Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 21,193
- 33,577
kamanda nakumbuka kuna siku uliwauliza " je zile sababu za kususia uchaguzi uliopita zimefanyiwa kazi?? wakakutukana
Wangekua wanasikiliza ingependeza zaidi.Ndugu zangu makamanda.
Kwanza poleni sana. Naona siku hizi mambo hayawaendei vizuri hususan kwenye chaguzi.
Hivyo ningependa kuwapa maneno mawili matatu ambayo naona yanaweza kuwafaa huko mbeleni.
Ni hivi, ifike mahali sasa mkane kuhusishwa na watu wanaowapa sifa na taswira mbaya kwenye jamii.
Watu ambao kazi waiwezayo ni kutukana matusi ya nguoni na kuchafua wenzao mitandaoni, kataeni kabisa kuhusishwa nao.
Mfano, huko Marekani ikitokea mgombea flani labda anaungwa mkono na limtu libaguzi au lijambazi, basi mgombea huyo atalazimika kuweka bayana msimamo wake kuwa hataki kuungwa mkono na limtu la hivyo na kama labda alipokea mchango wa fedha toka kwa hilo limtu, hizo fedha zitarudishwa.
Na nyinyi ifike wakati sasa muweke bayana kuwa hamtaki endorsement ya namna yoyote ile kutoka kwa yeyote yule ambaye kazi yake ni kutukana matusi yasiyo na mwisho.
Msiachie watu wanaoharibu taswira ya chama chenu ndo wa control the narrative kisa tu wanawatukana na kuwachafua mnaopingana na kushindana nao kisiasa.
Mnapokaa kimya bila ku denounce watu wa namna hiyo mnaishia kuonekana kama mnakubaliana na matusi yao kwa wengine.
Kama kweli chama chenu kina lengo la kuja kushika dola na kuunda serikali basi hamna budi kuhakikisha kuwa mbele ya jamii mnaonekana ni wenye uadilifu uliotukuka.
Kwenye siasa perception ni muhimu sana. Na perception hiyo hiyo ndo huwa uhalisia.
Jiangalieni.