CHADEMA yahaha kumaliza mgogoro Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yahaha kumaliza mgogoro Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by loiluda, Jul 25, 2011.

 1. l

  loiluda Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni tarajio la cdm kufanya vema ktk uchaguzi ujao na hata chaguzi ndogo zinazojitokeza kama jimbo la igunga lililowazi kwa sasa,basi viongozi wa ngazi ya taifa msikurupuke kaeni na madiwani Arusha kujua kiini cha tatizo na kutafuta solution,otherwise mtakuwa mnatengeneza mwanya wa kushindwa kirahisi na ccm uchaguzi ujao,ni rai yangu kwa uongozi wa cdm kulinda imani ambayo wananchi wengi wamejenga kwenu,huu ni wakt wa kuzozana,ni wakati wa chama kujipanga ili kupata viti vingi ktk uchaguzi ujao.
   
 2. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  KATIKA kile kinachoonekana ni kutafuta suluhu ya mgogoro wa madiwani wa Chadema katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amefika hapa juzi kwa lengo la kukutana nao. Hata hivyo, hakufanikiwa kwani alishauriwa kutozungumzia mgogoro huo kwa kuwa yupo katika ngazi ya Kamati Kuu ya chama hicho.

  "Ni kweli Mbowe alikuwapo hapa tangu Jumamosi, lengo lake lilikuwa kukutana na madiwani hao lakini baadaye alishauriwa kuwa asifanye hivyo kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama," mmoja wa wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini, alilieleza gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini na kuongeza:,

  “Mwenyekiti yuko hapa, nadhani atakutana na madiwani wanaovutana na viongozi wa kitaifa akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kuhusu hatua yao ya kufikia muafaka na kukubali baadhi ya nyadhifa ndani ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Arusha,” alisema mtoa habari wetu kwa sharti la kutotajwa gazetini.

  Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni alitarajiwa kusikiliza hoja za madiwani hao na kujadiliana nao kutafuta njia nzuri na sahihi za kuchukua badala ya kutunishiana misuli na vikao vya uamuzi, kama ilivyojitokeza kwa walioamriwa kujiuzulu nyadhifa zilizopatikana kutokana na muafaka wa umeya wa jiji hilo.

  Kikao cha CC ya Chadema kiliagiza madiwani waliopata nyadhifa za unaibu meya na uenyekiti wa kamati kujiuzulu nafasi hizo ndani ya siku tatu kufikia Julai 21, mwaka huu. Madiwani hao wakiongozwa na Estomih Mallah wa Kata ya Kimandolu na John Bayo wa Kata ya Elerai wamegoma kutekeleza agizo hilo na badala yake nao wakatoa masharti ya kuombwa radhi na Dk Slaa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa madai ya kudhadhalilishwa kwa tuhuma za kula rushwa ili kufikia muafaka huo na CCM.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo, wakati jitihada za Mbowe zikigonga mwamba, mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amechukua hatua za makusudi kumaliza mgogoro huo kwa kuzungumza kwa nyakati tofauti na pande zote zinazovutana. Mtei amekutana na madiwani hao, Lema na uongozi wa Chadema kuzungumzia mgogoro huo akitaka pande hizo zinazovutana zimalize tofuati zao kwa busara.

  Mtei alikutana na madiwani hao baada ya kumwomba afanye hivyo ili kuumaliza kwa amani badala ya kuvutana hadharani. Madiwani hao wa Chadema wilayani Arusha walikutana na Mtei nyumbani kwake Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha mwishoni mwa wiki na kuomba ushauri juu ya mvutano huo unaoendelea kukipasua chama hicho.

  Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Mtei hakukiri wala kukataa kukutana na madiwani hao. Alisisitiza kuwa Chadema hakiwezi kumeguka kutokana na mgogoro huo. "Sisi (Chadema) tuna mipango na sera zenye matumaini kwa Watanzania, hatuwezi kumeguka kwa mgogoro huo."

