CHADEMA Yajitoa mchakato wa Katiba; Yadai Rais kawauza!

- Chadema wajifunze kusikiliza mawazo ya wananchi kabla ya kukurupuka, kwenye la kwenda kwenda Ikulu wamekurupuka sasa warudi nyuma na kutafuta njia nyingine ya kushiriki kwenye katiba mpya ni lazima wawemo na zipo njia nyingi sana za kuipigisha magoti CCM ili kukubali their input, lakini kugomea is not one of them, Chadema njooni hapa mtusikilize kama mnavyofanya kwenye mengine!

- Hadithi nzima ya safari yenu Ikulu inanuka, lakini yaliyopita sio ndwele rudini nyuma mjipange upya, Yes I am CCM damu, lakini we need you maaana kule kwetu kuna magoi goi wengi sana wanahitaji kuamushwa usingizini! na ni TAIFA KWANZA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!

william umerudi baada ya kutupiga changa la macho khs magamba,nway wlcme bro
 
- Chadema wajifunze kusikiliza mawazo ya wananchi kabla ya kukurupuka, kwenye la kwenda kwenda Ikulu wamekurupuka sasa warudi nyuma na kutafuta njia nyingine ya kushiriki kwenye katiba mpya ni lazima wawemo na zipo njia nyingi sana za kuipigisha magoti CCM ili kukubali their input, lakini kugomea is not one of them, Chadema njooni hapa mtusikilize kama mnavyofanya kwenye mengine!

- Hadithi nzima ya safari yenu Ikulu inanuka, lakini yaliyopita sio ndwele rudini nyuma mjipange upya, Yes I am CCM damu, lakini we need you maaana kule kwetu kuna magoi goi wengi sana wanahitaji kuamushwa usingizini! na ni TAIFA KWANZA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!

Mtoto wa Malecela upo? Ndugu zako NJAA INAWAUA HUKO MTERA!
 
wale wenye mpango wa kuchomeka issues za Mbowe na Zitto hapa MSHINDWE NA MLEGEE! Hapa ni katiba tu msituvuruge tafadhali!!

Hongereni Chadema kwa kumvua nguo Kikwete na kumwacha mtupu japo washikaji wake wanamshangilia kwa kuweka madudu, hii nchi jamani ! Chadema mnaendesha siasa ya karne ya ishirini na moja lakini kwa waliozoea zile za mwaka 47 hata wakipewa darubini kali hawataweza kuona kile mlichofanikiwa. Watazamaji wengine wamechanganyikiwa jinsi boli linavyotandazwa hadi washika vibendera nao wameamua kuingia uwanjani !

Ni ajabu kuna watu wanaamini unaweza kupanda sukuma wiki ukavuna matikiti, ukapanda kunde ukavuna nyanya au ukapanda dengu ukavuna karanga, nchi hii jamani ! Ngoma wanayoipiga Chadema ni nzito na mdundo wake ni wa kisasa na kuucheza kunahitaji wepesi katika kuhamasisha viungo vyote mwilini zaidi ya tumbo. Ndiyo maana Chadema 1. Walilitega Bunge, 2. Wakamtega Raisi na sasa hatua iliyobakia ni kumfunua mwali.
 
nzenzu uliyoyaandika apo ndio ya kwako.huyo ulompa hayo majina hayamstahili.wewe ni njaa tu zinakusumbua.tobo lissu ni nani hapa tanzania mshamba tu aliyeenda kushangaa tausi ikulu na juice ya embe.kwanza cdm wanaingilia ndoa ya watu kama kawaida yao tumewazoea.wanamuonea mwenzao wivu badala ya kutafuta bwana yao mwingine.wameamua kuwa nyumba ndogo na wavumilie adha zake.hata hayo matamko ya MPWA WAKE MBOWE ( mnyika) ilikuwan ni changala macho, Hana jipya mfa maji tu.
 
