CHADEMA wapelekana kortini

Umenikosha kwa sentensi yako fupi na iliyobeba maana kubwa.

Hiyo ndiyo Democracy ya kweli, kama hukubaliani na jambo unapeleka shauri lako kwenye chombo cha kutafsiri sheria ili haki itendeke na sio 'kumpiga mtu bomu' au 'kitu kizito'.
 
Kwenda mahamani ni haki yake, we unadhani huku ni ccm kwenye nidhamu ya woga kama jamaa wako wa nzega? Acha waende kutafuna haki yao pale wanapooa wameonea huko ndiko tutajua kila kitu
 
Unatakiwa nawewe ujaribu kutumia kichwa chako vizuri. Kama kila siku unasema kwa sentensi fupi hivi zisizo na maana wala facts utabaki kuwa mzushi na muongo tu.

Hebu jaribu kuthibitisha kauli yako ili ueleweke mkuu.

nilishasema siku nyingi tu cdm ni wasanii
 
Ilikuwa Arusha na sasa ni mwanza yangu macho
 
hapo hawajachukua dola!! ugomvi moja kwa moja, je wakichukua??

Neno ugomvi kwako ni MSAMIATI chama kupitia vikao halali vimefukuza wahuni halafu wahuni wamekimbilia mahakamani hapo ugomvi uko wapi, ugomvi ni kama ule wa NZEGA watu wanashikiana BASTORA.
 
Hakuna mtu bora kuliko chama.matata na chagulani wamefika hapo kupitia chama.matata alikua ccm,alikuwa anagombea udiwani kupitia ccm,kwa mujibu wa watu ni kuwaalipata kura 2 ktk kura za maoni.baada ya kushindwa tu aliamua kugombea kwa tiketi ya cdm na kupata udiwani.Matata na chagulani wamekubalika kupitia chama.wengi wa madiwani wa cdm mza hawana elimu na waligombea basi tu baada ya watu kutojitokeza wakijua kuwa cdm haina nguvu mza.Hata Wenje asijisifu,naye aliingia kwa kubahatisha,hakuwahi kujulikana na hakupewa kabisa nafasi ya kushinda.viongozi wa chama mza sasa hivi hawawezi kuendana na kasi ya ukuaji wa chama,kwani cdm inakua kwa kasi sana mza.kuhusu chagulani kuzuiwa kufanya mkutano hizo ni njama za ccm kutaka kumpa umaarufu tu.huyo dogo hana lolote.sisi wana mza tunasubiri kwa hamu huo mkutano wa kujimaliza kabisa kwani hatapata watu zaidi ya wanaccm wenzake walioandaliwa.
 
Gwandaz, walikuwa wanasema hawana imani na mahakama. Kulikoni?
 

Matata anataka angejadilikwa na kamati ya wilaya kisha mkoa.Je huko kamati ya wilata na mkoa kuna watu wangapi.Period
 
Kwa akili yako ndogo, usanii wao upo wapi?

Kifarutz;Kila siku huwa sikubali siasa hizi zilizoibukia CHADEMA za kufukuza viongozi waliochaguliwa kwa kura za wananchi!Haiwezekani na ni kuiminya demokrasia kwa KAMATI KUU-CHADEMA yenye wajumbe si zaidi ya 20 KUWAFUKUZA MADIWANI/WABUNGE waliochaguliwa kwa kura nyingi za wananchi tena wengine wasio shabikia chama chochote(independents)!

Siasa hizi za kufukuzana nazipinga;kama mwakilishi kaenda kinyume na CHADEMA na hataki kujirekebisha inabidi tu ATENGWE NA APUUZWE hadi mwaka 2015!
 
Gwandaz, walikuwa wanasema hawana imani na mahakama. Kulikoni?
Shule muhimu: CDM haina imani na baadhi ya majaji na mahakimu wa mahakama si mahakama na ni baadhi... ok na toka Lissu awaumbue live wamenyooka! subiri hukumu ya Lema uone wanavyojipendekeza.
 
Shule muhimu: CDM haina imani na baadhi ya majaji na mahakimu wa mahakama si mahakama na ni baadhi... ok na toka Lissu awaumbue live wamenyooka! subiri hukumu ya Lema uone wanavyojipendekeza.

Bado hujajitetea ipasavyo, kama umechanganyikiwa vile.
 
Hizo ndo sera zilizotufikisha hapa, kamwe siziungi mkono. Msaliti yeyote inafaa atimuliwe mara moja. Chenge mwizi, Jairo, Ngeleja, Kikwete etc.. ni mifano mizuri, hao ni wasaliti wa taifa! Sera za kuvumiliana na kulindana hazina nafasi CDM. Tunachukia kumfukuza mtu ila usaliti tunauchukia zaidi. Kumbuka kuwa CCM ni mafia, wameingiza mapandikizi ndani ya chadema hivyo basi to make a story short maamuzi ya mwisho yanabakia kwa kamati kuu. Chadema bahati nzuri hatuna ombwe la uongozi. I repeat, hatufurahii kufukuza watu ndani ya chama. Bado shibuda huyu naye ni pandikizi na mabwepande
 
Mimi ni Mmoja wa watu waliotoa onyo kwa CHADEMA kuruhusu matata kugombea na kushinda umeya wa jiji la mwanza kwa sababu ya historia yake ya Ujambazi na Ukwepaji wa Kodi, hata Hotel yake ya Magnum pale ilipojengwa ni eneo la uwanja wa wazi ambalo alilichukua kibabe wakati huo kaka yake akiwa kigogo hapo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Mwanza.

Na ninaendelea kuunga mkono maamuzi ya kumfuta uanachama Japo yamechelewa sana
 

Matata waulize wenzako wa arusha uzuri wa cdm maamuzi yao uwa awakurupuki kutumia magazeti na mahakama ni kubuy time .M4c ikija mwanza ukweli wenu utawekwa hadharani.
 
Duh ,wanalaani kitendo cha mishe zao kutangazwa katika vyombo vya habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…