CHADEMA wapotozea ahadi ya Kuuza Gari!

CHADEMA wapotozea ahadi ya Kuuza Gari!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameipotezea ahadi ya kuuza gari la kisasa lililokuwa likitumiwa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi (CCM) waliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakati wa kampeni hizo, madiwani hao pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa walisema wataliuza gari hilo la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser Prado ili fedha zitakazopatikana zitumike kununua gari la kubeba wagonjwa kwa ajili ya hospitali ya manispaa hiyo.

Hospitali hiyo inayotoa huduma wakati ujenzi wake ukiendelea imejengwa ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Katika kampeni hizo, wagombea hao wa Chadema waliwalaumu waliokuwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo 2010-2015 ambao kwa asilimia 99 walichaguliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupitisha uamuzi waliouita wa kipuuzi wa kununua gari hilo huku hospitali hiyo ikiwa haina gari la kubeba wagonjwa.

Katika mikutano yao mbalimbali ya kampeni, Chadema waliwaomba wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini wamchague mgombea wao ubunge na wagombea wake ili wakafanye maamuzi mengi yenye maslahi mapana kwa wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuuza gari hilo ili fedha zake zikanunue gari la kubeba wagonjwa.

Ahadi hiyo na nyingine nyingi za chama hicho zilipokelewa na wapiga kura wa mjini Iringa kwa kumchagua kwa awamu nyingine ya miaka mitano Mchungaji Msigwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na kuwachagua madiwani 14 kati ya 18 wa jimbo hilo, kuunda halmashauri ya manispaa hiyo.

Wakizungumza na wanahabari hivi karibuni, Meya wa Manispaa hiyo, Alex Kimbe na Naibu wake Joseph Lyata walisema mpango wa kuuza gari hilo haupo tena kwa sababu taratibu za kupata gari la wagonjwa zinaendelea kufanywa kwa kasi kubwa.

Ni kweli kulikuwa na ahadi ya kuuza gari hili ili fedha zake zitumike kununua gari la wagonjwa, mpango huo haupo tena kwa sababu kuna mipango mingine ya kupata fedha zitakazotumika kununua gari rasmi la wagonjwa,? alisema Naibu Meya Lyata.

Lyata alisema kwa kuzingatia mpango huo, gari hilo litaendelea kutumika kwa matumizi ya Meya, Naibu wake na kwa shughuli nyingine za halmashauri pale inapolazimu.

Alisema halmashauri yao itahakikisha inavipitia vyanzo vya mapato vya halmashauri hiyo, zikiwemo kodi mbalimbali, na makusanyo yake yatatumiwa kununua gari la kubeba wagonjwa sambamba na kuongeza gari lingine la kubeba taka ili kuufanya mji wa Iringa uendelee na sifa yake ya usafi.
 
mbona maguful alikataa kupanda ndege lakin juz chopa mpya imeletwa hapa kaz tuuu
 
siasa za chooni hizi.., yani wananchi wanageuzwa maf*la mchana kweupe.
 
hahahahaaa shida za wananchi amezijua sas anaweza kuruka duh
 
Hata Mwenyekiti wao Freeman Mbowe alilikataa Gari la KUB lakini mwisho wa siku akalitumia na kuna wakati alienda nalo mpaka Kenya
Lizabon una kumbukumbu! ! gari lilienda Mombasa likaibukia Nairobi askari walilikamata walikuwa hawaelewi nyendo zake. kumbe lilikuwa na mikakati na yule mkenya Bashir Awale ambaye alikuwa mkurugenzi wa Stanbic ban ambaye amehusika na ukwapuaji wa biolioni 12 na kampuni ya Kitilya. Bashir Awale baadae alijifanya mmoja wa wataalam wa IT wakati wa uchaguzi wakim support Lowasa. nchi hii. mpaka leo sijaelewa Mungu wangu mafisadi wangeipeleka wapi nchi hii kama wangeshinda uchaguzi
 
CHADEMA ilishakufa siku nyingi.

siku hizi imekuwa pango la mafisadi ni kimbilio la mafisadi.

wangepata urais muda huu akina Rostam,Karamagi,Mbowe,Mengi,Lowasa na Kingunge wangekuwa washagawana tenda zote za serikali na vitalu vya gesi.

tunashukuru hili genge la ufisadi kushindwa.
 
