nuruyamnyonge
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 4,452
- 2,317
Nampongeza rais mteule Donald Trump kwa ushindi mkubwa.
Tupo watu kama sisi tunaopenda kupata nakala na kuisoma.Sasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.
Chadema kuna demokrasia hajawahi kujitokeza mtu kuchukua fomu ya uenyekiti akanyimwa,lakini nikuulize wewe kule ugambani huwa kuna ushindani wa nafasi ya mwenyekiti?taratibu za kuwashindanisha wagombea wenyekiti zikoje?Mpeleke na taarifa kuwa mfalme Mbowe hataki demokrasia ndani ya chama, naona atawasaidia
Bila kusahu kumwambia kuwa huku huwa kuna watu kama jecha na lubuva....Mnaweza Kuolewa kabisa huko marekani.
Lkn pia msisahau kabisa kumwambia Trump kuwa kila unapofika uchaguzi Mbowe huwa anabadili gia angani
Chadema kuna demokrasia hajawahi kujitokeza mtu kuchukua fomu ya uenyekiti akanyimwa,lakini nikuulize wewe kule ugambani huwa kuna ushindani wa nafasi ya mwenyekiti?taratibu za kuwashindanisha wagombea wenyekiti zikoje?
Tatizo Tuna Chama Kimoja Tu Bado, Wakali Marekani Wana Vyama Vingi.Tanzania Ukiachana Na CCM Kuna Vitega Uchumi Vya KichaggaLakini uchaguzi huu uwe funzo kwa afrika kuwa kuna haja mtu kila uchaguzi mtu akishindwa kutimiza alichoahidi apigwe chini apewe mwingine.pia tuwe na vyama vichache ambavyo ni strong
tutampa,tuna fesibuku page yakeHapo ndipo utagundua kwamba haukuna mwenye nia ya dhati na nchi hii!!? Eti mtu na akil zake mbovu tena bila aibu "Tutamwambia na kumpa kila taarifa kuhusu kubinywa kwa democrasia hapa TZ na Africa" acheni kutege ea kila kutoka kwa nchi za ng'ambo ,jaribuni kutatua matatizo yenu wenyewe!!
baniani mbaya kiatu chake dawa,atatunyooshea ishu ya zanzibarMNA halalisha dhuluma.kwa waafrika na black amerika.trump si ndugu kwetu
mkuu,pongezi za rais wetu kwa rais mteule wa amerika DONALD JOHN TRUMP Zimefikaje hapa Jf?Sasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.
sisi yanatuhusu OVASasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.
TAARIFA KWA UMMA –UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI
• Pongezi kwa Rais Mteule
• Ni ushindi wetu IDU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya amani hapo tarehe 09.11.2016, na kukamilisha kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.
Tunapenda kumpongeza Rais Mteule Mhe. Donald Trump na Chama chake cha Republican ambao ni wanachama wa IDU kwa ushindi wa kihistoria walioupata, na zaidi tunampongeza rais mteule Trump kwa hotuba yake ya awali ya kuwashukuru wananchi wa Marekani na hasa aliposema kuwa anaahidi kwa wananchi wote wa Marekani kuwa anaenda kuwa rais wa wote, na kuwa hilo ni jambo la umuhimu wa kipekee kwake.
“I pledge to every citizen of our land that I will be President for all Americans and this is so Important to me”.
Ushindi huu ni ushindi wetu sisi wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kidemokrasia (International Democratic Union-IDU)na unatuma salaam nzito kwa Madikteta popote pale walipo kuwa utawala mpya wa Marekani hautavumilia kuona Madikteta ambao wanaminya Demokrasia na Haki za Binadamu, kama alivyoahidi wakati wa Kampeni zake.
Tunaahidi kumpa ushirikiano wote kwenye vikao vya IDU ambavyo sisi tunashiriki kama wanachama wa umoja huu na tutampatia kila aina ya taarifa sahihi kadiri ya uwezo wetu kuhusu hali ya Haki za Binadamu na Demokrasia nchini Tanzania na Barani Afrika.
Mwisho, tunampongeza Hillary Clinton kwa kufanya kampeni za kihistoria na kukubali matokeo ya kura .
Imetolewa leo tarehe 09.11.2016
na;
John Mrema –Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.