Hongereni Chadema kwa kumvua nguo Kikwete na kumwacha mtupu japo washikaji wake wanamshangilia kwa kuweka madudu, hii nchi jamani ! Chadema mnaendesha siasa ya karne ya ishirini na moja lakini kwa waliozoea zile za mwaka 47 hata wakipewa darubini kali hawataweza kuona kile mlichofanikiwa. Watazamaji wengine wamechanganyikiwa jinsi boli linavyotandazwa hadi washika vibendera nao wameamua kuingia uwanjani !

Ni ajabu kuna watu wanaamini unaweza kupanda sukuma wiki ukavuna matikiti, ukapanda kunde ukavuna nyanya au ukapanda dengu ukavuna karanga, nchi hii jamani ! Ngoma wanayoipiga Chadema ni nzito na mdundo wake ni wa kisasa na kuucheza kunahitaji wepesi katika kuhamasisha viungo vyote mwilini zaidi ya tumbo. Ndiyo maana Chadema 1. Walilitega Bunge, 2. Wakamtega Raisi na sasa hatua iliyobakia ni kumfunua mwali.

Wataendelea kutega..nasi tunategeu...

hawana la maana tunajua wanachofanya, tunajua tunapata wapi habari ..oops

kwishney, nendeni kwenye tume mtoe maoni otherwise ..mtalialia tu
 
Hongereni Chadema kwa kumvua nguo Kikwete na kumwacha mtupu japo washikaji wake wanamshangilia kwa kuweka madudu, hii nchi jamani ! Chadema mnaendesha siasa ya karne ya ishirini na moja lakini kwa waliozoea zile za mwaka 47 hata wakipewa darubini kali hawataweza kuona kile mlichofanikiwa. Watazamaji wengine wamechanganyikiwa jinsi boli linavyotandazwa hadi washika vibendera nao wameamua kuingia uwanjani !

Ni ajabu kuna watu wanaamini unaweza kupanda sukuma wiki ukavuna matikiti, ukapanda kunde ukavuna nyanya au ukapanda dengu ukavuna karanga, nchi hii jamani ! Ngoma wanayoipiga Chadema ni nzito na mdundo wake ni wa kisasa na kuucheza kunahitaji wepesi katika kuhamasisha viungo vyote mwilini zaidi ya tumbo. Ndiyo maana Chadema 1. Walilitega Bunge, 2. Wakamtega Raisi na sasa hatua iliyobakia ni kumfunua mwali.

Mziki wa chadema ulikuwa umeshapendeza na soka lao lilikuwa tayari na mashabiki wa kutosha sana kusupport game zima.Ila kwa sasa itahitajika kazi kubwa sana kuludisha nyuma imani za wananchama na wapenzi kwa kuwa turufu ya mwisho ambayo ndio ilikuwa muhimu sana ilichezewa vibaya.

Wengi tulitegemea kuwa hawa jamaa siku ya PILI ndani ya IKULU tungepata jibu moja kati ya haya mawili
1: Jibu la kuwa wameafikiana na Rais kuwa HATASIGN MSWAADA WA SHERIA YA KUUNDA NA KUSIMAMIA MCHAKATO MZIMA WA UUNDAJI WA KATIBA MPYA. AU

2: Jibu la kuwa wameshindwa kuafikiana na Rais bahada ya yeye Rais kukataa makubaliano yake na wao CDM KUSITISHA KUSIGN mswaada huo na hivyo majibu yao kwa umma ni kuwa Rais wao kagoma kutekeleza maoni yao CDM ya kusitisha kusign mkataba huo.

Kukosekana kwa taarifa moja kati ya hizo mbili za aina hiyo ndiio kumeleta songombingo kubwa na ya aina yake kwenye tasinia ya siasa za Tanzania.

Kwa Watanzania CDM ilishaaanza kuwa chaguo lao la ukombozi wa Wananchi juu ya mwenendo mzima wa hatima ya Taifa lao.CDM kusema imetapeliwa na RAIS ni kukosa mashiko kwa kuwa RAIS aliyeko madarakani ni RAIS kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ambao ndio chama tawala toka mwaka 1977.Kwa kuwa RAIS ni wa CCM HAIKUWA SAWA KWA CDM KUMWAMINI ASILIMIA HAMASINI SAHAU MIA KWA KUWA YUKO PALE IKULU YA WATANZANIA KWA TIKETI YA CCM NA SIO TIKETI YA CDM.

NI UMBUMBU WA KIPUMBAVU MBALI YA UJINGA KUFIKILIA KUWA ETI RAIS AWASIKILIZE CDM PASIPO CDM KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUMUINGIZA RAISI KWENYE KITANZI [KITIMOTO] AMBACHO PASIPO HIALI YAKE ASHINDWE KUGOMEA MPANGO MZIMA WA HITAJI LA CHADEMA.

WAKAJIBWETEKEA FULL KUSHANGAA NYUMBA YAO WENYEWE,AMBAYO KWA ASILIMIA KUBWA KUPITIA PICHA KWA HISANI YA IKULU MAWASILIANO WANAONEKANA KUSHANGAA KAMA VILE ITS THE MOST PRIVILEGE HONOUR TO VISIT STATE HOUSE.

Watu waliosoma MARKETING wanajua strategy ambayo Rais Kikwete alicheza.Kilichowatokea chadema lilikuwa ni swala la KISAIKOLOJIA ZAIDI KULIKO WENGI WANAVYOFIKILIA.KAMWE RAIS JK ALICHOFANYA NI KUJUA WAKIITWA IKULU NA IMPRESSION YA RAIS KUJISHUSHA KUFIKIA KUWAHUDUMIA NA KUWAFANYA WAJISIKIE WAKO NYUMBANI BASI TAYARI ILIKUWA NI BONGE YA USHINDI.

HATA SIKU YA PILI WALIVYOLUDI SI AJABU KWA KUWA PICHA ZAKE ATUKUZIONA,WALIZUNGUSHWA NDANI YA MJENGO HUO AMBAO KAMA UKUJITAYALISHA SPIRITUAL NA MENTALLY KIMAPOKEZI NI LAZIMA UPAGAWE.KWA KUWA NYUMBA ILE NDIO THE TOP HOUSE OF ALL HOUSE IN OUR COUNTRY.

Kilichotendwa ni sawa na mtu kaingia kwenye duka kakuta Radio au TV inauzwa kwa Millioni moja [1,000,000] lakini label ya Radio au TV hiyo inaoshesha kuwa inauzwa shillingi 999,999 tu.Kama ukutayarisha akili yako vema utakulupuka kutoa fedha ukifikilia umepata aueni kumbe ni swala la Mtazamo.

Walipumbazika kisaikolojia kwa kuwa IKULU NI NYUMBA YA HADHI,na wao hawakujitarisha na mapokeo ya Mazungumzo na mazingira ya ndani ya IKULU.
Ukitaka kujua HESHIMA ya nyumba inaitwa Ikulu ikoje kasome kitabu cha Barack Obama kinaitwa "Dreams from My Father: A Story of Race and Inheritance"

Hakika Obama kwenye kitabu hicho anaelezea Ndoto [Dreams] zake za kuingia IKULU,toka wakati akipita magogoni ya USA,kwa nje miaka ya 1980s na picha aliyokuwa akiijenga na alipokuja kuingia ndani akiwa Mwanafunzi na hatimae Senator na mwisho Rais wa USA, ukifuata mtililiko mzima utajua ni jinsi gani obama alivyojitayarisha kuwa RAIS WA MAREKANI.

Hivyo CDM wamefanya jambo la AIBU kutuonyesha kuwa kumbe SPIRITUAL NA MENTALLY awajajianda kwenda kuwa wapangaji wa nyumba ile ya Watanzania kwa tiketi ya CDM.Kwa mantiki hiyo CDM HAWAJIAMINI NA HAWAKO TAYARI KUAMINIWA NA NDIO MAANA KWA UVIVU WA KUFILIA NA KWA KUTOKUWA TAYARI WANAJITOA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA.

