Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,390
Wadau, amani iwe kwenu.
Taarifa rasmi ni kwamba, Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) kimeshapoteza mvuto huko ng'ambo na kwamba wanachama wengi waliokuwa wanawaunga mkono wameacha kufanya hivyo na wanafanya yao kwa sasa. Inaelezwa kuwa chanzo cha hali hiyo ni baada ya kuridhika na mwenendo wa serikali ya Rais Magufuli ambaye kwa hakika anafanya kile ambacho walikuwa wanataraji. Tawi la London ambalo lilifunguliwa mwaka 2012, kwa miezi kadhaa sasa limeshindwa kufanya vikao vya ndani na inaelezwa kuwa viongozi wake hawana mawasiliano ya kiuongozi kwa takriban miezi minne sasa.
Tawi la DMV mpaka sasa limebaki na viongozi tu. Mapema mwezi Mei, waliitisha kikao cha wanachama wote lakini kimeshindwa kufanyika kutokana na kukosa akidi. Wanachama wao kwa sasa inadaiwa kuwa hawapo tayari tena kushiriki harakati za kisiasa za chama hicho na kwamba wanafanya kile kilichowapeleka nje ya nchi. Kwamba wana matumaini makubwa na serikali ya Magufuli kwa vile imeonesha mwanzo mzuri. Mwenyekiti wa tawi hilo, Kalley Pandukizi yupo mbioni kutangaza kuachia nafasi hiyo kwa madai kuwa ana majukumu mengi yanamkabili.
Ule mtandao wao wa kipropaganda maarufu kama CHADEMA DIASPORA, www.chademadiaspora.blogspot.com mpaka sasa hauna taarifa mpya. Taarifa ya mwisho ilichapwa kwenye mtandao huo tarehe 5 Novemba 2015 ambapo Liberatus Mwang'ombe, mtu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa Diaspora aliandika kuwashukuru wana Mbarali kwa kumpa ushirikiano wakati wa uchaguzi Mkuu licha ya kushindwa nafasi ya ubunge.
Wadau, binafsi nilidhani kuwa kupoteza mvuto CHADEMA ni hapa nyumbani tu kumbe hata huko ng'ambo! Lazima tuheshimiane tu.