Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza ziara zake rasmi za kukutana na wanachama katika jimbo hilo kwa lengo la kukagua uhai wa chama, pamoja na kufanya tathmini ya uchaguzi wa mwaka Jana 2015. Ziara hiyo iliyoongozwa na viongozi wa jimbo pamoja na aliyekuwa mgombea wa ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA (EMMANUEL KIMEA) imeanza leo katika vijiji kata ya Kwashemshi na Kerenge na inatarajiwa kuendelea katika kata nyingine za jimbo hilo.
Katika Ziara hiyo pia msafara huo umeambatana na madiwani wa Chadema katika jimbo la Korogwe vijijini ili kutoa chachu kwa kata nyingine kuchagua viongozi wa Chadema kwani ndio ambao wanatekeleza mambo wanayoahidi.