CHADEMA Yaanza Kuwanoa Wagombea Ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Yaanza Kuwanoa Wagombea Ubunge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Regia Mtema, May 25, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kinatarajia kuanza Mafunzo kwa Wagombea Ubunge Watarajiwa. Mafunzo hayo yanalenga kutoa Mafunzo muhimu kwa Wagombea hao ambayo yatakwenda sambamba na mafunzo kwa Makatibu wote wa Majimbo, Wilaya na Mikoa. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa Mfumo wa Kanda kama ifuatavyo;

  Kanda ya Kati- Dodoma,Morogoro na Singida ambapo Kituo cha Mafunzo kitakuwa Dodoma. Mafunzo yatafanyika tarehe 1-2 Juni 2010.

  Kanda ya Magharibi – Tabora,Kigoma,Shinyanga na Rukwa ambapo Kituo cha mafunzo kitafanyika Tabora.Mafunzo yatafanyika tarehe 1-2 Juni 2010.

  Kanda ya Ziwa- Mwanza,Mara na Kagera- ambapo Kituo cha mafunzo kitafanyika Mwanza.Mafunzo yatafanyika tarehe 5-6 Juni 2010.

  Kanda ya Kaskazini- Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo Kituo kitakuwa ni Arusha.Mafunzo yatafanyika tarehe 5-6 Juni 2010.

  Kanda zilizobaki Ratiba itatangazwa baadaye baada ya Mafunzo haya.

  Wale wote wanaotarajia kugombea na bado hawajaza fomu za chama,mnashauriwa kujaza fomu hizo mapema iwezekanavyo.Fomu zinapatikana kwenye ofisi zote za Mikao,Wilaya na Makao Makuu au tembelea website ya chama; www.chadema.or.tz

  Wagombea warajigharamia nauli lakini Chakula na Malazi vitagharamiwa na chama.

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na

  Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo -Bw Benson Kigaila 0787 383167, Afisa Mafunzo- Bi Regia Mtema- 0713 760534 au barua pepe regia@chadema.or.tz au John Mnyika 0784 222222, 0754 694553 au barua pepe mnyika@chadema.or.tz.


   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tumekupata mkuu. Tupo pamoja.
   
 3. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtu akikushawishi uichague chadema sema baabaa aaapeeeendiii!
  Ila akikwambia mchague John Mnyika sema hapo ndipo peenyeewee
   
 4. M

  Mkono JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii nimeipenda sana ,washa moto wapambanaji.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  May 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Changamka kama wataka kugombea na wewe usije ukapitwa na mafunzo haya muhimu mno.
   
 6. L

  Luveshi Senior Member

  #6
  May 25, 2010
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Naomba niongeze na Dk Slaa, Zitto, Tindu Lissu, na Dr Kitila kama kama atajitokeza.
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  May 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wote hao wanatarajia kugombea Mkuu..Ila Kitilla hagombei mwaka huu..
   
 8. L

  Luveshi Senior Member

  #8
  May 25, 2010
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Imenisikitisha hii, nadhani Dr badala ya kukaa nje alipaswa kuingia uwanjani.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  May 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jitahidini kumshawishi afanye hivyo..Hata sisi tunasikitika kumkosa mjengoni..
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tuwahamasishe wapigaji vijana kugombea kupitia CHADEMA, kwani tumeona mchango wa wabunge wa chadema pamoja na uchache wao. Kwa hiyo tusisite kuwahamasisha kugombea kupitia chadema. CHADEMA ni chama cha kuungwa mkono katika harakati ya kuleta mabadiliko TANZANIA.

  Mimi nawaunga mkono, wewe unasubiri nini?
   
 11. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mafunzo ya nini kura zimaibwa... hamna chenu..lol
   
Loading...