Chadema ya tumia plan b kueneza m4c.

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,282
9,913
Baada ya CDM kuingia katika msuguano na Serekali, Chadema kimebadilisha mbinu za kujiimarisha, chama hicho sasa kubuni mbinu nyingine ya
kujiendesha. "Tuko huko Mufindi tunajenga chama, vikao kila wakati," alisema Dk Slaa alipoulizwa yuko wapi na anafanya nini. Dk Slaa alisema CCM na Serikali yake, itajuta
kuzuia mikutano ya hadhara ya Chadema kwani baada ya uamuzi huo, chama hicho kimekuja na njia nyingine ya kujijenga maeneo ya vijijini.
"Hawa watajuta (CCM na Serikali) kuzuia mikutano yetu. Sisi tumekuja na njia nyingine
ya kukijenga chama vijijini," alisema Dk Slaa ambaye hata hivyo, hakubainisha njia gani
anayotumia sasa kukijenga chama hicho cha upinzani.

Alipoulizwa atamaliza lini ziara yake hiyo ya kukijenga chama kwa njia mbadala, alijibu," Tulipanga kutumia siku 44 katika mikoa mitano, lakini nadhani siku hizo zitaongezeka baada ya mikutano yetu kuzuiwa.”

Mwanzoni mwa mwezi huu, Chadema kilianza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini katika kile wanachokiita Movement for Change (M4C).
Hata hivyo, wakiwa mkoani Morogoro, chama hicho kiliingia katika mgongano na polisi katika
vurugu zilizosababisha kifo cha mfuasi wake mmoja na majeruhi wawili.
Baadaye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema aliipiga marufuku mikutano na maandamano ya chama hicho iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kwa kile kilichoelezwa
kuwa ni kupisha Sensa ya Watu na Makazi.
 
Sensa inaisha Jumapili. Mikutano ya hadhara ni haki ya chama chochote cha Siasa!. Mwema atafute sababu nyingine haraka haraka. Vinginevyo ziendelee plan B na A kwa pamoja!.. Mungu awatangulie Makamanda!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom