Chadema watumie staili ipi ili kushinda viti vingi vya ubunge?

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Ndugu wanaJF,

Ibara ya 63 na 64 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataja wazi wazi Majukumu ya Mbunge ni "Kuisimamia na kuishauri Serikali kwa niaba ya wananchi wa Jimbo analotoka". Kwangu mimi naona Wabunge ndio wanaotuangusha kama Taifa kwa kutotimiza wajibu wa ipasavyo.

Hali ya Wabunge kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo sio jambo la bahati mbaya; ila ni mkakati maalum wa CCM kuua Check and Balances katika Governance ya Nchi Hii. CCM imefanikiwa kufanya hivyo kwa kutopatiwa wananchi elimu ya uraia kabalaya kuanzisha Mfumo wa Vyama vingi vya siasa kama ilivyopendekezwa na Tume ya Nyalali. Hivyo idadi kubwa ya watanzania hawafahamu kazi kubwa ya Mbunge. Wengi wanaamini kuwa Kazi ya Mbunge ni kuleta maendeleo k.m kujenga madarasa, zahanati, hospitali, kutandika mabomba ya maji safi, kutoa mikopo n.k katika Jimbo analotoka; hata kama maendeleo hayo ya Jimbo moja yanapatikana kwa kuhujumu maendeleo ya watanzania wengine wote hata kufikia watanzania wengine kupoteza maisha kwa kukosa huduma, dawa, kutoweza kufika hosapitali kwa kukosekana barabara n.k

Kwa kuwa idadi kubwa ya watanzania hawajui "Kuisimamia Serikali maana yake ni nini"; Wabunge wengi wamekuwa wakihukumiwa na wananchi kwa maendeleo kiasi gani kaleta katika Jimbo lake na kushindwa kupima kazi Mbunge husika alizofanya katika nyanja ya "Kuisimamia Serikali"

Kwa kulitambua hilo wabunge wengi tunaowachagua wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta maendeleo kwa Majimbo yao tu. Wengi hufikia hatua ya kuwapigia magoti Mawaziri na Watendaji wa Serikali ili kupatiwa maendeleo katika Majimbo yao ili waweze kuchaguliwa tena. Hivyo kazi ya Kuisimamia na Kuishauri Serikali haiwezi kufanywa na Mbunge anayetafuta huruma ya Mawaziri na Watendaji wa Serikali ili aweze kuchaguliwa tena.

Kwa kufanya hivyo CCM imefanikiwa kuiondolea Serikali yake watu waliopaswa kuwanyapara au kuwasimamia kwa niaba ya wananchi. Matokeo yake viongozi na watendaji wa Serikali ya Tanzania wamebweteka, hawawajibiki kwa wananchi. Viongozi na watendaji wa Serikali hujihusisha katika vitendo vya wizi, ubadhirifu na uhamishaji wa rasli mali za taifa wanavyotaka kwa sababu wanatambua kuwa hakuna mtu wa kuwahoji. Hivyo kodi hazikusanywi vya kutosha, madini yetu hayana mwangalizi, mbuga za wanyama hazina mwanagalizi, vivutio mvy utali havina mwangalizi n.k.

Laiti kama wananchi tungekuwa tunawahukumu wabunge kutokana na mchango wao katika kuisimamia Serikali, mapato yote yatokanayo katika vyanzo vilivyotajw hapo juu yangekusanywa vizuri chini ya usimamizi wa wawakilishi wa wananchi, yaani wabunge, kutunzwa na matumiz yake yangeweza kusimamiwa vyema ili kuleta maendeleo katika majimboni yote kwa uwiano sawa.

Athari ingine ya wananchi kuwahukumu wabunge kwa kiwango cha maendeleo kilichofika Jimboni na sio uwezo wa mbunge kuisimamia Serikali; ni CCM kutumia utaratibu huo kuwakomoa wananchi wanaochagua madiwani na wabunge kutoka vyama vya upinzani kwa kuwanyima maendeleo ili wakome kuchagua wapinzani.

Athari ingine na mbaya zaidi ni kuporomoka kwa mfumo wa utoaji huduma kwa wananchi na kushamiri kwa rushwa kutokana na viongozi na watendaji wa Serikali kujua kuwa hawana mtu au chombo cha kuwasimamia.

Athari ingine mbaya sana ya mfumo hio ni wawekezaji na mafisadi kufadhili ujenzi wa madarasa, zahanati, mabomba ya maji n.k katika baadhi ya majimbo na hivyo kuwatumia wabunge kutoka majimbo hayo katika kupitisha miswada ya sheria na haja za kuruhusu uhamishwaji wa rasli mali za Taifa.

Vile vile Mafisadi walioliibia Taifa hili hutumia kiasi kidogo cha fedha walizoliibia taiafa hili kujenga maendeleo hayo katika majimbo ambayo wao ni wabunge kama vile Igunga, Bariadi, Monduli n.k na hivyo watanzania kuendelea kuwachagua tena na tena kwa kuamini kuwa wabunge hao wanatimiza wajibu wa Mbunge, hata katika kipindi chote cha miaka mitano ya Bunge liliopita Mapapa wa Ufisadi ambao ni wabunge kutoka majimbo hayo hawakuwaha hata siku moja kuanzisha aua kutetea hoja yoyote yenye maslahi kwa taifa. Lakini upo ushahidi wa jinsi walivyoshiriki kuliibia taifa.

Hivi sasa katika vugu vugu hili la watanzania kutaka mabadiliko katika chombo cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali yaani Bunge na kuhazimia kuchagua wabunge wengi wa upinzani; tufanya nini ili kuwaelimisha wananchi yafuatayo:-

a) Wananchi waondokane na Ubinafsi wa kutaka maendeleo ya majimbo yao kabla ya Taifa? Kwa maana wawachague wabunge wenye uwezo wa kwenda kufanya kazi ya Taifa kwanza na wawapime kwa kigezo hicho na sio maendeleo ya Jimbo.

b) Namna ya kumpima mgombe Ubunge; Yule atakaye tanguliza maslahi ya Jimbo wananchi wajue kuwa hajui majukumu ya Mbunge, nafasi anayoomba. Bali yule atakayeonyesha kujua Tanzania ina utajiri kiasi gani na atafanya nini kuhakikisha utajiri huu unakusanywa ipasavyo katika kapu kuu na kisha kusimamia matumizi yake kwa majimbo yote sawia.

It is suicidal kwa wabunge zaidi wa upinzani kuingia katika chombo hicho bila jitihada kufanyika mind set ya wananchi kuhusu "Kazi na Majukumu ya Mbunge".

Naombamawzo yenu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom