CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya.

Nimesha waambia siku nyingi hawa jamaaa
Walimdhalilisha baba lowasa eti ni fisadi kumbe ushahidi hawanaa kabisaa
 
Mbowe anasema na ninanukuu

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza.

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Wananchi wanahoji

Hivi walipomtaja Lowasa kama number one fisadi in Tz walikuwa na ushahidi? Je, hawakufahamu kuwa ni mtu mwenye nyadhifa nyingi na kumtaja tu ni kumchafua???

Mkuki kwa nguruwe....
Eti wananchi? Sema wewe ndio unahoji acha kusingizia wananchi.
 
Swali la kufikirika?hivi kama mtu anajihusisha na uuzaji wa hayo madawa,aka save kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha,Je kesho na kesho kutwa ataendelea na biashara hiyo?
 
Mbowe anasema na ninanukuu

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza.

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Wananchi wanahoji

Hivi walipomtaja Lowasa kama number one fisadi in Tz walikuwa na ushahidi? Je, hawakufahamu kuwa ni mtu mwenye nyadhifa nyingi na kumtaja tu ni kumchafua???

Mkuki kwa nguruwe....
Chama chochote cha upinzani hakina dola.Maana yake hakina wapelelezi, mapolisi na mahakama.Hivyo, inapotokea kuna tuhuma kama alizopewa Lowassa na mahasimu wake wa kisiasa ndani ya CCM na kupigiliwa nyundo na Tume ya Mwakyembe ni kazi ya wapinzani kupaza sauti kuwataka serikali wachukue hatua dhidi ya tuhumiwa. Serikali inapoambiwa kupitia vyombo kama bunge na wao kushindwa kuchukua hatua hapo ndipo wapinzani wanaamua kuishitaki serikali kwa wananchi ili waiadhibu serikali kupitia sanduku la kura.

Hivyo, vyama vya upinzani walifanya hivyo baada ya serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya tuhuma zilizoonyesha ushahidi (kwa mujibu wa Tume ya Mwakyembe).

Tukija kwenye hili linalofanywa sasa hivi ,hatuwezi kuliunga mkono kwa kuwa Serikali ina kila chombo chenye mamlaka ya kuchunguza, kukamata na kuadhibu. Sasa iweje Watu wanaitwa tena kupitia vyombo vya habari, hakuna ushahidi, mnaishia kuwaonya na kauli kuwa mnawachunguza na mwisho mnawachia huru kwa kuwa hamkujiandaa.

Tambua kuwa ,kitendo cha kumhusisha mtu na tuhuma nzito tena kwa kumtangaza kwenye vyombo vya habari ,mtu huyo hasafishiki kilahisi. Sasa kwanini umuharibie mtu maisha yake bila mafanikio uliyotaka kuyapata?

Kama kweli ni vita halisi kwanini wasipandikizwe wapelelezi watuhumiwa wakamatwe redhanded (wakiwa na vidhibiti) ? Ili kesi hizo ziwe na mashiko kisheria.

Kitendo kinachofanywa hivi sasa kina haribu maisha na hadhi za watu. Wakati serikali ina kila kitu ingeweza kuwakamata wakiwa na ushahidi kuliko hivi sasa unawaita ,wanaaibika alafu huwashitaki kwasababu huna ushahidi.

Tuheshimu utu wa watu, Tanzania ni yetu sote.Msifanye raia wengine wawe wanyonge kwenye nchi yao.
 
Jamani HIVI FAO LA KUJITOA LINARUDI LINI? Naona ccm wamefanikiwa kudivert attention muhimu ktk taifa. Ikiwemo ccm kula rambirambi za wana KAGERA na sakata la uhaba wa mvua na NJAA nchini....
 
Chama chochote cha upinzani hakina dola.Maana yake hakina wapelelezi, mapolisi na mahakama.Hivyo, inapotokea kuna tuhuma kama alizopewa Lowassa na mahasimu wake wa kisiasa ndani ya CCM na kupigiliwa nyundo na Tume ya Mwakyembe ni kazi ya wapinzani kupaza sauti kuwataka serikali wachukue hatua dhidi ya tuhumiwa. Serikali inapoambiwa kupitia vyombo kama bunge na wao kushindwa kuchukua hatua hapo ndipo wapinzani wanaamua kuishitaki serikali kwa wananchi ili waiadhibu serikali kupitia sanduku la kura.

Hivyo, vyama vya upinzani walifanya hivyo baada ya serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya tuhuma zilizoonyesha ushahidi (kwa mujibu wa Tume ya Mwakyembe).

Tukija kwenye hili linalofanywa sasa hivi ,hatuwezi kuliunga mkono kwa kuwa Serikali ina kila chombo chenye mamlaka ya kuchunguza, kukamata na kuadhibu. Sasa iweje Watu wanaitwa tena kupitia vyombo vya habari, hakuna ushahidi, mnaishia kuwaonya na kauli kuwa mnawachunguza na mwisho mnawachia huru kwa kuwa hamkujiandaa.

Tambua kuwa ,kitendo cha kumhusisha mtu na tuhuma nzito tena kwa kumtangaza kwenye vyombo vya habari ,mtu huyo hasafishiki kilahisi. Sasa kwanini umuharibie mtu maisha yake bila mafanikio uliyotaka kuyapata?

Kama kweli ni vita halisi kwanini wasipandikizwe wapelelezi watuhumiwa wakamatwe redhanded (wakiwa na vidhibiti) ? Ili kesi hizo ziwe na mashiko kisheria.

Kitendo kinachofanywa hivi sasa kina haribu maisha na hadhi za watu. Wakati serikali ina kila kitu ingeweza kuwakamata wakiwa na ushahidi kuliko hivi sasa unawaita ,wanaaibika alafu huwashitaki kwasababu huna ushahidi.

Tuheshimu utu wa watu, Tanzania ni yetu sote.Msifanye raia wengine wawe wanyonge kwenye nchi yao.
Pamoja na maelezo yako marefu lkn tume ya mwakyembe kaikuwa na ushahidi bali walikuwa na mashaka juu ya taratibu zilizotumika. Na kama ushahidi ungekuwapo lowasa angekuwa wa kwanza kushitaji mahakama ya mafisadi. Kashfa ni kashfa na makonda karusha jiwe, mbowe hakupaswa kuguna. Mwenyekiti wetu ni mpambanaji asingeweka hoja juu ya hili. angekuwa tu positive na kusema ataripoti ili nae awe na credibility ya kupambana. Au hadhi gn ingepungua zaidi ya kuondoa kuondoa chembe za shaka ktk jamii.

Kashfa siziungi mkono, walimchafua haswa lowasa bila ushahidi. Leo yeye kaumia kwa kuchafuliwa hadhi. Tuna safari ndefu ya kujifunza siasa kupitia Kwa lowasa.
 
Back
Top Bottom