Chadema yambana Makinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yambana Makinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Oct 1, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda atoe hadharani ripoti ya uchunguzi inayowahusisha baadhi ya wabunge kujihusisha na rushwa ili iweze kujadiliwa.Wakati wa Bunge la Bajeti, Spika wa Bunge aliunda Kamati ya Bunge ili kuchunguza tuhuma za rushwa zinazowakabili wabunge kadhaa ikiongozwa na Mbunge wa Mlali (CCM), Hassan Ngwilizi.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara, katika Uwanja wa Michezo Karatu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema wamepata taarifa kuwa tayari kamati hiyo imemaliza kazi lakini kuna mpango wa kutoipeleka kwenye Bunge zima.

  "Tumepata taarifa kuwa kuna mpango wa kuipeleka taarifa ya Ngwilizi kwenye kamati ya Uongozi ya Bunge, Chadema hatukubali, tunataka taarifa hiyo ipelekwe kwa Bunge zima na tuitolee maazimio," alisema Zitto huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

  Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema wabunge wote ambao wametajwa kuhusika katika taarifa hiyo ya Bunge wanapaswa kuwajibishwa, kwani haiwezekani kila siku Watanzania kusoma habari za ufisadi na watuhumiwa hawachukuliwi hatua.
  "Tunataka taifa zima lijue kilichotokea kwa wabunge wao, hivyo Chadema hatutakaa kimya, tunataka taarifa iwe wazi," alisema Zitto.

  Alisema ni aibu viongozi wa kitaifa kila siku kulalamika taifa ni maskini, wakati nchi ina rasilimali nyingi ambazo zinafaa kuwakomboa Watanzania kujiondoa katika umaskini.
  "Watu wanazalisha tani hadi 50 za dhahabu, halafu tunaambiwa taifa ni maskini, hapana tuna tatizo la viongozi wetu, taifa hili linapaswa kuwa tajiri," alisema Zitto.

  Hivi karibuni Mbunge Ngwilizi alikaririwa akisema kuwa kamati yake imekamilisha ripoti yake na kwamba imeikabidhi kwa Spika wa Bunge kwa hatua zaidi.
  Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza kuwa ripoti hiyo imewatia hatiani baadhi ya wabunge waliokuwa wakituhumiwa kuhusika katika kashfa ya kuikwamisha kwa njia ya rushwa, Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Raia Mwema.

  Fedha zilizofichwa Uswis
  Kuhusu fedha zilizofichwa Uswis na baadhi ya watu nchini, Zitto alisema wanaiomba Serikali izirejeshe fedha hizo na kwamba Chadema inapanga kupeleka bungeni azimio la kuomba taarifa rasmi juu ya fedha hizo.
  Alisema kati ya hizo wamebaini kuna ofisa mmoja mkuu wa jeshi mstaafu anamiliki zaidi ya Sh50 bilioni, hivyo Chadema inataka fedha zote kurejeshwa.

  Lissu aonya Katiba Mpya
  Naye Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu alionyesha wasiwasi kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba kuwa inaweza kuhujumiwa na CCM.
  Alisema ni vyema wananchi wakajitokeza kutoa maoni yao kwa wingi kwani katiba inahitaji kuwatumikia wananchi na siyo Katiba ya sasa.

  my thinking! Zitto si alisema atawataja serikali isipowataja sasa mbona anakuja na kauli tofauti tena?? tayari ameshikishwa??
   
 2. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  OSOKONI Sasa ameshikishwa na nani na ameshikishwa nini? Huwa busara inatakiwa unapotaka kutaja majina ya watu, Zitto ni Mbunge mahali sahihi pa kuwataja na kutaka hatua zichukuliwe ni Bungeni!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mada yako imepoteza ladha kwa kuleta chuki za kijinga. sasa zito anaingiaje hapa?
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hao watu tutawajua tu kama sio leo ni 2015, i cant wait siku makinda sio spika tena
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  sorry nilisahau kuweka chanzo ni mwananchi elekeza maswali yako huko!
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  wewe sio mjinga ila mpumbavu tena sana! kumbuka kuwa zitto alisema atawataja walioficha pesa uswisi kama serikali haitawataja, sasa akiwa karatu anabadilika na kuanza kusema Chadema inapanga kupeleka bungeni azimio la kuomba taarifa rasmi juu ya fedha hizo.yeye alisema kwenye bunge la october atawataja kwa nn anabadili kauli??
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  kumbuka kauli ya zitto kuwa atawataja walioficha pesa uswiss mwezi october sasa anabadilika na kusema Chadema inapanga kupeleka bungeni azimio la kuomba taarifa rasmi juu ya fedha hizo.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Tatizo la nchi yetu ndio hilo Spika ndiye aliyeshindwa kuwachukulia hatua wahusika in the first place, sasa tume imeundwa
  taarifa anapelekewa mtu yule yule aliyeshindwa kuchukua hatua in the first place, hatakachokifanya ni kuvuruga tu kwani kama alikuwa na nia ya kuwachukulia hatua angeshawachukulia toka hapo mwanzoni. huu ni udhaifu mkubwa.
   
Loading...