KAMA KWELI WANAJITOA HAKUNA JINA JINGINE BORA LA KUWAPA CDM LINALOWAFAA KAMA SI JINA LA MAADUI WA UMMA [PUBLIC ENEMY].YULE ALYEAMINIKA KUWA ANGEWEZA KUPAMBANA NA MWALIBIFU NABAADHI YA WANANCHI WAKAPOTEZA MAISHA YAO KWA KUSIMAMIA SAUTI YA KIONGOZI WA UKOMBOZI HUO YANI CDM,LEO FROM NO WHERE ANAIBUKA NA KUSEMA AHUSIKI NA MCHAKATO MZIMA WA HARAKATI KWA KUWA ANAJISKIA KUFANYA HIVYO.

HAKIKA CHADEMA WATANZANIA WALIO LALA [FARIKI] CHINI YA ARDHI KATIKA BAADHI YA MAMBO AMBAYO NYIE MLIYASIMAMIA NA KUYAAMINI KISHA MKAWAAMINISHA WANANCHI BAADAE MNAIBUKA NA KUKIMBIA KWA WOGA KAMA WATOTO WADOGO JAMII HAITAWAELEWA HATA KIDOGO.

NDIO WANANCHI WAMEICHOKA CCM,LAKINI HASIRA ZA WANANCHI DHIDI YA CDM KWA UOZO WA KUJISEMEA KUWA WANAJITOA KATIKA HARAKATI ZA KATIBA ZITAKUWA MARA MBILI ZAIDI YA HASIRA DHIDI YA CCM.

CDM MTAFAKARI SANA KABLA YA KUTENDA [THINK BEFORE YOU ACT].MUWAONBE MSAMAHAA WATANZANIA NA KUKUBALI KUWA MLIZIDIWA KETE NA KUWA KWA YALIYOTOKEA MMEJIFUNZA KUWA MAGEUZI SIO LELEMAMA NA KUWA CDM SASA YAPASWA KUWA NA MWELEKEO WAKE PEKEE [UNIQUE] NA KUTUAMINISHA WATANZANIA HIVYO.

KUVUNJIKA KWA KOLEO SIO MWISHO WA UJENZI.OMBENI MSAMAHAA WATANZANIA,KWA UJUMLA WATANZANIA NI WASIKIVU NA WANAJUA PIA USHAMBA WA IKULU NDIO ULIWAPONZA MKAJIKUTA HUKO MLIKO SASA, HIYO TUNAITA NI GAME FEVER.

Mabadiliko ya Katiba

Waandishi Wetu

cdm214.jpg

Freeman Mbowe na Dr. Slaa

MAKUBALIANO kati ya Serikali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayosubiri idhini ya Rais Jakaya Kikwete, yamekiweka chama hicho njia panda kisiasa, Raia Mwema, imebaini.

Hakuna muda rasmi ulioafikiwa wa utekelezaji wa makubaliano hayo kati ya Serikali na CHADEMA kuhusu muswada huo, ambao tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwishaupitisha na hivyo, kumaliza kazi yake kwa mujibu wa Katiba iliyopo sasa.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akiwakilisha upande wa chama hicho walitiliana saini na Serikali ikiwakilishwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi. Katika makubaliano hayo, wameahidi kuendelea kuuboresha Muswada huo wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, ili kukidhi mahitaji ya kuaminiana na mwafaka wa kitaifa.

Makubaliano hayo pia yanataka kuwashirikisha wadau wengine katika kuboresha sheria hiyo, uamuzi ambao unatajwa kuunga mkono ule ushauri uliotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, ambao hata hivyo ulitaka tu kushirikisha vyama vya siasa vyenye wabunge tu.

