Katika uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa kumi na moja,manispaa ya Shinyanga,CHADEMA,wamefanikiwa kupata viti 7 kati ya 11,na CCM,wakiambulia vinne!
Mitaa hiyo ni:-
1:Lubaga Farm
2:Mbuyuni
3:Magadula
4:Masekelo
5:Mwamala
6:Luhende
7:Chamaguha (Nyumbani kwa Mwenyekiti wa CCM,Wilaya).
CCM,imeshinda mitaa ya:-
1:Old Shinyanga
2:Bushushu
3:Lubaga
4:Bondeni(ambako,askari walifyatua mabomu ya machozi,baada ya kutokea vurugu,baada ya kutangazwa mgombea wa CCM,kushinda.)
Uchaguzi huo,uliofanyika jana,ilikuwa kujaza nafasi zilizokuwa wazi,ikiwa ni pamoja na mitaa iliyoongezwa,baada ya kugawanywa baadhi ya mitaa.