Lizabon una kumbukumbu! ! gari lilienda Mombasa likaibukia Nairobi askari walilikamata walikuwa hawaelewi nyendo zake. kumbe lilikuwa na mikakati na yule mkenya Bashir Awale ambaye alikuwa mkurugenzi wa Stanbic ban ambaye amehusika na ukwapuaji wa biolioni 12 na kampuni ya Kitilya. Bashir Awale baadae alijifanya mmoja wa wataalam wa IT wakati wa uchaguzi wakim support Lowasa. nchi hii. mpaka leo sijaelewa Mungu wangu mafisadi wangeipeleka wapi nchi hii kama wangeshinda uchaguzi

Taasisi za usalama ziwe makini na wageni.
Hata hivyo, uchunguzi makini unamfanya mtu mwenye akili ya kawaida kutilia shaka uhusiano wa kufukuzwa nchini na kashfa ya ufisadi kupitia Stanbic. Alifukuzwa ili kupoteza ushahidi?
 
lakini kufukuzwa peke yake bado hujapoteza ushahidi. kama ingekuwa lengo ni hilo basi labda na kesi yenyewe isingeibuliwa. halafu cha kushangaza zaidi wote hawa walikuwa team Lowasa. Bashir, Kitilya na wale wengi wakubwa wakubwa ambao wamesimamishwa kule TRA na Bandari. ni hatari iliyokuwa imetuzunguka
 
kwani gari za wagonjwa zikoje! ni hizihizi tu tofauti ni vifaa vilivyoko ndani ya gari, hilohilo liondolewe viti na kufungwa king'ora kitanda na vifaa vya kuhudumia mgonjwa tayari linakuwa la wagonjwa. Huyo meya gari la kwenda wapi? lipo gari la idara ya utawala siatumie hilo.
 
Chadema kwa miaka 5 Iringa imefanya kazi kubwa sanaaa....

Tenaa Mch Peter Msigwa kajitoa yeye mwenyewe kuanzia Barabara,

Hosptal ya Rufaa kaibolesha. Ni tofauti ya ile ya mwaka 2010 kurudi nyuma.

Usafi kuna Kuna magari ya kubeba taka kila kona tenaa ya kisasa.

Na menginee mengii sanaaa...

Hilo gari sisi wana Iringa tumeridhia Meya wetu alitumiee..

Msigwaa tenaaaa ndani ya iringa na madiwani 14.
 
acha uongo gari la taka ni moja tu, labda mengine yanasomba mchanga.
 
Jamani chadema ni waongo sana, kuna mzee mmoja wa chadema alisema atakwenda kuchunga ng'ombe lakini hadi leo anavinjari tu mijini.
 
Jamani chadema ni waongo sana, kuna mzee mmoja wa chadema alisema atakwenda kuchunga ng'ombe lakini hadi leo anavinjari tu mijini.

Vibaka ndani ya ccm mwaka huu lazima mtakufa njaa
 
kwani gari za wagonjwa zikoje! ni hizihizi tu tofauti ni vifaa vilivyoko ndani ya gari, hilohilo liondolewe viti na kufungwa king'ora kitanda na vifaa vya kuhudumia mgonjwa tayari linakuwa la wagonjwa. Huyo meya gari la kwenda wapi? lipo gari la idara ya utawala siatumie hilo.

Naona mapovu yanakutoka wachana na wana iringa wamejitambua kwa kuyakataa magamba
 
Back
Top Bottom