Chadema yamuunga mkono Maalim Seif urais Visiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yamuunga mkono Maalim Seif urais Visiwani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 7, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimesikia katika kituo cha Channel 10 taarifa yao ya saa moja usiku huu kwamba katika mkutano wake wa hadhara katika viwanha vya Jangwani leo hii, Mwenyekiti wa Chadema amesema kwamba Chadema inamuunga mkono Maalim Seif katika kinyang'anyiro cha kuwania urais Zanzibar.

  Binafsi naona ni hatua nzuri kwani inaonyesha mshikamano kwa upande wa upinzani kuung'oa utawala wa kidhalimu wa CCM.

  Najua MS ataingia sasa hivi na kuponda hatua hii njema ya Chadema -- kwamba wanafanya hivyo kwa sababu hawana mtu kule Zanzibar wa kumsimamisha kuwania urais.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Aluta continua, mpaka kieleweke tu!
   
 3. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Heee mbona una unatanguliza kitu ambacho kinaonesha kama unahofu na MS... Naona MS amekuwa tishio hapa JF!?!?!......
   
 4. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #4
  Aug 7, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bara.... VIPI..Professor KAGOMA...kumpisha Dr Slaa???
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Aug 7, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Kuwa tishio si lazima mtu awe na silaha,au mabomu ya nyuklia! Ukijipaka kinyesi basi ni tishio kwa umma wa wastaarabu. Ukiwa na guts za kujisadia Morogoro Rd mapipa saa 6 mchana basi wewe ni tishio.
   
 6. P

  Pokola JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nguruvi3 unamaanisha nini haswa????:yawn:
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Ndio inavyotakiwa hivyo chadema sehemu ambayo unaona huna nafasi yoyote ni vizuri kuunga upande wenye lengo sawa na wewe.sasa huku bara CUF hawataki kuwaunga mkono chadema japo kuwa wanaona kwamba wao nafasi yao ndogo,tuwaelewe vipi?
   
 8. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nadhani Chadena wanekuwa waungwana, na wamejua kuwa hata kama watasimamisha mtu huko ni kupoteza muda na rasilimali za nchi. Jambo ambalo ningependa kuuliza kwa wana JF, huku bara Chadema na CUF ni kipi kinakubalika zaidi? Ama nije karibu zaidi Lipumba na Slaa ni nani anayekubalika zaidi? kwa nini wasiwe waungwana kama kweli ni wanamapinduzi kukaa pamoja na kumuunga mtu mmoja? sisi wana mageuzi tunachanganyikiwa. Nimemsikia Lipumba akimlaumu Slaa kwa kugombea urais, akidai kuwa anahitajika zaidi bungeni, maana yake ni nini? Je ina maana Lipumba ana imani kuwa CCM bado itashinda hivyo Slaa anahitajika kuendelea kuwasumbua ama ana maana kuwa yeye akiwa raisi andependelea Slaa amkosoe akiwa bungeni? Mimi nadhani Profesor amejaa ubinafsi. Yeye alikimbilia kujitangaza mgombea urais kupitia CUF akitegemea kuwa Chadema hawatasimamisha mgombea na kumuunga yeye mkono. Huu ni ubinasfi.

  Nadhani Profesor inabidi akubali kuwa watanzania walikwishamkataa mara tatu zote, watanzania wa leo wanataka mabadiliko sio kugombea tu. Dr Slaa ni chombo kipya, na mtu aliyejizolea umaarufu mkubwa. Lipumba na CUF ni lazima wawe waungwana na kushirikiana na Chadema na kumpeleka Slaa Ikulu. Kinyume cha hapo Lipumba awe na uhakika kuwa mwaka huu kwa mara nyingine CUF itakosa hata mbunge mmoja kama kipindi kilichopita.
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  thats what i'm talking abt............KUDOS to Chadema kwa kumuunga mkono Seif - CUF kule Zanzibar
   
 10. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema hii ni mara ya pili kuwaunga mkono cuf.... kwenye uchaguzi wa 2000 - walimuunga Lipumba. Nadhani ni vizuri Lipumba pia akiwaunga mkono chadema mwaka huu.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Aug 8, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wakati nina imani kuwa Profesa ni kichwa sana kwenye Uchumi, nina wasiwasi naye kutokana na tamaa ya madaraka, na kushindwa kusoma nyakati. Kipindi hiki kama CUF na CHADEMA vingeunganisha nguvu, CCM inepigwa mweleka wa Pwaa!!. Profesa angeweza kuongoza wizara nyeti kama vile Fedha, Mipango na Uchumi wakati wa serikali ya coalition ya CHADEMA na CUF, au hata kuwa Waziri Mkuu chini ya Rais Slaa.
   
 12. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama nimemwelewa vyema, anamaanisha kuwa MS kajipaka vinyesi kwa hiyo ananuka na ni tishio ....fyuuuuu
   
Loading...