Chadema ya 2005 sio hii ya sasa..lkn pia Ccm ya 2005 sio hii ya Magufuli

karanga mbichi

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
269
222
Ukiwatazama UKAWA na Mbowe wao unaweza ukawaita jina lolote ama la dharau au la kishujaa, itategemea wewe muitaji Upo upande upi....
Niwakumbushe kitu kimoja, mwaka 2010 baada ya chadema kushindwa kuna watu walisema haitakaa washinde tena.... Ukweli mwepesi tangu 1995 mpaka 2015 miaka 20 sasa chadema haijawahi kupunguza idadi ya wabunge, mm naamini ata 2020 idadi ya wabunge wao itaongezeka.
Upinzani walioutoa chadema 2005 ikiwa ndo uchaguz wao Wa kwanza kusimamisha mgombea uraisi ni nusu ya 2010 na 2010 haufikii ata Robo ya ule Wa 2015.
Ni waambie wana ccm ata hili la bunge kutoonyeshwa kwa hoja nyepesi ata wanaccm linawakera. Mbowe anauliza TV zilizofungwa kwenye maofisi ya serikali ni za nn?. Mm namjibu labda za kutazama mziki maana wakati bunge linaendelea kuna muda TBC inaonyesha mziki tena Wa hovyo.

Lkn niwakumbushe UKAWA kitu kimoja ukiutazama mwenendo Wa ccm kizazi mnachopambana nacho sasa sio mtakachopambana nacho 2020. ccm ina hazina ya vijana weengi wanaokifia chama chao na kibaya zaidi wameanza kuingizwa kwenye mfumo, jinsi jasho linavyowatoka kupambana na magufuli km MTU mmoja kuna akina magufuli 20 watatoka 2025.
Ukawa ni wakati wa kuwatumia na kuwekeza kwa akina mtatiro, lijualikali, malya kwa idadi ya majimbo sasa ili kupambana vzr 2025, vingnevyo ccm itawasumbua kwa kuwa ina nafasi kubwa ya kuwatumia vijana wao kupitia majukwaa mbali mbali ya kiserikali.
 
WENZAKO WANAKUJA LAKINI BADO WANAPATA KIFUNGUA KINYWA.
12115800_10209157111354180_2363078490445719886_n.jpg
 
Back
Top Bottom