Chadema wasusia bajeti, ccm na cuf waipitisha

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana walisusia Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kilichokuwa mahususi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya maendeleo ya wilaya hiyo kwa mwaka 2011/2012.

Madiwani wa kata sita za Kasamwa, Katoro, Kagu, Kamhanga na Kalangalala walisusia kikao hicho na kulazimika kuondoka wakati kikao kikiendelea na kuwaacha madiwani wa vyama vya CCM na CUF wakiendelea na kupitisha bajeti hiyo.

Wakitoa sababu kubwa ya kususia kupitisha bajeti hiyo, baadhi ya madiwani hao walieleza kuwa kanuni mahsusi zinazohusika na upitishaji wa bajeti hiyo zimekiukwa, ambapo Diwani wa Kata ya Kalangalala, Peter Donald alisema kanuni za halmashauri zinataka madiwani kupatiwa makabrasha ya bajeti siku saba kabla ya kikao lakini wao wamepatiwa makabrasha hayo siku moja kabla ya kikao.

“Kanuni zinataka sisi madiwani kupata makabrasha siku saba kabla ya kikao ili kutuwezesha kuyapitia, lakini makabrasha haya sisi tumepewa jana…hivi kwa mahesabu ya haraka haraka hamuoni kwanza kwamba kanuni zimekiukwa, lakini pili hii ni mojawapo ya njia ya kutaka kutuburuza katika upitishaji wa bajeti hii…,’’ alisema diwani huyo.

Hoja hiyo iliungwa mkono na madiwani wengine wa chama hicho ambapo ilimlazimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Benson Tatala kueleza kwamba pamoja na kanuni kutaka hivyo, lakini tayari madiwani hao walikwishapitisha bajeti hiyo kwenye vikao vyao vya kamati.

“Waheshimiwa wajumbe bajeti hii tunayokuja kuijadili na kuipitisha hapa leo hii ni sisi hawa hawa ambao tumekaa na kuitengeneza na kuipitisha kwenye kamati zetu sasa hili la siku saba kabla ya kikao ni lingine lakini tunaamini kwamba kila kitu kiko sawa naomba tuendelee na kikao…’’.

Baada ya maelezo hayo madiwani wote walianza kuchangia na kuibuka pande mbili ambapo upande mmoja ulikuwa ukitaka kikao kisifanyike na mwingine ukitaka kifanyike na hivyo kuzusha mabishano makali hatua iliyosababisha hoja ya kura kupigwa ili kupata washindi ikaamriwa ambapo baada ya kura kupigwa madiwani waliotaka kikao kufanyika walishinda.

Ushindi huo uliwafanya madiwani wa Chadema kutoka ndani ya ukumbi huo na kuwaacha wenzao wa vyama vingine vya CCM na CUF wakiendelea na kikao ambapo baadaye walipitisha bajeti hiyo kwa kishindo.

Katibu Msaidizi wa Chadema wilayani Geita, Amos Nyanda alisema kwamba kwa kuwa Wabunge wao wamekuwa wakitumia staili ya kutoka ndani ya Bunge katika kufikisha ujumbe wao na hasa pale ambapo madai yao yanaonekana kupuuzwa, nao kama madiwani wameamua kutumia staili hiyo ili kufikisha ujumbe wao kwa serikali pamoja na watendaji wa serikali.
“Ndio tumetoka ndani ya ukumbi kupinga kanuni kukiukwa….hatuwezi kuendelea kupitisha bajeti yenye maslahi ya viongozi na si wananchi, lakini hatuishii hapa tu tunakwenda mbali zaidi na baada ya hapa tutahakikisha kwamba tunakwenda kwa wananchi na kuwaambia ukweli juu ya bajeti hiyo, ni lazima tuwachongee…’’
alisema Katibu huyo.

Hata hivyo alipoulizwa kwamba ni kwanini madiwani wao wamegomea kupitisha bajeti hiyo sababu ikiwa ni kucheleweshewa makabrasha wakati wao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati zilizoketi na kuandaa bajeti hiyo na kupitisha kwenye kamati zao, alisema hawezi kujibu swali hilo isipokuwa ni madiwani wenyewe.

Kwa upande wake Katibu wa CUF wilayani Geita, Severine Malugu aliwaponda madiwani wa Chadema kwa kukimbia kikao hicho cha bajeti kwa madai kuwa huo bado ni uchanga wa kisiasa ndio umewafanya kususia kikao, huku akibainisha kwamba mwanasiasa aliyekomaa siku zote anapigana hadi dakika za mwisho na hata akishindwa basi anakubali matokeo na kujipanga upya.

Source: Gazeti la Habari Leo, Mei 1, 2011.

Hawa CDM wanachefua style ya kususia vikao muhimu yapaswa waachane nayo, wao wanachangamkia posho tu, wala hawaangalii maslahi ya wananchi!
 
"Hawa CDM wanachefua style ya kususia vikao muhimu yapaswa waachane nayo, wao wanachangamkia posho tu, wala hawaangalii maslahi ya wananchi!"

mi nimeangalia argument yako haiendani na deduction
argument: wao wanachangamkia posho tu, hawaangalii maslahi ya wananchi
deduction: style ya kususia vikao muhimu

Sasa ukiangalia hapo anaesusia vikao na anaenda vikao kama muhuli yupi anapata posho zaidi? Najua ukiingia nusu unapata kidogo lakini sio kususisa. Vilevile inafahamika wazi maana ya KANUNI.. Walioitunga sio vichaa.. Kwani kila diwani ni member wa kila kamati? acheni kuwehuka kuweni wakweli. Nyie mnataka waingie wapitishe halafu 2015 wananchi wawatose kwa kuwa walikuwa mihuli ya Meya na mwenyekiti?

Pumbaaaafu
 
Kisa chenyewe Soko:

Wajanja wanataka lijengwe kwa 400Milioni kuweka mabanda uchwara.

Nendeni Geita mkajionee, Ule ukuta unaozunguka Halmashauri umegharimu 700Mil

Huu ni wendawazimu.
 
Huko kinondoni zimetengwa mil 44 kuandaa taarifa ya utekelezaji ya ilani ya ccm moto sio wa kitoto uliowaka bado kidogo wazichape
 
Hata hivyo alipoulizwa kwamba ni kwanini madiwani wao wamegomea kupitisha bajeti hiyo sababu ikiwa ni kucheleweshewa makabrasha wakati wao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati zilizoketi na kuandaa bajeti hiyo na kupitisha kwenye kamati zao, alisema hawezi kujibu swali hilo isipokuwa ni madiwani wenyewe.

hebu tuyafikirie haya maneno aliyoyamumunya. kwa mwenye akili anaona upeo wa hawa chadema. wanataka huruma ya wananchi.
kama kuna kasoro sitayari wanazijua au wameshiriki kuzianzisha, kwa hiyo suala lilikuwa kuziainisha kama kweli wako kwa maslahi ya wananchi. hawa jamaa kweli ni mabogus.
 
Back
Top Bottom