Chadema waonyeshe mfano katika hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema waonyeshe mfano katika hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Feb 16, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pasi na shaka CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye nguvu kwa sasa. Katika uchaguzi uliopita CHADEMA wameonyesha wanaweza, huku vijana wanaharakati na wasomi wakipata nafasi za ubunge.

  Katika issue ya wabunge kupewa milioni 90 za kununulia magari, nilitegemea CHADEMA wawe mstari wa mbele kupinga fedha hizo kwa vitendo na si kusema tu. Fedha hizo ni nyingi sana hasa katika kipindi hiki ambacho maisha kwa wananchi wa kawaida yamekuwa magumu. Katika issue hii sijawasikia CHADEMA wakisema chochote, mbali na Mh.Lema. Moja kati ya sera ya CHADEMA ni kupunguza matumizi ya serikali. Je, katika hili milioni 90 za kununulia magari sio matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi?

  Hapa CHADEMA lazima waonyeshe mfano na kuzikataa fedha hizo ili kujitofautisha na chama mfu cha CCM, vinginevyo wananchi watashindwa kutofautisha walanchi na watetea nchi.

  CHADEMA SHOULD TALK THE WALK AND WALK THE TALK!
   
 2. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Dharura ya kuondoa mgao wa Umeme au magari ya wabunge? Which has highest priority this time?
   
 3. n

  nchasi JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  CDM siku zote tunawaamini. Tunawasihi ili muendelee kutujengea imani ktk hili la 90million hebu wekeni bayana kuwa hampo tayari kufumbia macho ili hizo pesa zilete maendeleo ya Shule za Kata na kuboresha angalau maslahi ya walimu. Jamani walimu wanatakiwa wajaliwe ili waweze kufundisha watoto wetu kwa moyo. TANZANIA INAHHTAJI WABUNGE MAJASIRI KAMA WA CDM. Tuwakilisheni ktk kutetea rasilimali za TZ ziweze kuwafikia wote. Naamini wabunge mtaona ujumbe wetu na mtaufanyia kazi, tutawaona wasaliti kama hamtasema lolote jambo. Tuangalieni raia wenu au na nyie mlitumia gharama kubwa kwenye kampeni kwa ajili ya kuhonga watu wawachague sasa mnataka kufidia. Tunaamini hamkufanya hivyo maana ni sisi ndio tuliwalinda mpaka mwisho, tunawaomba mtutetee maana hizo ni kodi zetu ambazo mkipokea sisi huku maisha yanakuwa magumu sana ili tufidie hilo gape. Maana lazima maisha yapande mara dufu hata nyie ni masgahidi kwa maisha yalivyo sasa.
   
 4. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu umeanza vizuri ila kuna machache nitakukosoa kabla sijakuunga mkono katika hoja yako.
  1.Hii dhana ya Chadema kuna wabunge wasomi sielewi!kwa level ipi?maake wengi ni kama Vicent Nyerere,Mr II ama rafiki yangu Lema.Tuache kuhuisha visivyokuwepo sema wabunge "machachari".
  2.Kuna dhamira kuu na dhamira ndogo.Dhamira kuu ya Mwanadamu utawaliwa na tamaa za kiroho kwa maana ya vitu kama pesa na vinginevyo.Hawa wanasiasa hasa CDM wengi ni watu wa hali ya chini kimaisha na ubunge ni "Zali" tu kwa maana haikutarajiwa,hivyo kwa ukata hawezi kuthubutu kurudisha fedha ama kugeuza matumizi kwa manufaa ya citzens,tena fedha yenyewe mkopo.

  Ila itakuwa bora kwa atakaye tangaza kufanya kama tunavyopendekeza.Wanasiasa wengi hawadumu katika nafasi zao hasa ubunge kutokana na ahadi zisizotimilika mfano: Bunge la sasa limepoteza asilimia 70 ya wabunge wa bunge lililopita.Kusema na kutenda wengi kwao ni vitu viwili tofauti!Yataka Moyo!
   
 5. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumbukumbu zinaonyesha CHADEMa walishawahi kupinga haya magari pamoja na mishahara ya Tshs. 7,000,000/- .kilichotokea walizomewa sana na kufuatiwa na vijembe vya mbwa mwizi.
  Ushauri wangu kwao ni kuzipokea kisha kununua magari rahisi. pesa inayobaki waeinde majimboni mwao wakaitishe harambee ya kuziongezea ili kununua ambulance za hospitali za wilaya zao. kwa majimbo yenye wabunge wawili Gari husika zipelekwe kusiko na Wabunge wa CHADEMA lakini kwa maandamano makubwa ya kuhamasisha wananchi watambua mchango wa CHADEMA!
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Good, one of good ideas, tatizo ni kwamba watendaji wako wapi?
   
 7. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mi mtazamaji kwa hili, sitii NENO kwa kweli.
   
 8. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa mchango wako,japo tukubaliane kutofautiana katika dhana ya usomi?msomi ni nani/anatakiwa awe na elimu gani
  ?anyway,CHADEMA lazima wachukue hatua katika hili,vinginevyo tutawageuka.Tuumhangaika pamoja,tumeumia pamoja,tumepiga kampeni pamoja,tulikula pamoja na kulala pamoja,kwa nini hili litutenganishe?
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haya hapa ndio pakuanzia,hiyo hela waikatae nasi wananchi tusikie kuwa wabunge wa CDM wamefanya kweli.

  Kusema kweli hili linawezekana kabisa kwani mshahara wao unawawezesha kabisa kununua gari ,wabunge wa Uingereza wanatumia baiskeli,nawashauri Chadema wakatae katakata .

  Kubwa zaidi ambalo limesemwa na Tundu Lissu .....""Historia haiheshimu wanaoogopa, tusije kusahau bei ya mabadiliko, bei yake ni kupigwa, kufungwa hata bei kubwa zaidi ya kifo,"....! Huu ni ujumbe tosha ambao kila mzalendo ni lazima afahamishwe na niliwahi kusema hapa JF kuwa njia wanayoipita Chadema inacost hizo alizozitaja Lisu ,hivyo isije kuonekana kuwa CDM inawatosa wananchi ,hapana njia inayopitwa sasa ni njia ya hatari hivyo kila mmoja ni lazima aijuwe na kama haijui ajulishwe,ili isiwepo lawama baadae.Hongera Mheshimiwa kwa kulielewa hilo na kulitangazia ila usiwache kulitangaza kila utakaponafasika.Kwani wengine ni masito.
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nilifikiri namna hii lakini tatizo linakuja, huu ni mkopo ambao mbunge husika anatakiwa kuulipa, sasa nani yuko tayari kupokea kuupeleka kwenye ambulance afuye anabaki anadaiwa, hapa chadema must come out clean, hakuna haja ya kukubali hizo pesa
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180

  Nadhani Mr Mwankuga wote mmepoteza uelekeo. Hoja yako ukiangalia kwa haraka utaona kama vile kuna favor wabunge wamepewa. Lakini ninaona kulingana na nafasi zao hao waeshimiwa huo ni mkopo tofauti haukutoka Benki hivyo hauna liba.
  Hawa jamaa ubunge umetumika kama dhamana ya kuwakopesha fedha zote hizo. Kwa mahesabu ni kwamba wamepewa Tshs 90,000,000/= kwa muda wamiaka mitano. Miaka mitano ni miezi sitini (60months). Watakatwa Tshs 1,500,000/= kila mwezi kwa miezi sitini bila liba.
  Mkopo huu utawafanya waheshimiwa hawa waweze kuanza maisha ya ubunge vizuri kujiweka sawa, usafiri, nyumba ya kuishi na mambo mengine kadhaa kwenye maisha yao ya ubunge. Hizo fedha ni mikopo na wajue wanazirudisha polepole!!!!!!!

   
 12. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu asante kwa kuweka mambo sawa kwamba huo ni mkopo na wala sio pesa kwamba wamepewa bure kwa ajili ya kununulia magari. Leo tunasema wabunge wa CHADEMA wazikatae hizo hela halafu iweje wakiishazikataa? Kwamba wabunge wa CHADEMA hawapashwi kuwa na magari yenye hadhi na yatakayowawezesha kutembelea wapiga kura wao kwa ufanisi zaidi? Kwa mawazo yangu sio sahihi kuzikataa hizo pesa ila kama mchangiaji mmoja alivyosema wanaweza kuchukua hizo pesa, wanunue magari yenye bei ya chini ya hapo na zitakazobaki wazipeleke kwenye majimbo yao kusukuma maendeleo!!!! Kuzikataa hizo pesa kwangu mimi sio uamuzi sahihi.

  Tiba
   
Loading...