Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa CHADEMA kikiwa chini ya Mtendaji wake mkuu (KATIBU MKUU-TAIFA), Mhe. Wilbroad Peter Slaa. Hakika kila Mtanzania anaona kazi unayoifanya ya kuhakikisha chama chetu kina kuwa juu na Watanzania wote wanatuunga mkono. Mungu akupe uhai, naamini ipo siku tutaifikia Nchi ya Ahadi!
Hayo maneno yalielekezwa kwa ex Padre Slaa, sio kwa kubahatisha, Halima anajuwa anachokiongea, Slaa anajuwa na wewe unaejidai kupinga unajuwa, na mimi najuwa na nna uhakika wengine kwa sasa wanajuwa maana kamili ya kutufikisha "Nchi ya Ahadi".