CHADEMA yaigaragaza CCM kwenye kesi ya uchaguzi Simanjiro

CHADEMA yaigaragaza CCM kwenye kesi ya uchaguzi Simanjiro

Sema Kweli

Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
53
Reaction score
20
Habari zilizo tufikia hivi punde ni kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wamekigaragaza Chama Cha Mapinduzi kwenye kesi ya msingi ya kupinga kuenguliwa kwa Mgombea wa Chadema katika kijiji cha Narakauwo.

Katika hukumu iliyo tolewa na mahaka Wilayani Kiteto ni Mahakama imekubaliana na Hoja za Walalamikaji Ambao ni Bwana Saruni Ole Sanjiro kama Mgombea alie enguliwa kwa Hila za CCM kuwa alienguwa isivyo halali na mahakama imetoa hukumu ya kutengua ushindi wa hila walio upata CCM na kuamuru uchaguzi kurudiwa na wadaiwa kutakiwa kulipa Gharama zote za uendeshaji wa kesi.

Tuchukue nafasi hii kuwapongeza mawaakili wa chadema katika kesi hii na kumpongeza kwa zati kabisa Bwana saruni kwa kudai haki hii yamsingi kwa huu utakuwa ni mwanzo kwa wana simanjiro wote kujua kwamba haki huwa ipo na kuondoa tabia iliyo zoeleka kwa wana CCm kudhulimu haki za watu wengine kwa kujiona kuwa wao ndio kila kitu.

Hukumu hii ni mwanzo tu wa safari na salam za kutosha kwa MB Sendeka ambae amekuwa ndio chanzo chote cha migogoro wilayani Simanjiro.

MUNGU WABARIKI WAPENDA HAKI WOTE MUNGU IBARIKI SIMANJIRO MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Kiteto. Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kwa Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ambao uliwaweka madarakani makada wa CCM.

Awali, Mei 30 Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto ilitengua matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti wa Kijiji cha Lobosireti kwa kukiuka sheria na utaratibu.

Chadema ilifungua kesi kadhaa mahakamani hapo kupinga kitendo cha wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kufanya uchaguzi Desemba 14, mwaka jana.

Hukumu hiyo ya jana, inatokana na kesi zilizofunguliwa na Chadema wilayani Simanjiro kwenye kata za Endiamtu na Mirerani, wakipinga wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kupigiwa kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana.

Hakimu Mkazi Mfawidhi mahakama hiyo, Elimo Massawe aliagiza kurudiwa kwa uchaguzi wa viongozi wa vitongoji vya Zaire, Kisimani, Tenki la Maji, Endiamtu, Kairo na Kazamoyo vilivyoko Kata ya Ediamtu.

Hakimu Massawe alitaja vitongoji vingine kuwa ni Sekondari, Kilimahewa, Tanesco, Kazamoyo Juu, Mji mpya, Tupendane na vitongoji vya Kata ya Mirerani ambavyo ni Kangaroo, Songambele A, Getini na Songambele B.

Katika kesi hiyo, Chadema iliwakilishwa na mawakili James Millya, Shadrack Kimomogoro na Daudi Haraka na Mahakama iliamuru walipwe Sh160 milioni za gharama za kesi hiyo ambayo ilichukua takribani miezi sita hadi kutolewa hukumu.

Katibu Mwenezi wa Chadema mkoani Manyara, Ambrose Ndege alisema Mahakama imetenda haki kwa kutoa hukumu sahihi na wanajipanga ipasavyo kuhakikisha watashinda vitongoji vyote pindi uchaguzi huo utakaporudiwa.

"Tuliwaeleza tangu awali kuwa uchaguzi ukifanyika tutawashinda saa nne asubuhi hivyo tunawasubiri uwanjani na tutaongoza Mamlaka ya Mji wa Mirerani kwani wananchi wanatukubali," alisema Ndege.

Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM wa Kata ya Endiamtu, Mashaka Jeroro alisema wanatarajia kukata rufaa kupinga hukumu hiyo akisema wagombea wa Chadema walikosea kujaza fomu ndiyo sababu wakawekewa pingamizi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hiyo ni habari njema......mmmh.... habari njema kwelikweli
 
Hongereni sana watu wa simanjiro kwa kusimama kidete na kupigania haki yenu na hiyo ni ishara njema ya kitachotokea mwezi october mwaka kwa jimbo zima kuchukuliwa na chadema kwahiyo jaji ameanza mapema kutuma salamu za ushindi
 
Cc W. J. Malecela tunaomba tamko la kukemea uozo na hila dhidi ya eliyemwengua mgombea wa Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Huu mwaka wa mwisho kwa utawala wa ccm
VOTE FOR UKAWA.
 
