Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao
Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao.
Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili.
Hivi ni kwa nini hawa askari wanapenda sana kuleta taharuki ktk matukio kama haya halafu wanawasingizia chadema kwamba ndio wanafanya fujo... Yaani mpenzi wa Yanga akakae kwenye benchi la mashabiki wa simba.. lazima watamgawana tu.
Chadema waache mambo ya kizamani. Hata ikiwa ni polisi ndio iweje? Kwani wakitaka kukushikeni wote mliopo hapo watashindwa??!!!
Acheni vurugu zisizo na msingi.
Kuweni waungwana.