CHADEMA awali walipinga uamuzi wa kuwashirikisha katika mazungumzo ya pamoja kati yao na Rais na vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kwa sasa CHADEMA kipo njia panda kisiasa ingawa msimamo wake kuhusu mchakato wa Katiba kuwashirikisha wananchi wengi unaweza kubaki kama awali.

Harakati za kisiasa za CHADEMA mwenendo wake sasa unategemea zaidi utekelezaji wa makubaliano hayo ambayo pia yanategemea namna Ikulu itakavyoshughulikia.

"Inawezekana kabisa Rais anaweza kutia saini muswada huo ili uwe sheria lakini katika uamuzi huo anaweza kutekeleza matakwa ya makubaliano hayo wakati wa maandalizi ya kanuni ambazo hutungwa na Baraza la Mawaziri kwa kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Lakini katika makubaliano yale tumeona kinachopaswa kufanyiwa mabadiliko ni sheria na si muswada. Kwa hiyo kwa lugha nyingine, CHADEMA wamekubali Rais asaini muswada lakini mara utakapokuwa sheria basi ifikishwe bungeni kwa ajili ya mabadiliko," alisema mmoja wa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, hatua hiyo ya CHADEMA sasa imeanza kutofautiana na ile ya NCCR-Mageuzi ambao wabunge wake waliungana na wabunge wa CHADEMA kususia muswada huo, baadhi wakisusia hata mjadala na wengine wakishiriki mjadala lakini wakisusia upitishaji wake.

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, tayari amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema; "Tulitoka nje ya Bunge ili kupinga muswada na si kutafuta njia ya kwenda kumwona Rais Ikulu. Hoja yetu ilikuwa wananchi hawajashirikishwa na bado hoja hiyo imebaki hivyo."

Kafulila anaungwa mkono na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambao kwa pamoja wanataka muswada huo urudishwe bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza.

Katika muswada huo, kati ya mambo yanayolalamikiwa ni pamoja na wananchi kutoshirikishwa kikamilifu katika kutoa maoni yao kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kaitba na Sheria, malalamiko ambayo hata hivyo, yamepingwa na uongozi wa Bunge, kupitia kwa Katibu wake, Dk. Thomas Kashilila.

Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari ambayo pia yamechapishwa katika gazeti hili kurasa za 16 na 17, Dk. Kashilila anathibitisha kuwa muswada huo umefuata hatua zote, kinyume cha malalamiko yanayoelekezwa kwa Bunge kama taasisi.

Kikao kati ya Kikwete na CHADEMA kimeelezwa kuwa ni muendelezo wa mazungumzo ya chini kwa chini ya kidiplomasia yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wastaafu na wanataaluma mbalimbali, ambao walionekana kutaka suluhu ya kisiasa kwa maslahi ya Taifa zaidi badala ya muelekeo wa awali uliokua umejikita kwenye siasa za vyama.

Mawaziri Wakuu Wastaafu, Dk. Salim Ahmed Salim na Joseph Warioba, ambao ni wana CCM, waliripotiwa kufanya juhudi binafsi za kufanya mazungumzo na wanasiasa wa CHADEMA kuhusiana na suala la mjadala wa katiba, mazungumzo ambayo hayajawahi kurasimishwa, kabla ya kikao rasmi cha Kikwete na CHADEMA.

Tayari kumekuwa na wasiwasi kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa CCM na CHADEMA kuhusu mazungumzo kati ya Kikwete na CHADEMA, kila mmoja ukihofia hatima ya mazungumzo hayo itakua nini na kwa maslahi ya nani kisiasa, hofu ambayo imeyakumba pia makundi mengine ya kijamii, ambayo hayakushirikishwa.

Mhe. Kafulila,
kama unasoma hapa, ni wakati wa wewe kusimama na kutwambia wananchi hiyo parallel process ipo au hamna. kama ipo, unaizindua lini. Kama hamna tujue moja kwamba sasa ni maumivu tu
 
- Chadema wajifunze kusikiliza mawazo ya wananchi kabla ya kukurupuka, kwenye la kwenda kwenda Ikulu wamekurupuka sasa warudi nyuma na kutafuta njia nyingine ya kushiriki kwenye katiba mpya ni lazima wawemo na zipo njia nyingi sana za kuipigisha magoti CCM ili kukubali their input, lakini kugomea is not one of them, Chadema njooni hapa mtusikilize kama mnavyofanya kwenye mengine!