Ni kweli kabisa kwani kwenda kudai matokeo mahakamani kwa maeneo kama Simanjiro ilikuwa kama jambo la ajbu sana ila kwa hatua hii ni ishara kwamba ukombozi sasa umewadia sio kwa simanjiro tu bali ni kwa Taifa zima.

Kesi hii ni kati ya kesi zingine zinazo endelea kiteto juu ya hujuma mbalimbali ambazo wagombea wa upinzani walifanyiwa na viongozi wa ccm kwa kushikiana na kamati ya rufaa iliyo kuwa ikiongozwa na dasi wa wilaya ya simanjiro kwa matokeo haya ya leo ni ishara kwamba hak itapatikana kwa wote kwenye kesi zilizo bakia kwani hujuma ziko sawa.

Salama kwa ccm mwaka huu wa uchaguzi mkuu ni kwamba watanzania wa leo sio wale wazamani ambao walikuwa tayari kuona haki yao ikiporwa na wao kukaa kimya,watanzania wa leo wanaju haki zao na wako tayari kuzidai popote na kwa gharama yeyote.

UMOJA NI NGUVU SIKU ZOTE.
 
Kimsingi uchanguzi ungekuwa huru ccm na serikali yake wangepata only 30% za kufutia machozi. Haya yote wamefanya makusudi ili watu wadanganyike kuwa ccm bado inakubaluka. Tutegemeni vurugu uchaguzi mkuu maana huu ni premium na watu hawatasubiri kwenda kudai mahakamani watataka ushindi wao uheshimiwe siku hiyohiyo ya kutangaza matokeo.
 
Na bado. Mpaka ile 43% ya ushindi WA CCM waliopata kwa hila irudi kwa wananchi.Ikumbukwe kati ya asilimia 78 za ushindi wa jumla waliopata CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 43% waliopata kwa wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa hila na asilimia 35 tu ndiyo waliopata kwenye sanduku la kura!
 
Hiyo si shiiiiiiiiida CCM nayo itaigaragaza UKAWA kwenye uchaguzi mkuu Oct. 2015. Najua mtakasirika lakini ukweli ndio huo.
 
Hiyo si shiiiiiiiiida CCM nayo itaigaragaza UKAWA kwenye uchaguzi mkuu Oct. 2015. Najua mtakasirika lakini ukweli ndio huo.

Maoni yako yanaheshimiwa.Kwa hali ilivyo kama mtaendelea kusema EL ni fisadi basi mapema kabisa mtashindwa na mukimteuwa mahasimu wake ndani ya CCM watasaidia UKAWA na ifikapo mchana Ukawa watakuwa wameshinda.Tatizo liko ndani ya CCM hata ukiangalia kwenye bunge sasa hivi utajuwa kuna mpasuko na hiyo ndiyo furaha ya UKAWA.."kufa kufaana"
 
Na mimi mkuu naheshimu na kuyafanyia kazi mawazo yako.
 
Watu wameelimika bwana huwezi pewa elimu ya kujua haki zako na Mh. Lema halafu ushindwe kudai haki yako. Habari njema hii natamani october iwe kesho kura ipigwe, ikianza amshaamsha ya kukumbusha watu wanachotakiwa kufanya october na huu muunganiko wa UKAWA nawaonea huruma mafisihadi.
 
Hatimaye HAKI imetendeka Katika kesi ya msingi ilofunguliwa na CHADEMA dhidi ya kuenguliwa mgombea wetu kwa nafasi ya mwenyekiti wa kijiji cha Narakawuo.

Hukumu imeshatoka na tumeshinda kwa kishindo!

Hongera CHADEMA, Hongera wakili wetu James Millya, Viongozi wa Chadema Wilaya Olesanago na Oleleshwa, Hongera Saruni Olesanjiro Mwenyekiti wetu mtarajiwa wa Narakawuo!

Uongo, ghiliba, na ulaghai kamwe haujawai ishinda HAKI....

Bado hukumu ya Jmbo zima, hiyo itakuwa trella...

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simanjiro na Mungu ibariki CHADEMA na watu wake!!!!
 
Ole sendeka akachunge ng'ombe sasa mkombozi wa wana Simanjiro ni Ole Millya
 
Back
Top Bottom