Chadema washambulia waandishi

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wakuu JF
Wafuasi wa Chadema jana walifunga Barabara ya Moshi-Arusha eneo la Maji ya Chai na kulishambulia gari walilokuwa limebeba waandishi wa habari.

Waliokuwa katika msafara wa CCM ulikuwa ukipita barabara hiyo ukitokea kata ya Leguruki.

Muda mfupi baadaye polisi walifika na katika eneo hilo na kuwatawanya wafuasi ho.

Katika hatua nyingine gari la wafuasi wa Chadema lilivamia mkutano wa CCM katika kata ya Leguruki na kutimua vumbi uwanjani hapo kwa muda kabla ya kuondoka na kutokomea kusikojulikana.

SOURCE MWANANCHI MACH 19.2012.
 
Kuna mtu amekwambia hapa ni Polish Post mpk utuletee ripoti ya matukio ya uhalifu?

Green Guards walikuwa wapi, au hujui kama CCM ina wanamgambo wa kigaidi?
 
Tatizo huwa mnakurupuka...hii kitu ipo hapa JF tangu jana mida ya saa tatu usiku...chanzo ni green guard wa ccm kuwateka madiwani wa cdm kutoka Moshi na kuwalazimu vijana wa cdm kwenda kuwaokoa madiwani wao na walifanikiwa...na gari moja la green guard lilifukuzwa na redbregade na kulazimika kukimbilia kituo cha polisi...waandishi wa habari walijikuta ni wahanga katika mazingira hayo...acha ushabiki usio na maana.
 
Hata mwananchi imeanza uongo???
Jana chadema ilikuwa kwa pole na maji ya chai.
Legutuki wameendaje? Wanaujua umbali kweli kati ya leguruki na maji ya chai, leganga na kwa pole??
Au hizi habari unaziandikia ofisini kwa kuletewa umbea bila wewe mwenyewe kuwepo tukioni??

Polisi gani waloenda kutatua?
Mwandishi gani kaletewa fujo?

Mbona haisemwi ya Greenguards kuzuia msafara wa chadema? Au mnaona aibu mana mlikimbizwa???

Njooni Arumeru mjionee mseme yaliyo kweli
 
Kuna mtu amekwambia hapa ni Polish Post mpk utuletee ripoti ya matukio ya uhalifu?

Green Guards walikuwa wapi, au hujui kama CCM ina wanamgambo wa kigaidi?
My friend, with all due respect; umeandika utumbo ambao sikuwahi kutegemea kutoka kwako

i usually read your posts na kuona a lot of sense, sijui nini kimekukuta hadi umejibu hivi.. hata iweje, hatuwezi kusherehekea uovu wa namna yoyote ile. iwapo itatokea chadema kushika dola (iwapo), je tutategemea mamngapi ya namna hii???

Tukio kama kweli limetokea basi ni la kulaaniwa, na kauli yako ni ya kujidharaulisha sana, nasikitika hata aliyekupa thanks/like kajidhalilisha
 
Hili mbona liko wazi, mamluki wa Magamba wameandaliwa kufanya hivyo ili kuigombanisha CHADEMA na wandishi wa habari! Wana wa Arumeru kuweni makini na njama hizi chafu za magamba.
 
Tatizo huwa mnakurupuka...hii kitu ipo hapa JF tangu jana mida ya saa tatu usiku...chanzo ni green guard wa ccm kuwateka madiwani wa cdm kutoka Moshi na kuwalazimu vijana wa cdm kwenda kuwaokoa madiwani wao na walifanikiwa...na gari moja la green guard lilifukuzwa na redbregade na kulazimika kukimbilia kituo cha polisi...waandishi wa habari walijikuta ni wahanga katika mazingira hayo...acha ushabiki usio na maana.

SOURCE; MWANANCHI gazeti pendwa.
 
Wakuu JF
Wafuasi wa Chadema jana walifunga Barabara ya Moshi-Arusha eneo la Maji ya Chai na kulishambulia gari walilokuwa limebeba waandishi wa habari.

Waliokuwa katika msafara wa CCM ulikuwa ukipita barabara hiyo ukitokea kata ya Leguruki.

Muda mfupi baadaye polisi walifika na katika eneo hilo na kuwatawanya wafuasi ho.

Katika hatua nyingine gari la wafuasi wa Chadema lilivamia mkutano wa CCM katika kata ya Leguruki na kutimua vumbi uwanjani hapo kwa muda kabla ya kuondoka na kutokomea kusikojulikana.

SOURCE MWANANCHI MACH 19.2012.

Ah kawaida yao
 
Hivi vyama vya siasa sasa vimekuwa kero,
Kila chama kinawahuni.

Watoto kwa wazee ipo kazi.
 
ndo shida ya majina bandia kwani haka kamada ni kati ya viongozi wa chama chenye ukame wa madaraka na sie tumo kuisoma hasa we wakufagiria kufanyiwa fujo wanahabari,kuvamia mikutano ya wengine,kubishie gazeti,kusifia cdm,kutoheshimu mawazo ya wengine nk. Sorry kwani hauwezi change go on.
 
Back
Top Bottom