CHADEMA yatajwa mgomo chuo kikuu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yatajwa mgomo chuo kikuu...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Leonard Robert, Jan 12, 2012.

 1. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Nimeshangazwa sana habari hii iliyopewa uzito wa juu na kukolezwa wino kwenye Gazeti la CCM (uhuru) leo..

  Gazeti ili linadai lime wahoji wasomi hao, nanukuu "siri ya mgomo wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (udsm) imefichuka ,ikidaiwa unachochewa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

  Madai hayo yalitolewa jana na baadhi ya wanafunzi wanaondelea na masom chuoni hapo, waliodai kuna wabunge viongozi wa chama hicho wanachochea mgomo walidai wamekuwa wakipandikiza chuki kwa baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO)" mwisho wa kunukuu..

  Hivi ndugu zangu tunaitaji msaada wa viongozi wa chadema kushinikiza wenzetu wapewe mikopo? Je ni viongozi gani walichochea mgomo huo juzi? Je zigo hili abebeshwe Lema tena?

  Au ni mbinu ya magamba kuhalalisha fukuzafukuza yao hapo udsm..kuna wakati fulani fukuzafukuza hii ilihusishwa na mkuu wa kaya kuzomewa mbele ya mseveni.

  Ndugu zangu nini maana ya hii habari?
   
 2. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Karibu wadau.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Washenzi hao magamba,wamefikiria kwa kutumia masaburi yao wametoka na upupu huo,hawakubali kubadilika ndo maana nchi inaharibika
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  wanashangaza sana kila watu wakilalamika au kuamua kupigania haki yao utasikia wametumwa na CHADEMA..nashindwa kuwaelewa.
   
 5. a

  adobe JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  My friend ngoja ....au.... Hivi udsm cku hizi wanasoma watu toka wapi?nigeria,somalia au libya na irak?ngoja ninye bia yangu na kitmoto nikimaliza ntarudi humu
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Usishangae kusikia hivyo; kwani ni kawaida serikali inaposhindwa kutimiza majukumu yake inatafuta chaka la kujifichia. Hizi ni siasa za kutaka kupoteza nini chanzo ili muafaka upatikane na si kwamba hilo gazeti lina ukweli na kile wanachoandika. Wakiambiwa wataje majina ya hao wanafunzi waliowahoji ili waeleze ni ktk mazingira gani chadema imehusika watakosa majibu. Kwani chadema inahusika vipi na mikopo ya wanafunzi? Na chadema inahusika vipi na uongozi wa udsm kufanya maamuzi ya kikatili na kinyama dhidi ya wanafunzi?

  Mimi ningeshauri serikali yangu itafute muafaka wa suala hili na si kwa udsm pekee bali ni kwa vyuo vyote na mfumo wa elimu nchini, kwani tuna tatizo kubwa sana. Serikali ijaribu kuangalia chanzo na kutoa solution na si kukimbilia kufukuza wanafunzi wkt wana madai ya msingi. Lkn kwasasa tusitegemee muafaka, kwani serikali yetu ina hali mbaya sana ki-pesa, kwani kwa taarifa nilizonazo, si tu kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchini tanzania ndiyo wenye tatizo la pesa lkn kuna jamaa yangu anasoma nje ya nchi kanifahamisha kwamba wanataabika sana kwani serikali yetu imeshindwa kuwatumia pesa ya matumizi ni ni muda mrefu sasa na kusababisha baadhi yao washindwe kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Mbaya zaidi kuna baadhi yao wameondolewa kwenye nyumba walizokuwa wanaishi kwa kushindwa kulipia, kwani serikali yetu imeshindwa kutimiza sehemu ya mkataba ontime kama walivyokubaliana. Cha ajabu, hiyo pesa ambayo wanatakiwa kuwalipa ilitolewa pia na nchi husika kwa serikali yetu lkn bado serikali imetumia pesa ya mdhamini bila kuwapa wanfunzi kama walivyokubaliana na mdhamini. Na hii hali inaweza kusababisha uhusiano mbaya kati ya tanzania na hiyo nchi hisani, na ukizingatia hiyo nchi ina uchumi imara duniani na inatoa msaada mkubwa sana kwa serikali yetu.

  Pia waandishi wa habari badala ya kutafuta habari zenye kuleta muafaka wa tatizo, wao wanafikiria kuhamisha attention za watu kwa kuhusisha chadema na hiyo migogoro. Serikali yetu haioni kwamba kwa maamuzi yake ndiyo maana kundi kubwa sana ya vijana nchini wanaichukia serikali? Hivi serikali ingekuwa na dira na kuto slution kwa mambo ya msingi nchini kama elimu, afya, miundombinu, nishati, n.k ; je hao wapinzani wangepata hoja wapi za kusemea? Haya ndiyo matatizo ya kutokuwa na vision ktk uongozi wa serikali yetu. Yaani serikali ipo tu na wala haijui ni kwanini ipo na inataka kwenda wapi? Mwisho wake serikali inaona ni bora iwatumie waandishi wa habari kama hawa ambao maandishi yao hayaonyeshi tatizo lilipo wala kutoa muafaka na badala yake wanaipendelea serikali bila ya kuwa na hoja za msingi.
   