- Hadithi nzima ya safari yenu Ikulu inanuka, lakini yaliyopita sio ndwele rudini nyuma mjipange upya,
Yes I am CCM damu, lakini we need you maaana kule kwetu kuna magoi goi wengi sana wanahitaji kuamushwa usingizini! na ni TAIFA KWANZA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!

Mkuu hapo kwenye Black hiyo kazi iliyowapa Chadema ina baraka za kamati kuu au NEC ya CCM? maana kama mnakubali kuwa nyie chama twawala mmelala na hamuwezi kuamka wenyewe mpaka muamshwe na tena mnaotaka wawaamshe ni chadema, kweli mtakuwa mmewapa mzigo mzito..mnastahili kuwapongeza na kuendelea kuwapa moyo.
 
Hakika Chadema kujitoa kwenu kwenye kwenye mikakati na michakato ya Mbio za ujenzi wa Katiba Mpya ya Watanzania tafuteni JINA sahihi tuwaiteje, zaidi ya Maadui wa Umma [Public Enemy].Tunaomba pia kujua kuwa Mtaishi wapi ni Tanzania au Anga yenu wenyewe?

Nawasilisha
 
Hujajibu swali la msingi mkuu??

Je madai ya chadema ni wananchi wote??

Mathalan, akawakubalia chadema kikaja kikundi kingine (say jukwaa la katiba) na hoja zao..huo mzunguko utaisha lini??

Kuweni practical kidogo siyo kulalamika kila kitu..

Kama ungekaa chini na kusoma vizuri nini CDM walipeleka bungeni na hatimaye kwa JK usingekuwa unauliza haya maswali. Nakushauri soma zile kurasa 17 sio nyingi kabla hujaja huku. Tatizo letu kubwa ni uvivu wa kusoma na wepesi wa kulaumu na kuhoji majibu ambayo yapo.
 
Nalia na mkombozi wangu chadema, mbona mnajichanganya sana. Hatukuona makubaliano ya maana baada ya kikao na jk alafu mnatuambia amekiuka kusaini. Si kweli, jipangeni vizuri na mpunguze kukurupuka. Hizi thread ni za wanachadema na watu waliochoshwa na ccm. Tafadhali msivuruge wapiga kura tukashindwa kupata ukimbozi 2015

Bila katiba mpya bora kura za 2015 ni bure.
 
Hongereni Chadema kwa kumvua nguo Kikwete na kumwacha mtupu japo washikaji wake wanamshangilia kwa kuweka madudu, hii nchi jamani ! Chadema mnaendesha siasa ya karne ya ishirini na moja lakini kwa waliozoea zile za mwaka 47 hata wakipewa darubini kali hawataweza kuona kile mlichofanikiwa. Watazamaji wengine wamechanganyikiwa jinsi boli linavyotandazwa hadi washika vibendera nao wameamua kuingia uwanjani !

Ni ajabu kuna watu wanaamini unaweza kupanda sukuma wiki ukavuna matikiti, ukapanda kunde ukavuna nyanya au ukapanda dengu ukavuna karanga, nchi hii jamani ! Ngoma wanayoipiga Chadema ni nzito na mdundo wake ni wa kisasa na kuucheza kunahitaji wepesi katika kuhamasisha viungo vyote mwilini zaidi ya tumbo. Ndiyo maana Chadema 1. Walilitega Bunge, 2. Wakamtega Raisi na sasa hatua iliyobakia ni kumfunua mwali.
Rewrite it, in reverse!
 
