CHADEMA ya baridi, CHADEMA imepoa chali

CHADEMA ya baridi, CHADEMA imepoa chali

The Giantist

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2018
Posts
214
Reaction score
86
Tangu tuanze kushiriki uchaguzi wa vyama vingi vya siasa katika siasa za Tanzania mwaka 1995. Ni wazi kuwa vilizuka vyama vingi kwa vipindi tofauti na vilionesha umadhubuti wa kujaribu kuchuana na Chama Dume CCM. Tunafahamu historia vizuri kwamba kilianza NCCR-Mageuzi, kikafuata CUF, kisha CHADEMA.

Na kwa kusema ukweli CHADEMA hiyo haikuwekwa kwa juhudi za wana-CHADEMA wenyewe katika mwaka 2015 isipokuwa ni makapi ya CCM wakiongozwa na Mzee Lowassa hata kukifanya CHADEMA kionekana walau chama, chenye uthubutu katika kupambana na CCM kwenye. Ndio kusema kuwa karibu sehemu kubwa ya matokeo ya kura ya Mzee Lowasa yalichagizwa na baadhi tu ya makapi ya CCM. Ukweli anajua Mwenyekiti Mbowe.

Sasa ni miaka mitano tangu wimbi lile la Mzee Lowasa lipite na pia ni zaidi ya mwaka tangu. Mzee Lowasa arejee kwao CCM. Mpaka sasa CHADEMA inaonekana imepoaaaaa baridiiiii. Na hii ni ishara ya wazi kuwa:

Mosi, hawana tena ajenda madhubuti kwa ajili ya ustawishaji wa maisha ya watanzania. Kwa maana hakuna tena ajenda kwenye Huduma za jamii, kama vile Elimu, Afya na Maji. Kwa miaka mitano ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya uchaguzi ya 2015/2020. Mmeshuhudia jinsi ambavyo serikali imepoga hatua katika kuhakikisha jamii inastawi na kukua kwa kuziboresha huduma zote tatu za jamii. Sisemi sana ila ni matumaini yangu kuwa mnaona na baro mnaendelea kushuhudia yanayoendelea hata sasa.

Pili, ni dhahiri kuwa ile ajenda kuu ya CHADEMA kwamba Demokrasi na Maendeleo haina tena mashiko kwa wananchi na ukizingatia kuwa wananchi wamekwisha ona Demokrasi ikitendeka kwa uwazi na haki na usawa na kwamba maendeleo yameweza kupatikana kwa kuwepo kwa demokrasi pana ndani ya nchi. Inafahamika kuwa hakuwezi kuwepo na matendo ya rushwa na ubadhirifu sambamba na demokrasi! Kwa hiyo Ilani ya CCM chini ya jemedari DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, imefaulu kwa kiasi kubwa mno katika mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na uzembe katika utendaji wa kazi ili kujenga Demokrasi pana na kuleta maendeleo ya nchi.

Tatu, ajenda ya kwamba tangu tupate Uhuru Tanzania haijawahi kumiliki hata kandege, hako kaajenda kamekwisha kufilia mbali hakapo tena. Nafikiri CHADEMA hapa watakuwa wamefurahishwa sana, kwani wamekwishaletewa Ndege za kutosha ipo Boeng, Airbus, Bombardier n.k Mungu awape nini tena ndugu zetu CHADEMA. Hivyo basi ni wazi kuwa kutekelezwa kwa ilani ya CCM kwa ukamilifu na kwa kiwango kikubwa zaidi, umekuwa ni mwiba mkubwa sana katika kuendeleza siasa za CHADEMA. Hiyo haitoshi pekee, suala la maboresho ya uangalizi wa anga ya Tanzania, kwa kununuliwa Rada kubwa na za kisasa. Nikiyasema yote sitaweza kumaliza, lakini kumbuka maboresho yna ujenzi wa viwanja vikubwa vya kimataifa vya Ndege, usiisahau Songwe International Airport.

Nne, sekta ya Nishati. Watanzania ni mashuhuda katika upande huu. Kwa wastani katika miaka yote ya utekelezaji wa ilani ya CCM ni katika miaka mitano ya DKT. MAGUFULI JOHN POMBE, ni umeme wa kutosha umepata kutumika zaidi kuliko miaka mengine. Hii maana yake nini, hakukuwa na kero za kukatika umeme mara kwa mara, hii imesababishwa na utendaji kazi imara wa shirika letu la umeme, pamoja na kuwepo kwa mitambo Safi ya kuzalishia umeme. Hii pekee yake haitoshi. Kumbukeni mradi mkubwa ambao utaenda kumaliza kabisa tatizo la umeme nchini Julius Nyerere Hydropower!

Tano, utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutumia fedha zetu wenyewe, ikiwa ni pamoja na SGR, Daraja la Surander, utanuzi na ujenzi wa flyover Ubungo, na Mfugale Bridge, ujenzi wa viwanda n.k kubwa na kuliko yote ni kufanikiwa kulifikisha taifa katika uchumi wa kati!

Naomba niishie katika hoja zangu hizi Tano ili kwamba kila hoja iweze kuwakilisha mwaka wa ombwe ya pili ya uchaguzi wa mwaka 2020-2025 yaani mitano mengine. Sasa CHADEMA kimekufa ajenda, kimekufa uthubutu, kimekufa nguvu kimekufa morali, kimekufa chakali na hata kimepoteza mvuto.

Giant
Suati ya Mdodomia
 
Mkuu mada yako ina ukweli ila miradi ya kimkakati inatumia mikopo, kama SGR ni pesa ya Exim Bank! tafuta data kamili!
 
Huyo jemedari wenu anatakiwa atoe maelezo yakwanini alitaka kumuua Lissu kwa kiroba cha marisasi?
Bahati nzuri atatakiwa kujibu wakati wa kampuni!
 
Freeman Mbowe is not fit for purpose.
 
Wewe ni mjinga anayefurahia siasa dhalimu za ccm kuzuia wapinzani na kuwapiga na wengine kuwaua. Huoni kuna shida kwa sasa jinsi nguvu ya dola inavyoharibu siasa na demokrasia ya Tz, au unataka watu wafanye fujo ndio uone kwamba wana nguvu?
 
Write your reply...
Tatizo ni yule dikteta kufungia vyombo huru vyote vya habari vimebaki vile vya kumsifu na kumtukuza tu. Sasa habari za Chadema utazipataje
 
chadema, chadema kila siku, leteni mada zingine, kama imepoa unatuletea mada ya kitu kilichopoa ya nini? watu tunataka vya moto
 
Back
Top Bottom