  Hata hivyo, Mtei aliwataka viongozi wa Chadema, madiwani wake na Lema kutumia busara na kupunguza jazba katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

  Source: gazeti la Mwananchi, July 25, 2011

  Chama cha Magwanda; TUONDELEENI UGOMVI ARUSHA, wananchi wanataka maendelea kupitia vikao vya madiwani!!!
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  At least sasa madiwani wameanza kutia akili kuliko kukimbilia magazetini kitu ambacho kingezidi kuwaweka mbali na chama.
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye blue. Tuondolee ushangingi humu jf. Ushangingi wako peleka huko huko kwa hao magamba wenzio.
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Kwanza kutokuelewana sio tatizo kwa binadamu!Unapoona mtu anashabikia mambo mepesi kama haya ujue uwezo wake wa kufikiri ni matatizo,hebu kaeni chini na mjibu mlolongo mrefu wa matatizo ya kuwafukarisha watanzania tangu uhuru!
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Feedback, unapenda sana kujifariji na kujiliwadha na msongo wa mawazo uliyokuwanao! wapi Madiwani wameanza kutia Akili? Wakati msimamo wa Madiwani upo palele wanataka Slaa, na Lema. wawaombe msamaha kwa kuwasingizia kuwa wamachukuwa rushwa kutoka Magamba
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kitendo cha madiwani kurudi kwa wazee wa chama ni hatua ya kujirudi.
   
 8. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ushindi wa 2010 umeshaanza kuwaingia kichwani chadema!
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hakuna ata Diwani mmoja aliekwenda kwa wazee! Mzee mtei ndio kaamua kuingilia kati suala hilo kuongea na pande zote
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Duh!! haya madiwani walikwenda kwa Mzee Mtei wa CCM.....umefurahi sasa.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Utakuwa wakati muafaka kuhakikisha kwamba mgogoro kati ya madiwani na chama unamalizwa kwa njia inayofaa, vilevile chama pamoja na madiwani wana kazi kubwa ya kurudisha heshima ya chama kwa wananchi.
  Suala la mauaji ya Arusha pamoja na kesi iliyopo mahakamani. Tunataka serikali itoe tamko kuhusu mauaji ya Arusha. Kuhusu kugawana vyeo haikuwa mmoja ya masharti ya chama kwenye muafaka unaoendelea kati ya chama na serikali.
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hivi inawezekana kweli mgogoro huu wa arusha ukamalizika bila madiwani wa chadema kushiriki katika uongozi wa manispaa??

  Najaribu kufikiria na kuangalia alternative, kwakuwa ni lazima ifike mahali madiwani wafanye kazi za maendeleo ya wananchi, hawawezi kuwa katika mvutano kwa miaka yote mitano. Pengine wakazi wa arusha mna mtazamo ama maoni gani kuhusu njia bora ya kumaliza kabisa tofauti zilizopo huko baina ya madiwani wa chadema na uongozi wao wa kitaifa na dhidi ya meya wa jiji.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mwita Maranya,

  kwakuwa chama kama chama inaongozwa kama taasisi, ninahakika watafikia mahali sasa wakaamua kutumia hekima na busara, kuitumia katiba ya chama vizuri mgogoro ukaisha kwa namna inayofaa na kwa njia ambayo hata wananchi wakaelewa na kuwa na imani na chadema.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kama kamati kuu imetoa maelekezo kwa madiwani kujiudhulu nyadhifa walizojipatia kupitia muafaka, na madiwani wamekaidi, ni katiba gani ama kipengele gani cha katiba viongozi wa chadema wanaweza kukitumia kuumaliza huo mgogoro??

  Mi nadhani katika hili uongozi wa Taifa wanalazimika kukubaliana na muafaka wa madiwani wake ama vinginevyo waamue kutupa jongoo na mti wake.
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Who blinked first kati ya pande hizi mbili.Wote hawana fall back position lakini Kamati Kuu stands to lose face.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Haya Feedback, madiwani wamejiuzulu nyazifa zao umefurahi ehee! piipozzzz!!
   
 17. M

  Maskini Jeuri Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narejea kauli ya kwanza toka kwa katibu wa
  CDM "CHADEMA ipo tayari kupoteza chochote
  Hata Kama Ni kizuri na kitamu namna gani Kama
  Hakikupatikana kwa njia ya Demokrasia ya kweli na
  Haki"
  My take,
  Hakuna haja ya kuendeleza huu mjadala Kama
  CDM Ni wasimamizi wa Democracy Kama logo yao
  Ilivyo. Wananchi Ni waelewa!
  Umaarufu wa Mallah umeletwa na CDM bwana
  Na tunamfahamu, tatizo hapa Ni posho za vikao.
  Na Kama Lema na yeye anahusika kwa namna yoyote
  Ile, nae apewe kibano. Mkikubali hadaa ya magambaz
  Kwenye kufunga hiyo ndoa mmeliwa.
  Huu Ni mtizamo wangu!
  Tena kulikuwa na agenda gani Kati yao na msaliti shimbunda!
   
Loading...