Si suala la kwamba ccm wamefanya ama hawajafanya, muhimu ni kuangalia kama ushirikiano huo una athari gani kwa chama chetu ama nchi yetu. Vyama vya siasa duniani kote vinashirikiana katika nyanja mbalimbali kadri ya mahitaji ya kila chama na nchi husika.
Lakini najua ninyi mliolishwa nyamafu na ccm huwa mkiona jambo limefanywa na Chadema hamuachi kutokwa na mapovu. Kila jambo linalofanywa na Chadema huwezi kulifananisha na jinsi ccm wanavyolifanya ama kutaka kuigeuza ccm kuwa ndio msahafu huo ni ufinyu wa fikra.
Na kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na ccm si kwakuwa ni ccm bali kwakuwa ndivyo mfumo wa maisha ulivyo ama mfumo wa kijamii unavyotaka na si suala la ccm. Ukweli ni kwamba ccm hawajawahi kuasisi kitu chochote ambacho kimeweza kutumiwa kama mfano huko duniani kwahiyo jaribuni kupanua akili yenu kutooona kila kitu kwa miwani ya ccm.
Hiki unachokisema hapa hakihusiani punge na hoja hoja yangu ambayo niliijenga kutokana na mabandiko ya hao wanajanvi waliokuwa wanataka kuharalisha kilichofanywa kimakosa na CCM na kudai CHADEMA nao wako entitled kukifanya.
Kuhusu bandiko lako. Mashirikiano ya vyama na vyama huwa yapo. Mashirikiano ya vyama yanapovuka mipaka ya nchi, first priority inakuwa ni utaifa na athari zake. Ni ubinafsi wa kupindukia pale chama kinachotegemea kuongoza nchi kinapofikiria tu faida yake kwanza wakati kinajihusisha na mashirikiano ya kimataifa na kufanya hivyo, ni kuonyesha jinsi kilivyo desparate kisiasa au kutojua athari zake.
Chama cha kisiasa kinapofikia hatua ya kufanya kampeni ya kisiasa kwa mgombea urais wa nchi nyingine ni makosa makubwa katika jicho la kidipromasia. Kwa nchi ambazo ni makini, hata michango ya kisiasa kwa wagombea hairuhusiwi kupokelewa kutoka kwa mwananchi, kampuni na kikundi ambacho ni cha kigeni, kufanya hivyo ni kosa la kijinai(criminal offence) achilia mbali foreigner na magari yao kufanya kampeni kwa miezi.
Kwa hiyo unataka kuniambia nini matarajio ya CHADEMA kuhusika moja kwa moja katika kampeni nchini Kenya?. Unafikiri kuna athari au haipo kisiasa na kiuchumi?.
Na kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na ccm si kwakuwa ni ccm bali kwakuwa ndivyo mfumo wa maisha ulivyo ama mfumo wa kijamii unavyotaka na si suala la ccm. Ukweli ni kwamba ccm hawajawahi kuasisi kitu chochote ambacho kimeweza kutumiwa kama mfano huko duniani kwahiyo jaribuni kupanua akili yenu kutooona kila kitu kwa miwani ya ccm.
Tanzania yapongezwa kwa kutatua migogoro Afrika
Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika.
Pongeli hizo zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama wapenda amani barani Afrika.
Hii ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nayo imepongezwa.