CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya.

CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya.

Kikuba

Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
13
Reaction score
8
TAMKO LA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB) KUHUSU UDHAIFU WA SERIKALI KATIKA KUKOMESHA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.

Ndugu wanahabari, kwanza kabisa napenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wangu, ili niweze kuzungumza na watanzania kupitia kwenu kuhusu hatari kubwa inayolikumba taifa ya madawa ya kulevya.

Biashara haramu ya dawa za kulevya imekua kwa kasi sana hapa nchini miaka ya hivi karibuni licha ya kuwa na vyombo lukuki vya ulinzi na usalama na licha ya kuwa na Tume maalumu ya kudhibiti madawa ya kulevya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera Uratibu na Bunge Mhe. Wiliam Lukuvi tarehe 26 Juni, 2013 siku ya maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya huko Dodoma ni kwamba katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012 watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini. Aidha, watanzania wapatao 240 walikamatwa na madawa ya kulevya katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika ya kusini na hivyo kutia doa taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa. Kutokana na kukithiri kwa biashara hii haramu, Serikali kupitia maadhimisho hayo ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani ilitangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya kuwa ni janga la taifa.

Mtakumbuka pia kwamba hivi majuzi, muda mfupi baada ya Serikali kutangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya ni janga la taifa , walikamatwa wasichana wawili ambao ni watanzania huko Afrika ya kusini wakiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya randi milioni 42.6 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 6 za kitanzania.

Ndugu wanahabari, matukio yote haya yametokea ndani ya kipindi cha miaka sita tu ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne ambapo kuna viongozi wa juu Serikalini ambao waliwahi kusema kuwa wanawajua watu wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya lakini mpaka sasa hawajawataja wahusika na wala hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wahusika.

Ndugu wana habari, miongoni mwa viongozi wa serikali na taasisi nyingine waliosema kuwa wanawafahamu wafanya biashara ya madawa ya kulevya ni:-

Rais Jakaya Kikwete, ambaye alipiga hatua kubwa zaidi na kusema anawajua hata viongozi wa dini wanaofanya biashara hiyo. Licha ya maaskofu na viongozi wengine wa dini kumtaka Rais awataje wahusika hao wa madawa ya kulevya ili kuuweka ukweli wazi, Rais hajafanya hivyo mpaka sasa.

Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya: huyu alisema anayo majina ya vigogo (kwa maana ya viongozi) wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini hajaweka majina hayo hadharani na wala haijulikani kama wahusika hao wamechukuliwa hatua yoyote hadi sasa.

Mbunge wa Mwibara – Kange Lugola alisema katika bunge la bajeti 2013/2014 kuwa kama Rais na Kamishna wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya wanawajua "kwa majina" watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya na hawataki kuwataja watu hao wala kuwachulia hatu yamkini watu hao ni miongoni mwa mawaziri ndio maana kuna kigugumizi cha kuwataja na kuwachukulia hatua. Tangu Mhe. Kange Lugola alihusishe baraza la Mawaziri na kashfa hiyo ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya hakuna hatua yoyote ilivyochuliwa na Serikali kuthibitisha au kubatilisha kauli hiyo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi aliwahi kutoa taarifa ya wazi kuwa kuna kundi la matajiri wanaoshirikiana na viongozi wa Jeshi la Polisi waliokuwa wanapanga njama za kumwekea mtoto wake dawa za kulevya ili wambambikizie kesi ya dawa za kulevya na hivyo kuchafua heshima ya Bw. Mengi na familia yake. Ndugu mengi alisisitiza katika taarifa yake kwamba yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na mamlaka nyingine zinazohusika ili kubaini njama hizo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika lakini mpaka leo Ndugu Mengi hakuhojiwa ili kuthibitisha kauli yake jambo linaloashiria kwamba kuna ukweli katika kauli yake.

Baada ya matukio yote haya na baada ya Serikali kukaa kimya kuhusu matukio hayo, mimi kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ninatoa tamko kama ifuatavyo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete awataje na kuwachukulia hatua watu aliosema anawafahamu wanaojishughulisha na biashara ya dawa za kulevya la sivyo akubali kubeba shutuma kwamba Serikali yake ndio Mratibu Mkuu wa biashara ya dawa za kulevya ndio maana anashindwa kuchukua hatua.

Kamishana wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma juu ya hatua alizochukua dhidi ya wahusika wa biashara ya dawa za kulevya aloiosema anawafahamu la sivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimika kuwashawishi wananchi kuamini kwamba yamkini na yeye yumo katika mtandao wa wafanya biashara haramu ya dawa za kulevya ndio maana anasita kuwachukulia hatua wahusika hao ambao alishakiri kuwa anawafahamu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma kuwa ni tatizo gani linaloikabili mamlaka yake hadi kufanya viwanja vya ndege vya Tanzania kuwa ndio njia rahisi ya kuingiza na kusafirishia madawa ya kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki?

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi wawajibike kwa kutoa maelezo kwa umma kuwa ni kazi ipi wanayofanya ikiwa madawa ya kulevya yanaingizwa nchini na kusafirishwa nje ya nchi kwa kasi kubwa zaidi?

HITIMISHO: Ni vema kama taifa tukatambua madhara ya madawa ya kulevya kwa vijana wetu ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kupuuzia na kutochukua hatua kwa wahusika wa dawa za kulevya ni kuangamiza nguvu kazi ya taifa. Nguvu kazi ya taifa ikishaharibiwa na dawa za kulevya hatuna taifa tena. Hivyo Serikali ifahamu kwamba kuendelea kulifumbia macho jambo hili kwa manufaa ya mafisadi wachache ni kulihujumu taifa na huo ni usaliti dhidi ya kiapo ilichokula cha kulitumikia taifa na kusimamia usitawi wa wananchi wa Tanzania. Aidha, Serikali itambue pia kwamba kuendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote juu ya jambo hili kunatoa dalili kwamba yamkini ya yenyewe inahusika na biashara hiyo.


MUHIMU: IKIWA SERIKALI ITAENDELEA KUPUUZIA JAMBO HILI AMBALO LINALIANGAMIZA TAIFA, BASI KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI ITAENDESHA OPERESHENI NCHI NZIMA ILI WANANCHI WAPIGE KURA KWA WAHUSIKA WAKUU WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, NA BAADA YA ZOEZI HILO, TUTAANIKA HADHARANI (KWA KUWATAJA MAJINA) WAHUSIKA WA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.



Vincent Josephat Nyerere (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

NA WAZIRI KIVULI WA MABO YA NDANI YA NCHI

Imetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2013
 
Chadema inabidi wajue pia kuwa bangi nayo ni madawa ya kulevya.

Cc: Mbowe, Lema, Sugu...
 
Hivi CCM wanaamini kuwa unga unalipa kuliko madini?Nadhani dawa ni kuwalisha watoto wao wote, kwa hila ama kw akuwashawishi....nadhani watapata adabu.Ikibidi pia wao na wake zao.
 
kama chadema italivalia njuga jambo hili, sina shaka mwisho utakuwa mzuri. Lakini kama waziri kivuli ataishia kuongea na wana habari tu yumkini nae takakuwa miongoni mwao
 
"Nina list ya majina ya wauza unga wote nchini." Janga la Taifa
 
Inasikitisha.ila sio mbaya kwao.kwa sababu kwao mkwanja unaingia.RIP NGWEA
 
Wewe vincent, si kwenu bangi ni mboga au mmeacha siku hizi?
 
"Nina list ya majina ya wauza unga wote nchini." Janga la Taifa

Hiyo list bora uihifadhi kabatini daima. Ukiitoa tu basi consequences zake ni balaa kama unyama wa The Zetas na Los Pepes kule Tijuana na Acapulco
 
Kikwete aliwahi kujinasaibu kuwa anawafahamu kwa MAJINA wauza unga wakubwa..baada ya hapo aliziba mdomo hata swala lenyewe la madawa ya kulevya halizunngumzii tena why??? Nina shaka huenda hii biashara ikawa na mkono wa vigogo wa Ikulu!!
 
Chadema inabidi wajue pia kuwa bangi nayo ni madawa ya kulevya.

Cc: Mbowe, Lema, Sugu...
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Mbona wewe hili la madawa ya kulevya linaonekana halikukeri? yani kwenye serious issue unaleta mzaha au wewe nimhusika? anyway kwakuwa siku zinu zinahesabika endelea kufurahia tu ila ukae ukijua hata kama unamapembe kama faru yanamwisho wake.
 
Tusipokuwa makini na kuacha ushabiki kwenye mambo nyeti yanayolihusu taifa letu, itakuwa vigumu sana kupata majibu na njia sahihi za kutatua matatizo yanayoikumba nchi yetu. Rais wa nchi alitangaza mwenyewe kuwa anayo majina ya watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Tangu atangaze hivyo, hakuna hatua zozote zimechukuliwa na mamlaka husika. Mbaya zaidi badala ya ukubwa wa tatizo kupungua, leo tunashuhudia watu wakisafirisha kwa viroba kana kwamba wamebeba mchele ama unga wa mahindi tofauti na ilivyokuwa imezoeleka awali wahusika kusafirisha madawa hayo kwa kuyazamisha kwenye matumbo yao.

Watu wanapouliza kulikoni, wehu wengine wanakuja na kebehi na dharau nyingi kana kwamba ni jambo dogo na jepesi tu kwao. Tatizo ni kubwa, hao wanaoongelea bangi kuwa inalimwa wapi, au watu Fulani wanaitumia kama mboga, nafikiri hilo sio jambo la kujadili na mnachoonesha ni kutaka kuharibu mada husika tu.
 
