CHADEMA watimuana Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA watimuana Morogoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Mwema, Nov 7, 2011.

 1. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Chadema watimuana Kilombero
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 06 November 2011 20:09
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Venance George, Morogoro

  WANACHAMA wa Chadema Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro umewatimua madarakani viongozi wa chama hicho wilaya kutokana na kuwapo kwa mgogoro wa makundi uliodumu zaidi ya miaka mitano sasa.

  Akizungumza kwa jia ya simu, katibu wa chama hicho Mkoa wa Morogoro, Abeli Luanda alisema hatua hiyo imefikiwa na wanachama wa chama hicho baada viongozi hao kuwagawa wanachama.

  Inadaiwa kati ya makundi hayo kundi la kwanza lilikuwa likimuunga mkono mbunge wa sasa wa viti maalumu Regia Mtema na kundi lingine lilikuwa likimuunga mkoano mbunge wa viti maalumu mkoa kupitia Chadema, Susan Kiwanga.Wabunge hao walipohojiwa na uongozi wa taifa endapo wao ni chanzo cha kuwapo kwa makundi hayo wabunge hao walisema wao siyo chanzo cha tatizo hilo.

  Kwa mujibu wa barua ya chama hicho ambayo imetiwa saini na Katibu wa Mkoa wa Morogoro, Abeli Luanda, inaeleza kuwa chama hicho kwa hivi sasa hakiwatambui viongozi hao.

  Viongozi walioenguliwa madarakani ni pamoja na mwenyekiti wa wilaya Salimu Ngozi, katibu Mashaka Manjoti, katibu mwenezi John Makumbo, Mtunza hazina Beno Chelele, Mwenyekiti vijana, Godfrey Lwena, Katibu vijana Magnus Kamchape, Mwenyekiti wa wanawake, Mwajuma Lihoniko, Katibu wanawake Mwanaidi Mpeta na Mwenyekiti wazee, Gaudence Ligombe.

  Wengine waliotimuliwa ni wajumbe wa kamati utendaji ambaye ni Suzan Kiwanga, Amina
  Mwitimba, Said Mnasi, Bertha Mchopa, Janeth Lusoli na Said Kwanja.

  Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Luanda alisema amefikia uamuzi wa kuwaruhusu wanachama wa chama hicho kufikia uamuzi huo kutokana na uongozi wa chama hicho taifa kuarifiwa kwa muda mrefu pasipokutoa taarifa na kwamba hatua hiyo ni ya kikatiba.Alisema hivi sasa viongozi hao watakuwa wanachama wa Chadema tu na kwamba wataendelea na nyadhifa zao katika ngazi ya kata.

  Luanda alisema anaheshimu uamuzi wa ya mkutano mkuu wa Mlimba na maelezo ya waraka namba 1 kutoka ofisi ya katibu mkuu Taifa ambao uliandikwa Agosti 1, mwaka huu ambao ulitoa baraka ya kuundwa kwa kamati tendaji ya muda.

  Waliochaguliwa katika kamati ya muda ni Mwenyekiti Wendelin Ngonji, Kaimu Katibu Mkuu, Moses Kisenime, Katibu mwenezi Anthony Kamonalelo na wajumbe ni pamoja na Baraka Shayo, Koba
  Ng'onji, Nassoro Kuandika, Hadija Salum na Devota Matimbwi.

  Mwenyekiti aliyesimamishwa Salimu Ngozi alisema hatambui mabadiliko hayo kwa kuwa alichaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu na siyo kung'olewa na kikundi kidogo cha wanachama walioitisha mkutano huko Mlimba.

  Ngozi alisema hata mkutano uliofanyika Mlimba haukuwa halali kwani uliitishwa na baadhi ya viongozi wa kata kwa kuwaalika marafiki na siyo wajumbe halali wa mkutano mkuu.

  CHANZO GAZETI LA MWANANCHI 7 NOV 2011
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Makundi yaliyokuwa yakikitafuna Chama caha Demokrasia na maendeleo katika wilaya ya KILOMBERO yamefasababisha Chama hicho kusambaratika

  baada ya Wananchama kujaribu kuusimamisha uongozi uliokuwepo huku wakidhania kufanya hivyo ingekuwa ni suluhu ya kumaliza mpasuko huo.

  Makundi hayo ni yale ambayo mojawapo lilikuwa kimuunga mkono mbunge wa sasa wa viti maalum, REGIA MTEMA na lile lilokuwa likimuunga mkono mbunge wa viti maalum mkoa kupitia Chadema, SUZAN KIWANGA


  Kumbeeeeeeeee, du mimi nilifikiri ni Ndani ya CCM tu yaani SITTA na LOWASSA kumbe hata ndani ya CHADEMA napo kuna makundi?. Oh yes I remember, ZITTO NA MBOWE nani awe mwenyekiti wa Chama ilikuwa ni balaa kama siyo mzee mtei.

  Nini hatma ya CDM pamoja na uchanga wao huo?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  noo huyu regia ana kiherehere sana...ngoja 2015 ifike najua atanipiga fitna sana nitakapo taka kugombea jimbo la kilombero lakini mi ninaye....
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Wewe unadhani nini kifanyike?maana sio unapost thread halafu hutupi idea zako,maana muda wa kulaumu bila kutoa njia mbadala naona umepitwa na wakati,na hii ya kudhani viongozi fulani hawawezi kupishana kifikra nalo ni tatizo kubwa kwa elimu yetu ya siasa na uraia.
  Mkuu kwanza tupe mawazo yako nini kifanyike,usije tu ukawa bingwa wa kuona kosa au udhaifu halafu huna njia ya kushauri .
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Regia Mtema ndiyo nani? Yule aliyeingia mjengoni kupitia viti vya wasiojiweza?
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Regia huwa ni mtu wakuropoka na asiye na uelewa nashindwa kuelewa kwa nn viongozi wa cdm mpaka leo hii wamemvumilia na kuna mkubwa ndani ya chama ***mla
   
 7. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wakuu naona heshima inapotea..tumejifunzia wapi haya matusi makubwa namna hiyo..let's respect each other..toeni hoja na siyo matusi..!
   
 8. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mpiga picha maarufu issa michuzi vp we ni kabila gani? Vp mbona ujaipeleka hii habari kule kwenye blog yako?
   
 9. S

  Shembago JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi tupo Morogoro na niwashika dau wakubwa wa Chadema na wengine tulijitosa 2010 lakini magamba wakachakachua.Regia Mtema hamumuelewi kabisa,Ni kijana mahiri aliyekwenda shule tena siyo shule ya Historia au Jiographia ni Shule ya "Great Thinker" Kumbuka Regia alishinda Ubunge Kilombero Magamba wakamchakachua ni kati ya wadada waliogombea 2010 Ubunge na kupata Kura nyingi Kuzidi hata alizopata Halima mdee mbunge wa kawe!! kwahiyo sio kilaza kama wengine wanavyopayuka huku JF.

  Chadema hatutaki viongozi wanogawa wanachama kwa masilahi yao,hivyo kuwaondoa Viongozi hao ni sahihi kabisa.

  Namtakia Mheshima Regia afya njema ili 2015 achukue kiti chake alichopokwa na chekibob yulle wa Magamba!

  Kwa taarifa yenu hata hapa Moro mjini Abood Tumbo joto!!
   
Loading...