka kwenda wapi? Mwisho wake serikali inaona ni bora iwatumie waandishi wa habari kama hawa ambao maandishi yao hayaonyeshi tatizo lilipo wala kutoa muafaka na badala yake wanaipendelea serikali bila ya kuwa na hoja za msingi.