Tatizo ni kuwa wafanyabiashara wengi wa madawa ya kulevya ni vigogo na rais ana majina yao ila hataki kuyataja. Ana maana gani? Au ndio yaleyale ukinitaja nitakutaja? Inasemekana madawa mengi sana huletwa na viongozi VIPs ambao hawakaguliwi airports.
 
suala la madawa siyo kama tunavofikiria na kuwa na hamu ya kutajana jamani hili suala linataka utayari wa wananchi kuchukua maamuzi mazito kama yaliyopendekezwa na mh mbunge la kukusanya majina ya wauzaji kutoka kwa wananchi lasivyo tutatajana tu na mwishowe amna kitakachoendelea. RIP AMINA,RIP MANGWEA.
 
ana majina yote ya wauza unga ,anachofanya yeye sio kuwakamata bali ni kuwaongezea mtaji na kuwalinda ili wasikamatwe .na ndio maana wengi wanakamatwa nje ya nchi badala ya nchini kwetu .huyu jamaa ni dhaifu sana hana sifa za kuongoza nchi
 
Tatizo la pro-ccm wa JF ni moja tu yaani upuuzi, hawa jamaa ni wapuuzi wa kiwango cha kutisha.Madawa ya Kulevya yanaangamiza nguvu kazi ya taifa na kuchafua taswira ya nchi kimataifa kitu ambacho kitaathiri uchumi pia.Hakuna mwekezaji atawekeza effeciently kwenye taifa lenye magenge ya wauzaji wa dawa za kulevya na mateja kila mtaa hivyo ni vema tukasimama pamoja kwenye hili kama alivyolisema Mb.Kange Lugola bila kujali itikadi. Leo ZeMarcopolo na FaizaFoxy mnaleta ukada kwenye suala hili ovu, are you rational?
 
Last edited by a moderator:
150 kg crystal Meth. Zilokamatwa Afrika kusini zenye thamani ya Tsh 7 billioni ni nyingi mno, nadhani madawa haya yanatengezwa nchini. The truth is Meth. can be easily proccessed at home using common chemicals and base material ephedrin ,the active ingredient in common cold tablets.
 
Hapo kwenye muhimu ndo moja ya mambo ambayo yananifanya nione kama vile upinzani nao hawapo serious na mambo yanayogusa wananchi moja kwa moja...eti kama itaendelea kupuuza?????!!!!!

Yaaani ni kama anajua kuwa wanapuuza ila kama wakiendelea ndo watachukua hatua!!!!!
Yaani unaita waandishi kutoa ultimatum bila time limit?????
Halafu si katoka bungeni huyu na alisoma bajeti kivuli,ndo angeweka hii ili iingie kwenye hansard..unasikia kelele za nyokaaa nyokaaa hutoki..akitoweka ndo unaanza angepigwa kichwani angekufa fastaaa!!!

Ile nguvu ya kuhamasisha maandamano na kuota weakness ya incumbents ingetumika na kwenye majanga kama haya Tanzania ingekuwa mahala salama sana kuishi na wala msingekuwa na haja ya kutafuta wanachama...tungemiminika mpaka mkose kadi za kutupa!!!!!!

Kwa wanachama na wafuasi wa vyama hapa kuna habari.,kwa mtu neutral kama mimi nimechoshwa na matamko yasiyo na tija ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida!!!!!!

It might be a good start though
 
Tatizo la pro-ccm wa JF ni moja tu yaani upuuzi, hawa jamaa ni wapuuzi wa kiwango cha kutisha.Madawa ya Kulevya yanaangamiza nguvu kazi ya taifa na kuchafua taswira ya nchi kimataifa kitu ambacho kitaathiri uchumi pia.Hakuna mwekezaji atawekeza effeciently kwenye taifa lenye magenge ya wauzaji wa dawa za kulevya na mateja kila mtaa hivyo ni vema tukasimama pamoja kwenye hili kama alivyolisema Mb.Kange Lugola bila kujali itikadi. Leo ZeMarcopolo na FaizaFoxy mnaleta ukada kwenye suala hili ovu, are you rational?

Kahiyo kuwakumbusha kuwa BANGI nayo ni madawa ya kulevya ni ukada?
 
Nchi hii inaangamizwa kwa mikono yetu wenyewe wenye nchi. Bado siku zote nitakuwa nazikumbuka makala za Mzee Mwanakijiji juu ya kutamalaki kwa nguvu za kifisadi ndani ya taifa. Na hili ndo mojawapo ya madhara yake, wanafahamika lakini hawakamatwi japo vyombo husika vya dola vipo na vinafanya kazi masaa yote. Inawezekana labda nao wakikamatwa nchi itatikisika kama wale wengine ambao mh. Pinda aliwahi kusema bungeni!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom