CHADEMA wataka wabunge 2015 kufanya mtihani

CHADEMA wataka wabunge 2015 kufanya mtihani

Jenifa

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
605
Reaction score
305
Paper noma, tutasikia waheshimiwa wakiandika mambo ya zombi

Nafasi zao kutangazwa magazetini
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia Chadema au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema Chadema haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.

“Sasa kwa kuwa Serikali imetoa majibu yake bungeni kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda tunasubiria mwenyekiti wetu Mbowe awasilishe ripoti kwenye kamati kuu ndipo tutakapoamua.

“Pia suala la mwakilishi wetu katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu litazungumzwa kwenye kamati kuu, chama kikijitoa hata kama akibaki hayo yatakuwa ni mawazo yake,”alisema.

Hata hivyo alisema kuwa amani ya imevurugwa na viongozi wa Serikili na vyama vya siasa kutokana na kutanguliza ushabiki wa siasa badala ya uzalendo na misingi ya taifa.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba Magharibi, Ntundu Emmanuel amehamia Chadema akidai kuchoshwa na matusi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
 
kuwa Mbunge Ufanye MTIHANI????? au nimesikia vibaya? Hivi huo mTihani utaandaliwa na nani? Chama au wananchi? sijui utakuwa ni wa nini CIVICS au manake matakwa ya wanachi ni kama ukubwa wa DUNIA lol!! anyway kuishi kwingi kuona mengi huenda tukapata kitu kipya kuingiza kwenye GUINESS book kama ilivyo kwa aina ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hadi leo wazungu hawajui inakuwaje umedumu kiasi hiki!!. na hisia kuwa huu utakuwa wizi wa demokrasia, tafakari....
 
Mkuu ni dhahiri hii approach itazuia kuwa na viongozi vilaza mithili ya akina Lusinde Matusi, Mwigulu, Kigwangala na Misukule wengi walioko CCM.
 
Mkuu ni dhahiri hii approach itazuia kuwa na viongozi vilaza mithili ya akina Lusinde Matusi, Mwigulu, Kigwangala na Misukule wengi walioko CCM.

...Sasa msahishaji mkuu ndio atakuwa Mwenyekiti Mbowe (Division O), just thinking aroud...
 
tumekuelewa mheshimiwa Dr. Slaa. Naona nchi yetu inaanza kubadilika kutoka katika utamaduni wa kizamani kuelekea katika utamaduni wa kisiasa zenye muelekeo wa DOT.COM. Naomba utaratibu huu ufanyike pia katika ngazi za viongozi wa chama pia. Kwa maana ya kumpata mwenyekiti, katibu, na wakurugenzi wa taifa wa chama na usiishie kwa wabunge peke yao.
 
Labda uwe ni wakupambunua mambo, tofauti na hivyo sidhani kama uitakuwa poa kwani kuna watu wanauwezo wa kupambanua mambo lakini ukiwarudisha darasani hakuna kitu
 
Ni hoja ya msingi maana kazi ya chama ni kutafuta viongozi bora waliofundwa, wenye uelewa na masuala ya siasa, wenye uwezo wa kufikiri na wenye maadili ya uongozi. Binafsi huo ni mwanzo mzuri!
 
hiyo mitihani iwekwe online pia.km aptitude zingine sio mahard copy tu.
 
Sijajua kama hii imekaa vizuri, hata ivyo ifanyiwe utafiti wa kina na iboreshwe zaidi. Tupo pamoja!
 
Sisi vilaza itakuwaje, mbona mtatutenga? CDM fikirieni upya hii kitu kitaumiza wengi.
 
iwafikie Afande Sele na mrisho Mpoto watakaogombea 2015 lakini mpaka sasa hawana chama
 
Huwa mtiahani hautaliki? make huu wa ndalichako na ulinzi wote unavuja.
 
...Sasa msahishaji mkuu ndio atakuwa Mwenyekiti Mbowe (Division O), just thinking aroud...

Hayo ni mawazo yako mkuu, kwani hadi sasa Dr. Slaa hajaelezea mfumo mzima wa huo mtihani, utakuweje na uta sahihishwa vipi. Kwa mtizamo wangu binafsi sidhani kama utakuwa ni mtihani wa kukaa darasani bali zitatumika techniques za kupima understanding capacity na IQ ya mgombea na lengo kuu hapa ni kuondoa vilaza bungeni.
 
Hizi ni mbinu za kuwapiga chini Lema na Sugu. Mbowe atajipasisha hata kama akichemsha.
 
Huwa mtiahani hautaliki? make huu wa ndalichako na ulinzi wote unavuja.

Is this constitutional? Katiba ya CDM inazungumzia hii paper? Angalieni, watu watapiga paper wakifeli wanawahi kotini! Kumbuka Grade A students husomea Udaktari, Uhandisi, Sheria n.k., Grade B hujiajiri wenyewe na kufanya biashara zao, Grade C hujiunga na vyama vya siasa na kuwatala Grade A na B. Hakuna shaka paper ikisetiwa vizuri, wengi 'watazungusha'. Mjiandae pia kupambana na udanganyifu mf. Madesa, mig, mimba n.k.
 
tumekuelewa mheshimiwa Dr. Slaa. Naona nchi yetu inaanza kubadilika kutoka katika utamaduni wa kizamani kuelekea katika utamaduni wa kisiasa zenye muelekeo wa DOT.COM. Naomba utaratibu huu ufanyike pia katika ngazi za viongozi wa chama pia. Kwa maana ya kumpata mwenyekiti, katibu, na wakurugenzi wa taifa wa chama na usiishie kwa wabunge peke yao.

naiunga mkono hoja YAKO mkuu.
 
Makamanda naona sasa wengi watakimbia kugombea ubunge maana paper linatisha aisee

Napendekeza paper lisahishwe na Dr.Ndalichako itakuwa poa zaidi!
 
Back
Top Bottom