Uchaguzi 2020 CHADEMA yailaumu NEC kwa vifo vya mawakala watano wa chama hicho

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amewalaumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa vifo vya mawakala watano wa chadema katika ajali ya gari iliyotokea barabara ya Molo – Sumbawanga

Mnyika amesema mawakala hao wamefariki walipokuwa wanawahi ofisi za Mkurugenzi kuapishwa kutokana na utaratibu kubadilika na kuwataka mawakala wote waapishwe ofisi za halmashauri

Mnyika amesema maeneo mengine nchini hayana jiographia nzuri hivyo kuna kata ambazo hutumia muda mwingi kufika halmashauri

Aidha amesema CHADEMA wako pamoja na wanafamilia waliofiwa lakini shughuli za kuhakikisha mawakala wanaapishwa zinaendelea

Mawakala waliofariki awali walikuwa wanne, na watatu walikuwa mahututi, na mmoja kati ya kmahututi amefariki hivyo amefanya idadi ya waliofariki imefikia tano
 

Tundu Lissu atoa tamko: Figisu za uchaguzi zimeanza, Mawakala wa CHADEMA wakataliwa kuapishwa 21/10/2020​



Tundu Lissu afafanua lazima wasimamizi wa uchaguzi wazingatie Kifungu cha 7.4 Kanuni kuhusu mawakala wa wagombea wa vyama baada ya kujaza fomu namba 6 zinasema ngazi ya Kata inaweza kufanya zoezi la kuapisha na siyo lazima ifanyike ktk ngazi ya mkurugenzi
 
Kweli chadema ni vilaza na mbumbumbu, ajali ya gari unailaumu tume ya uchaguzi!!! Kweli abongo wa viongozi wa saccos wanajua wenyewe unakaa wapi ila si kichwani, maybe ipo kwenye kiungo pendwa, sio kwa comedy hii
 
chadema ni Watoto, unategemea nini kutoka kwa Mtoto? Kila kitu siyo kosa lake, cha muhimu ni kuwachukulia kama walivyo na kuwaacha kwani wengi wao ni failure hata kwenye maisha yao binafsi, ...

1603301522635.png
 
..Very sad.

..Tume ya Uchaguzi wajitafakari.

..Figisu-figusi zote hizi ni kwa faida ya nani?

..Tume haipaswi kuwa kikwazo kwa wagombea na wapigakura kushiriki uchaguzi.
Sina hakika kama kuna wa kulaumiwa katika tukio hili!!

Poleni Sana wafiwa, inauma Sana aisee, vifo vya ghafla kiasi hiko, haviwezi kuzoeleka hata kidogo!

Sisi sote ni udongo na udongoni tutarudi
 
Back
Top Bottom