CHADEMA yashindwa vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yashindwa vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jan 26, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Chama cha demokrasia na maendeleo kimeshindwa vibaya katika uchaguzi wa udiwani kati ya kati mjini Arusha.
  Katika uchaguzi huo CCm ilipata ushindi mkubwa wa zaidi ya 68% uku CHADEMA ikiambulia 22%.CHADEMA ilitumia nguvu kubwa katika uchaguzi huo,mwenyekiti wa CHADEMA F Mbowe alitumia siku tatu za mwisho kumpigia debe mgombea wake Bwana Simba kitu ambacho kiliwashangaza wakazi wa jiji la Arusha hasa ikizingatiwa uchaguzi ulikuwa ni kata tu.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ngongo; Shukrani,

  On a positive note, ningesema CCM YASHINDA UCHAGUZI WA KITI CHA UDIWANI ARUSHA KWA KISHINDO...
   
  Last edited: Jan 26, 2009
 3. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbowe alikwenda Arusha kati siku mbili za mwisho wa kampeni. Wakati ambapo chama hicho kilikuwa hakijafanya kampeni zozote huko. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa CHADEMA nayo imeishinda CCM Kigoma Ujiji kata ya machinjioni pamoja na CCM kuweka nguvu kubwa sana huko. Nadhani kila chama kimetetea kiti chake. CCM Arusha, CHADEMA Kigoma Ujiji

  PM
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  CUF inaonekana kama vile haipo kabisa huku Tz Bara. Kuna mtu anaweza kumshauri vizuri Lipumba?
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Huyo Lipumba atashaurika vipi wakati CUF ni ya Pemba tu? Lipumba na Seif ni vichwa ngumu na hawana maslahi yoyote kwa watanzania

  Huo ndio ukweli mtupu, anayebisha na atoe sababu
   
 6. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hee, viongozi wa CHADEMA si walikuwa kwenye operesheni Sangara mkoa wa Dar es salaam? Mi nilishangaa sana kusikia Mbowe amekwenda Arusha siku mbili za mwisho wa kampeni: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23456-polisi-watawanya-msafara-wa-mbowe-arusha.html niliuliza nikaambiwa alikwenda kupokea viongozi wa CCM waliohamia CHADEMA kwenye wilaya ya Arusha mjini na pia nasikia na yule aliyekaribia kuishinda CCM kwenye uchaguzi wa Ubunge Arusha Mjini anaitwa somebody Lema naye alihamia CHADEMA siku hiyo kwenye mkutano wa Mbowe. Hivyo, kwa kuwa kulikuwa na kampeni, alitumia mkutano huo kumnadi pia mgombea udiwani. Kwanini CHADEMA hakikupeleka nguvu kata ya Arusha kati? Au ilikuwa ni kata ya CCM sana?

  Asha
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  TZ kama hizi chaguzi zingekuwa huru na wazi wapinzani kwa sasa wangekuwa mbali. Uchaguzi wa Udiwani uko chini ya TAMISEMI (Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa). Wakati CCM walipoona halmashauri mbili uchaguzi mkuu uliopita zitaongozwa na upinzani (Kigoma nk), ikabidi walete muswada wa Waziri wa TAMISEMI awe na uwezo wa kuteua madiwani akiona kuna umuhimu kufanya hivyo. Wapinzani shirikianeni mutuongoze kupata tume huru na badiliko la sheria kandamizi.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Ngongo, ahsante sana kwa hii habari, sasa ni wakati muafaka tujitayarishe na chaguzi nyingine na kuangalia tulipokosea ni wapi!.
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Duh, inauma sana. Mgombea wa CHADEMA alikuwa navuta watu wengi sana kwenye mikutano yake. Nakumbuka CCM walipopoita sokoni wakitangaza kuhusu mkutano wao walizomewa hadi matangazo yao hayakusikika kabisa. Alipokuja mgombea wa CHADEMA umati ulikuwa mkubwa sana.

  Hata hivyo kuna jamno huenda imeshangia kushindwa huko; wafanyabiashara wengi wa sokoni si wakazi wa kata ya Mjini kati.

  Lakini pia CCM ni mafisadi, nadhani ungetupa idadi ya waliopiga kura ikilinganishwa na waliojiandikisha ili tuweze ku-analyse vizuri zaid. Uzoefu ni kuwa CCM hununua shahada za wapiga kura hasa wanaodhaniwa kuwa wa upinzani iliidadi ya wapiga kura wa upinzani ipungue nao wachukue ushindi (rejea chaguzi za Tarime na Kiteto). Sina hakika Mbeya vijijini.
   
 10. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umegusa penyewe. Utakumbuka mwaka jana kuna uchaguzi ulifanyika Arusha kata ya Sombetini, CHADEMA ikaiunga mkono TLP na Zitto Kabwe akaenda kusaidia kampeni hatimaye TLP ikaibuka ushindi. Katika uchaguzi ule baada ya kampeni kuelekea kushinda mafisadi wakaingilia kati ambapo kadi za wapiga kura zilinunuliwa kwa maelfu. Kata ya Sombetini ilikuwa na wapiga kura zaidi ya elfu 25 lakini wakapiga kura watu elfu 3 tu. Lakini hawakati huo wakawa wamechelewa, katika hizo hizo kura, TLP ikashinda kwa msaada mkubwa wa CHADEMA.

  Ushindi wa TLP uliendeleza ugomvi CCM Arusha kati ya kundi la Lowassa na lile kundi lingine ambalo mpaka wale wabunge waliobambikiziwa kesi ya rushwa na Lowassa pamoja na Sendeka wanaliunga mkono.

  Sasa ilipojitokeza kiti wazi safari hii, wakapata habari kwamba CHADEMA inakwenda kugombea na kushinda. Palikuwa pia na mgawanyiko ndani ya CCM. Ununuzi wa kadi ulianza mapema sana sasa. Naambiwa waliopiga kura wanakaribia elfu moja tu, wakati maelfu hawajapiga kura. Nitafuatilia kupata matokeo kamili. Nafuatilia pia matokeo ya Kigoma ambapo CHADEMA wamewashinda CCM.

  Ila kilichonishangaza katika uchaguzi huu ni kuwa TLP ambayo ndio ilikuwa na nguvu Arusha kabla ya kuanza kuitukana CHADEMA ilikuwa na mgombea katika uchaguzi wa Arusha kati, mgombea wao amepata kura 1 tu. Yaani kura yake mwenyew. CUF nayo ilikuwa na mgombea katika uchaguzi huo ambaye amepata kura 2 tu. Vyama vyote vya upinzani vilivyokuwepo katika uchaguzi huo kwa maneno mengine vimepata asimilia 0 ya kura, isipokuwa CHADEMA ambayo imepata zaidi ya asilimilia 20. Mwenye matokeo ya uchaguzi 2005 atuwekee hapa manake wakati huo inaonyesha TLP na CUF walikuwa na nguvu zaidi Arusha mjini. Nini kimetokea?

  PM
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka inawezekana ushindi huu ni mtamu kwa CCM sasa lakini kama hizi taarifa kuwa LEMA amejiunga na CHADEMA ni wazi CHADEMA watashangilia ushindi mkubwa zaidi 2010.

  Tukumbuke kuwa kiti hiki kilikuwa chini ya kijana machachari ambaye alitoka straight from Sokoine University na kuingia katika siasa kupitia TLP. TLP ambayo LEMA alikuwa mgombea wao kwa muda mrefu na akiwa na ufuasi mkubwa hapo. Hata hivyo huyu kijana MAWAZO ambaye alipata support kubwa ya Zitto wakati wa campaign aliamua kujitoa TLP na kuachia kiti kwa madai kuwa TLP hawako serious kitu ambacho kilikuwa na ukweli wake kiasi fulani. Hata hivyo nilisikia kuwa huyu kijana amejiunga na CCM.Hivyo ni wazi kuwa wapiga kura wa Arusha kati waliumizwa sana na uamuzi wake ambao waliona kuwa ni wa kisaliti lakini pia uliwavunja moyo wa kuwaamini WAPINZANI kwa ujumla.

  Tanzanianjema
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 15. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Ngongo

  Mbona husemi chochote kuhusu haya? Hebu bonyeza hapa:
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23485-ccm-yashindwa-vibaya.html

  Asha
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Asha Abdallah heshima mbele.
  Nimeona hayo matokeo ya huko Kigoma yanafurahisha sana,yaani ushindi mnene bila F Mbowe(Ranger Rover Vogue) na Fuso lenye spika kubwa.
  Vipi mbona kuhusu Godbless Lema husemi kitu.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Full Stop.
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa huko Mtwara ni makorodani ? Wacheni chuki binafsi ,CUF ipo na ni chama imara ambacho kinajulikana kimataifa na msione kama hawapo maana wakiwepo ni shangwe na vigelegele ila kama hawapo mnakuja na maneno ya ajabu ajabu.
  Hivi mnafikiri ni chama gani chenye madiwani wengi huko ubantuni.
   
 19. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  1.Hizo ndio zinaunda jimbo la uchaguzi.

  2.Arusha is politically stratergic.
   
Loading...