CHADEMA yampongeza Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,066
Reaction score
64,227
TAARIFA KWA UMMA –UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

• Pongezi kwa Rais Mteule
• Ni ushindi wetu IDU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya amani hapo tarehe 09.11.2016, na kukamilisha kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.

Tunapenda kumpongeza Rais Mteule Mhe. Donald Trump na Chama chake cha Republican ambao ni wanachama wa IDU kwa ushindi wa kihistoria walioupata, na zaidi tunampongeza rais mteule Trump kwa hotuba yake ya awali ya kuwashukuru wananchi wa Marekani na hasa aliposema kuwa anaahidi kwa wananchi wote wa Marekani kuwa anaenda kuwa rais wa wote, na kuwa hilo ni jambo la umuhimu wa kipekee kwake.

“I pledge to every citizen of our land that I will be President for all Americans and this is so Important to me”.

Ushindi huu ni ushindi wetu sisi wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kidemokrasia (International Democratic Union-IDU)na unatuma salaam nzito kwa Madikteta popote pale walipo kuwa utawala mpya wa Marekani hautavumilia kuona Madikteta ambao wanaminya Demokrasia na Haki za Binadamu, kama alivyoahidi wakati wa Kampeni zake.

Tunaahidi kumpa ushirikiano wote kwenye vikao vya IDU ambavyo sisi tunashiriki kama wanachama wa umoja huu na tutampatia kila aina ya taarifa sahihi kadiri ya uwezo wetu kuhusu hali ya Haki za Binadamu na Demokrasia nchini Tanzania na Barani Afrika.

Mwisho, tunampongeza Hillary Clinton kwa kufanya kampeni za kihistoria na kukubali matokeo ya kura .
Imetolewa leo tarehe 09.11.2016
na;

John Mrema –Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
 
UKAWA baada ya kushindwa kulinda kura zetu uchaguzi uliopita, sitakaa kuruhusu tena hata mchepuko wangu kupanga foleni kupiga kura zisizo na usalama. Trump angekuwa Tz basi Hillary angekuwa raisi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya amani hapo tarehe 09.11.2016, na kukamilisha kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.

Sasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.
 
TAARIFA KWA UMMA –UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

• Pongezi kwa Rais Mteule
• Ni ushindi wetu IDU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya amani hapo tarehe 09.11.2016, na kukamilisha kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.

Tunapenda kumpongeza Rais Mteule Mhe. Donald Trump na Chama chake cha Republican ambao ni wanachama wa IDU kwa ushindi wa kihistoria walioupata, na zaidi tunampongeza rais mteule Trump kwa hotuba yake ya awali ya kuwashukuru wananchi wa Marekani na hasa aliposema kuwa anaahidi kwa wananchi wote wa Marekani kuwa anaenda kuwa rais wa wote, na kuwa hilo ni jambo la umuhimu wa kipekee kwake.

“I pledge to every citizen of our land that I will be President for all Americans and this is so Important to me”.

Ushindi huu ni ushindi wetu sisi wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kidemokrasia (International Democratic Union-IDU)na unatuma salaam nzito kwa Madikteta popote pale walipo kuwa utawala mpya wa Marekani hautavumilia kuona Madikteta ambao wanaminya Demokrasia na Haki za Binadamu, kama alivyoahidi wakati wa Kampeni zake.

Tunaahidi kumpa ushirikiano wote kwenye vikao vya IDU ambavyo sisi tunashiriki kama wanachama wa umoja huu na tutampatia kila aina ya taarifa sahihi kadiri ya uwezo wetu kuhusu hali ya Haki za Binadamu na Demokrasia nchini Tanzania na Barani Afrika.

Mwisho, tunampongeza Hillary Clinton kwa kufanya kampeni za kihistoria na kukubali matokeo ya kura .
Imetolewa leo tarehe 09.11.2016
na;

John Mrema –Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Safi sana CHADEMA.

Kumpongeza aliyeshinda ni dalili ya kujitamkia mafanikio soon.

Mwaka 2020 tuko pale mjengoni mitaa ya Chimwaga tukipitisha miswaada kuwa sheria.

Mungu yu pamoja nasi
 
Trump angekuwa Tz Basi Hillary Angekuwa ameshaanza na kushona suti za kuingilia IKULU kwa sababu ya uwepo wa watu ambao Ni MANGULI katika kutengeneza matokeo,lkn kwa sababu democracy imetamalaki ndani ya USA basi aliye na kura nyingi ndo anayetangazwa mshindi.Hongereni sana WAMAREKANI kwa hicho mlichokionyesha kwa AFRIKA na Dunia at all.
 
Ch
Safi sana CHADEMA.

Kumpongeza aliyeshinda ni dalili ya kujitamkia mafanikio soon.

Mwaka 2020 tuko pale mjengoni mitaa ya Chimwaga tukipitisha miswaada kuwa sheria.

Mungu yu pamoja nasi

Chimwaga chuo kikuu???
 
Lakini uchaguzi huu uwe funzo kwa afrika kuwa kuna haja mtu kila uchaguzi mtu akishindwa kutimiza alichoahidi apigwe chini apewe mwingine.pia tuwe na vyama vichache ambavyo ni strong
 
Sasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.

Mbona Bwaba Yule leo alitoa pongezi tena kwa kiingereza kibovu? Na hii unasemaje sisi inatuhusu au?
 
TAARIFA KWA UMMA –UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

• Pongezi kwa Rais Mteule
• Ni ushindi wetu IDU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya amani hapo tarehe 09.11.2016, na kukamilisha kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.

Tunapenda kumpongeza Rais Mteule Mhe. Donald Trump na Chama chake cha Republican ambao ni wanachama wa IDU kwa ushindi wa kihistoria walioupata, na zaidi tunampongeza rais mteule Trump kwa hotuba yake ya awali ya kuwashukuru wananchi wa Marekani na hasa aliposema kuwa anaahidi kwa wananchi wote wa Marekani kuwa anaenda kuwa rais wa wote, na kuwa hilo ni jambo la umuhimu wa kipekee kwake.

“I pledge to every citizen of our land that I will be President for all Americans and this is so Important to me”.

Ushindi huu ni ushindi wetu sisi wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kidemokrasia (International Democratic Union-IDU)na unatuma salaam nzito kwa Madikteta popote pale walipo kuwa utawala mpya wa Marekani hautavumilia kuona Madikteta ambao wanaminya Demokrasia na Haki za Binadamu, kama alivyoahidi wakati wa Kampeni zake.

Tunaahidi kumpa ushirikiano wote kwenye vikao vya IDU ambavyo sisi tunashiriki kama wanachama wa umoja huu na tutampatia kila aina ya taarifa sahihi kadiri ya uwezo wetu kuhusu hali ya Haki za Binadamu na Demokrasia nchini Tanzania na Barani Afrika.

Mwisho, tunampongeza Hillary Clinton kwa kufanya kampeni za kihistoria na kukubali matokeo ya kura .
Imetolewa leo tarehe 09.11.2016
na;

John Mrema –Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
"tutampa kila aina ya taarifa"

najua ya zanzibar,uhuru wa kisiasa,sheria ya mtandao,sheria ya huduma za habari tayari mnazipanga kwenye bahasha tayari kwa safari
 
Sasa kama unawapongeza wananchi wa marekani hizo salamu si uzipost posta uwapelekee huko kwao marekani.Acha kujishaua hapa.Sisi waswahili hayatuhusu wapelekee huko kwao marekani.
mkuu soma ujumbe huo mkali kama upanga ndani ya mbavu
 
Back
Top Bottom