Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
kabla ya kujadili turejee uamuzi wa Serikali ta Tanzania kuzuia Bunge kuoneshwa ''live''. Hapa ndipo ''kiki'' zilianza,ukuta ukazaliwa na harakati ''mfu'' ikiwemo kuandika barua lukuki kwa umoja wa ulaya na Marekani.
Kama kweli Chadema ni chama cha ''kidemokrasia'' kiutangazie umma wa Tanzania kupinga udikteta wa Marekani na Uingereza dhidi ya bunge na wabunge.
Nianze na Marekani, mwezi uliopita tumemshuhudia Trump akiwabagua wabunge wenye asili ya kiafrika na kilatino huku ukizingatia kuwa yeye hakushinda uraisi kwa kura nyingi bali kwa kupora ushindi kupitia 'NEC' yao inayoundwa na genge linalojiita ''electoral college''.
Uingereza, hawa amiri jeshi mkuu ni malkia/mfalme ambaye hapigiwi kura na wabunge wote huapa kiapo cha kutii maamuzi yake bila kuwa na fursa ya kupinga mahakamani kwani yeye ndiye ''katiba''. Zaidi ameidhinisha amri ambayo itawakosesha wabunge wa uingereza haki ya kujadili mustakabali wa taifa lao kuhusu kujitoa umoja wa ulaya. Chadema kumbukeni mliandika barua kuwaomba hawa wazungu wawasaidi ili Bunge liwe ''live'' sasa angalia wao wanafanya nini?
Kibaya zaidi, Chama cha Conservative ambao chama tawala ni chama rafiki yenu mara kadhaa mmetamba kushirikiana nao.Kiongozi wa Conservative ambaye ni Waziri mkuu wa UK kaandika barua kumshawishi malkia ambaye yupo juu ya katiba na bunge ''kuwapiga pin'' wabunge.
Mkiendelea kuandika barua kuomba msaada wa ''kidemokrasia'' kutoka uingereza na Amerika mnapata laana.Huwezi kuomba thawabu toka kwa shetani labda uwe ''kashetani''.
Nimalize tu kwa kusema 'makamanda'' msio na madhara amkeni kumekuchaa.