CHADEMA: Wapi walipofanikiwa na wapi waliposhindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Wapi walipofanikiwa na wapi waliposhindwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PapoKwaPapo, Jan 13, 2012.

 1. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wasalamu wanajamvi?

  Nianze na kusema kwamaba nawapongeza sana uongozi wa juu wa Chadema mpaka hapa walipo fika kwa mafanikio makubwa ya kisiasa zaidi ya chama chochote cha siasa kilichowahi kutokea hapa kwetu Tanzania.

  Pamoja na kuwa na mafanikio hayo haimaanishai kwamaba hakuna wanapokosea, kupo tena kwingi tu. Kwamfano wamefanikiwa sana kujiwekeza katika vyuo vikuu na mashule kwani kwasasa ukiwana unadai haki ukiwa shuleni jibu la kwanza unaloambiwa wewe ni Chadema. kwa hilo nawasifu sana kwa kuamsha ari ya wanafunzi.


  Kwa mimi binafsi ningepesa sana kuona Chadema kwasasa inachukua hatua na kuanza kujiwekeza kwenye makundi mengine ya kijamii kwa mfano akina mama, sijui baraza la wanawake Chadema linafanaya nini? Sijui kwanini viongozi wa juu hawataki kuchukua hatua ya kulijenga baraza hili na hatimaye chama kwa ujumla wake, wafanya kazi waserikali vile vile.

  Serikali kivuli ya Chadema yaani serikali ya upinzani haifanyi kazi yake ipasavyo hata kidogo, kuweza kusema kwamaba hiki ni chama mbadala, bado siwezi sema hivyo sijaona hata waziri kivuli mmoja ambaye ni active memba kwenye wizara yake.

  Ningependa kuona na kusikia waziri kivuli wa sheria anatembelea mahakama kuu na kuona utendajio wao wakazi, huko ni kujifunza na kujiweka karibu na hao watendaji wakuu wa serikali yeyote duniani, vivyo hivyo kwa waziri kivuli wa mambo ya ndani, kwa mfano atembelee magereza, kwa waziri kivuli wa afya naye awepo mahospitali. Kwangu mimi huko ndiko kuwa chama mbadala unayejiandaa kuchukua madaraka watati wowote.

  Amka Chadema anza kufanya kazi.

  Natanguliza shukrani,

  J J Pikadili.
   
 2. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wasalamu wanajamvi?

  Nianze na kusema kwamba nawapongeza sana uongozi wa juu wa Chadema mpaka hapa walipo fika kwa mafanikio makubwa ya kisiasa zaidi ya chama chochote cha siasa kilichowahi kutokea hapa kwetu Tanzania.

  Pamoja na kuwa na mafanikio hayo haimaanishai kwamba hakuna wanapokosea, kupo tena kwingi tu. Kwamfano wamefanikiwa sana kujiwekeza katika vyuo vikuu na mashule, kwani kwa sasa ukiwa unadai haki hako ukiwa shuleni jibu la kwanza unaloambiwa wewe ni Chadema. kwa hilo nawasifu sana kwa kuamsha ari ya wanafunzi.


  Kwa mimi binafsi ningependa sana kuona Chadema kwasasa inachukua hatua na kuanza kujiwekeza kwenye makundi mengine ya kijamii kwa mfano akina mama, sijui baraza la wanawake Chadema linafanaya nini? Sijui kwanini viongozi wa juu hawataki kuchukua hatua yakulijenga baraza hili na hatimaye chama kwa ujumla wake. Kwa wafanya kazi waserikali vile vile.

  Serikali kivuli ya Chadema yaani serikali ya upinzani haifanyi kazi yake ipasavyo hata kidogo, kuweza kusema kwamba hiki ni chama mbadala, bado siwezi sema hivyo sijaona hata waziri kivuli mmoja ambaye ni active memba kwenye wizara yake.

  Ningependa kuona na kusikia waziri kivuli wa sheria anatembelea mahakama kuu na kuona utendajio wao wa kazi, huko ni kujifunza na kujiweka karibu na hao watendaji wakuu wa serikali yeyote duniani, vivyo hivyo kwa waziri kivuli wa mambo ya ndani, kwa mfano atembelee magereza, kwa waziri kivuli wa afya naye awepo mahospitali, na mawaziri wengine na wizara zao. Kwangu mimi huko ndiko kuwa chama mbadala unayejiandaa kuchukua madaraka watati wowote.

  Amka Chadema anza kufanya kazi.

  Natanguliza shukrani,

  J J Pikadili.
   
 3. N

  NGONYA NM Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunapokea salam lakini nina wasiwasi na ufuatiliaji wako wa mambo Je unafahamu waziri kivuli wa mambo ya ndan ninami? Unafikiri anaposema nimehamua kwenda rumande kwa hiari yangu mwenyewe ALIKWENDA KUFANYA NINI? NATHUBUTU KUSEMA They are active than hi ya ccm ndg zito waziri kivuli wa uchumi alieleza jinsi yakukabiliana na mfumko wa bei. Je umeshamsikia mkulo?sheria ni Tundu lisu amelitikisa bunge na hata rais anajianda kupeleka sheria yamabadiliko ya alichosaini Ndug yangu CHADEMA SIO WA2 WA HOVYO KAMA WENGNE NA VIONGOZ MAKINI NA SERIKAL Yetu imeonesha njia kwamambo meng hzo ni cheche subiria tukamtae nchi 2015 MUNGU IBARIKI CHADEMA MUNGU IBARIKI NCHI YA ASALI NA MAZIWA INAYOLIWA NA WACHACHE
   
 4. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtoa mada una mawazo mazuri ambayo uongozi wa juu wa chadema inabidi waufanyie kazi hasa hili la mawaziri vivuli, Ni zitto tu ndo anaonekana kufanya uwaziri wake vizuri wengine wote hakuna kitu, Lissu ni kweli anajitahidi lakini mawaziri wengine waliobakia mbona hatuoni lolote wanalolifanya?
  Wanatakiwa wawe wanafuatilia kwa karibu mambo yanavyokwenda ktk wizara zao husika na kutuhabarisha sisi wananchi wakiwa wametoa na njia mbadala. swala la kusubiria kuonekana na kusika wakati wa bunge tu haitoshi.
   
 5. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mdee mtu wa makazi lakini hata kwenye mafuriko sikumsikia. msigwa pamoja na kuwa ana hoja nzuri ila kapiga usingizi na wengine wengi tu wamelala. Kutegemea mikutano ya Dr Slaa peke yake ni kumuumiza mzee wetu. Naamini wote wakifanya kama zitto chadema itakaa imeshaini muda wote
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  tunahamasishana sana..hii ni moja ya mikutano

  [​IMG]
   
 7. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu Ngonya NM heshima mbele
  Kwanza mimi ni mfuatiliaji wa mabo kuliko unavyodhani, Kwanza swali la kujiuliza Chadema wana mawaziri vivuli wangapi? Wangapi wako active? Kwenda rumandemande mwenyewe kwa Mh Lema si kwenda kama waziri kivuli bali alikwenda kama mbunge wa Arusha mjini. Tunataka kuona utendaji wa mawaziri vivuli na si kama mbunge.

  Wapi alipo waziri kivuli wa nyumba na makazi? Lini umesikia Lissu amekwenda mahaka kuu kuangali utendaji wa mahakama hiyo?
  Tunachotaka nihawa watu kutumia nafasi zao hizo kuonyesha kama wanaweza. Nataka nikuhakikishie kitu kimoja mkuu huwezi kuchuka nchi ukiwa na watu ambao hawaelewi utendaji wa serikali.........
  Kwasasa Chadema ilibidi wajipange zaidi kiutendaji kuonyesha kwamba wanaweza kuendesha nchi. Nafasi waliyoipata ni adimu sana na katika nafasi hii wanaweza kujenga au kubomoa, sisemi hivyo kwasababu naichukia Chadema bali kutaka kuijenga.

  Ulishajiuliza swali hili kwamba kunauwezekano wa Chadema kama chama kimekuwa na kikafika mwisho wake wa kukua?

  Nawasilisha
  J J Pikadili.
   
 8. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu Gwota heshima mbele mkuu

  Nadhani umeniso mkuu, chama kimekuwa kikimtegemea Slaa peke yake, inakuwa kama tunajenga jamii ya nabiii mmoja naye akiondoka hamana la kufanya tena.
  Uongozi ni kama mpira wa miguu ukitaka kushinda lazima wote muwe mnacheza kwa pamoja na si kutegeana, mkianza hivyo lazima mshindwe na hili ndilo linalotokea kwa Chadema kwa sasa.
   
 9. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu na wengine je?? ulishawahi kusikia huyo ndiye waziri wa aridhi? au viwanda? jiulize?
   
Loading...