Ahsante sana Mkuu nakubaliana nawe katika yote uliyoyaandika. Yule SAS juzi alimuomba Kikwete kukutana ana kwa ana na Viongozi wa CHADEMA ili kutafuta muafaka wa kutunga katiba mpya, sasa Kikwete anaonyesha dalili za kutaka kuuteka nyara mjadala wa katiba na hivyo kuandika katiba ambayo Watanzania wengi hatutaikubali. Kupoteza miaka zaidi ya mitatu na labda mapesa chungu nzima kutunga katiba ambayo Watanzania wengi hatutaikubali itakuwa ni hasara kubwa kwa Taifa letu maana halii itahakikisha Magamba kuchakachua tena uchaguzi wa 2015 kupitia vile vitengo maarufu vya CCM vyombo vya dola na tume ya uchaguzi wa magamba.

Kama tulivyokwishaona sasa hivi vyombo vya dola vimepiga marufuku maandamano kwa kisingizio cha kuwepo kundi la wahuni wa kutoka Somalia bila hata kutwambia Watanzania Wasomali hao wameingia lini nchini, wako mikoa ipi na je wana silaha zipi na polisi inafanya nini katika kuhakikisha wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

- Chadema wajifunze kusikiliza mawazo ya wananchi kabla ya kukurupuka, kwenye la kwenda kwenda Ikulu wamekurupuka sasa warudi nyuma na kutafuta njia nyingine ya kushiriki kwenye katiba mpya ni lazima wawemo na zipo njia nyingi sana za kuipigisha magoti CCM ili kukubali their input, lakini kugomea is not one of them, Chadema njooni hapa mtusikilize kama mnavyofanya kwenye mengine!

- Hadithi nzima ya safari yenu Ikulu inanuka, lakini yaliyopita sio ndwele rudini nyuma mjipange upya, Yes I am CCM damu, lakini we need you maaana kule kwetu kuna magoi goi wengi sana wanahitaji kuamushwa usingizini! na ni TAIFA KWANZA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!

Willy sioni ubaya wa CDM kwenda Ikulu. Kumbuka katiba tuliyonayo, na ambayo imempa raisi madaraka makubwa na wote tunaitambua ndio yenye matatizo. CDM wamejitahidi kutafuta njia njema ili kuweza kushawishi hata wale isiyokubaliana nao na huo ndio uongozi, sio wote lazima wawe upande wako ila wanahitaji kujua unafikiri nini. Nia ya viongozi wa CDM ni kupata katiba bora kwa nchi yetu. JK anaweza kuwa na nia njema au mbaya, ila zaidi ya kuwa raisi ana utu wake. Najua anamapungufu mengi kubwa ni uwezo mdogo wa kutoa maamuzi. CDM wametimiza wajibu wao kazi ni kwake. Unapotafuta haki lazima uhakikishe umetumia silaha zote kabla ya silaha ya mwisho ya kitim tim.

Sioni ubaya wa viongozi kutafuta katiba bora kwa njia zote za maongezi kabla ya kwenda barabarani kama kina Dr king????

Najua watu wanataka fujo ili wakipake chama chetu matope. Tutapata katiba mpya bora asubuhi au jioni.
 
Mh. Tundu Lissu kwa kupitia Account yake ya Facebook Ameyaandika haya akimnukuu mkuu wa kaya:

Kichekesho: Huyu ni Rais wa nchi?

"Hata mimi naona mnazo hoja za msingi, tatizo nisipo saini wenzangu katika chama hawatanielewa." Jakaya Kikwete

sasa kama ni kweli jakaya kikwete aliyasema haya kwa mujibu wa Tundu Lissu inakuwaje leo mnyika anaitisha press na kushangaa kwamba kwanini kikwete amesaini mswaada wakati alishawaambia kuwa anatakasaini mkataba toka wakiwa ikulu.
 
Mkuu, kwani umejiuliza na kutafakari kwa makini sababu zinazowafanya wajitoe ni zipi? Rudi nyuma utathmini sababu hizo halafu urudi na jibu wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom