CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani tabia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia magari ya serikali kwa shughuli za chama hasa katika sherehe mbalimbali za chama hicho.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kihesa mkoani hapa, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema CCM ilitumia magari ya serikali wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Alisema wabunge na viongozi wa CHADEMA hawatakubali kushuhudia mali za serikali zikitumiwa na CCM katika shughuli za kisiasa na kwamba atafuatilia kwa makini kiasi cha fedha zilizotumika kuyahudumia magari hayo.
Nitaongoza mapambano na kuyapiga mawe magari ya serikali, halmashauri au ya mahakama yatakayoonekana yakifanya kazi za CCM halafu watuambie yalienda kufanya nini. Mimi nitaongoza mapambano hayo kwa sababu yale magari ni ya serikali, CCM inunue magari yao, alisema Msigwa.
Awali mbunge huyo alilalamikiwa na wananchi wa Sentema juu ya baadhi ya viongozi wa kata hiyo kuwachangisha wananchi michango mbalimbali bila kupata matumizi ya fedha walizozichanga, hali ambayo inawakatisha tamaa kuendelea kuchangia.
Katika mkutano huo, mbunge huyo aliwapokea wanachama wapya 78 na kuzindua tawi jipya katika Kata ya Kihesa.
Source:Tanzania Daima