 7. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  wanaosoma udsm ni wananchi wa kawaida tu kutoka hapahapa tanzania tena waliowengi ni watoto wa wakulima wasio na kitu,mdio maana hawako tiyari hata kile kidogo ambacho ni halali yao kichukuliwe..
   
 8. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Mkuu RTI umenena,kama hali imefikia huko..yaani ata wale wanaosomea nchi za watu wanateseka kiasi hicho tunakoelekae ni kubaya sana.na huko je wakiamua kudai haki yao.CHADEMA itausishwa?
   
 9. MsakaGamba

  MsakaGamba JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 392
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa uvivu wa kufikiri uliotawaliwa na ujinga ma ccm wanaendelea kujidhihirisha kuwa wanafikiri kwa kutumia masaburi. Hata ahadi za jk kuto kutekelezeka wataisingizia chadema.
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  inaoneka chadema imewashika pabaya hadi wanaiota..hivi kwanini hii serikali ya jk inaruhusu uzushi na uposhaji unaofanywa na hiki kigazeti.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kama ndiyo basi wakubali kumbe chadema ilishinda kwani huwezi ukawa na ushawishi wa kila sehemu kama hukubariki waipishe iongoze nchi.....
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwani wanauwezo wakufikiri tena?
   
 13. j

  jigoku JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hilo chama la Magamba limeshajiishia tunasubiri siku tu,maana linatapatapa tu,badala ya kutafuta chanzo na njia ya kumaliza migomo UDSM wao wanakimbilia CDM.majizi sana haya magamba,lakini hawajui ya kuwa wanajichimbia shimo kwa kufanya maamuzi ya kiuaji namna hiyo,huwezi kusema watu wasidahiliwe chuo chochote hapa nchini na watu wakaendelea kukufurahia,haki yao wanadai wanalipwa virungu,mabomu na maji ya kuwasha,ila wao hela za kulazimisha watanzania waone wameleta maendeleo tangu uhuru zilipatikana,kwani kulikuwa na haja gani kufanya sherehe zenye kugharimu pesa nyingi?ujinga wa magamba-ccm utatupeleka pabaya
   
 14. d

  defence JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Mimi nilikuwa nasubiri muda tu wala hii habari siyo ya kushangaza maana hata
  kabla hazijaandikwa nilitaraji mwisho wa siku itakuwa hivi. Tukumbushane kabla
  ya uchaguzi ni hawa hawa chama cha magamba waliwapeleka pale Diamond Jubilee
  huku mgombea wao akiwa na bashasha tele kuwahakikishia kuwa suala la kukosa
  mikopo litakuwa historia leo badala yake wamepelekewa POLISI wenye silaha
  sijajua kama hela za ahadi ya mikopo ndizo wamenunulia silaha ua?Mimi
  sioni logic ya kuwa na fikra fupi fupi kama mkia wa mbuzi ni wajibu wa watawala kuhakikisha elimu
  na mikopo inatolewa kwa wakati kama walivyohakikishiwa wao mpaka leo wanaitwa
  MAPROFESA MAWAZIRI WENGINE MARAIS, Mwl.Nyerere alifanya kazi na nakumbuka
  katika moja ya mikutano yake alisema haelewi kwanini watu wanakimbilia IKULU
  ilihali yeye amekaa pale miaka 25 hajaona faida zaidi ya mateso ya kifikra kutokana
  na ufukara wa ANAOWATALA, mm nadhani watanzania wa leo si wale wakupewa
  ahadi za KUTABIRI kama watawala walivyozoea ni wakati wa kuamka na kusonga
  mbele hela za sherehe za mapinduzi na miaka hamsini ya uhuru ulioko kizani tunazo
  hizi za kuwapa posho zao shahiki Madaktari na mikopo ya wanafunzi ni ngumu kuzipata,
  viongozi waache kutumia MASABURI kufikiri watumie AKILI si kutafuta sababu fupi kama mkia wa
  MBUZI
   
 15. T

  Tewe JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kama mkuu wa kaya hajui kwanini nchi ni maskini unatarajia kuna gamba anayeweza kutafuta chanzo cha tatizo?
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  SWALI!

  Kwanini vyuo vikuu karibia yote Nchini hawaipendi chama iliyo madarakani??
   
 17. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na gazeti la magamba japo mi tangu niambiwe kuwa la magamba cjawahi kulisoma. Ni kweli walichoandika kwasababu chadema wameshindwa
  1. Wameshindwa kuwapa mikopo
  2. Hata mgomo wa madaktari ni sababu ya cdm kwani wameshindwa kuwalipa mshahara
  3. Hata mgomo wa waalimu ni cdm kwa kushindwa kulipa mishahaera na malimbikizo yao
  ushauri: Chadema wameshindwa kutekeleza majukumu ya kuihudumia jamii hivyo ni bora wawaachi ccm na ccmb waendeshe nchi.
   
 18. G

  G.JUMA Senior Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du! Huu ni utata mtupu.
   
 19. B

  Buto JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukishakuwa magamba lazima utakuwa kilaza
   
 20. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  kwa hali hii nchi nzima ni CHADEMA maana matatizo yanaongezeka na watu wanazidi kulalamika.
   
Loading...