CHADEMA wanaweza kuingia kwenye Serikali ya mseto na CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wanaweza kuingia kwenye Serikali ya mseto na CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Feb 16, 2012.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sheria ya uanzishaji wa Katiba mpya imepitishwa Bungeni baada ya maridhiano ya Chadema, CUF, NCCR na vyama vya kijamii na kufanya sheria hiyo iaminiwe zaidi na wadau. Kutokana na Rais kuridhia mapendekezo ya Chadema na kuanzisha maelewano ambayo Bungeni waliyaita MAPENZI YA MDA inaweza kuanzisha makubaliano ya kuanzisha Serikali ya mseto kati ya CCM na Chadema Tanzania Bara kama ilivyo kwa CCM na CUF Tanzania Visiwani?
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,744
  Trophy Points: 280
  suicidal!
   
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nadhani chadema na ccm ni wazoefu katika mambo ya serikali za mseto.ulizia kigoma na tarime.au mkuu una kipya cha kutueleza?
   
 4. Mnusaji

  Mnusaji Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  laaabuda yatokee maajabu............umoja wa kitaifa mpaka damu imwagike kama kule zenj sio kirahisi..........hara kenya walidundana sana tuuuuuu
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kiini cha serikali ya mseto ni kwamba mshindi wa wazi ktk uchaguzi mkuu hakupatikana (chaguo la wananchi).. sii nchi imeshindwa KUTAWALIKA (chaguo la viongozi) kama inavyotumiwa na nchi za Kiafrika. Tumepoteza maana na matumizi ya neno hili na ndio maana hata serikali za mseto huwa hazileti mabadiliko kwa wananchi bali neema kwa viongozi.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi naona kama mwanzo mzuri kwa hata marekebisho ya Katiba ya CCM yanawaweka kando wenye siasa kali ndani ya CCM. M/kiti atakuwa na nguvu ya maamuzi na kusikilizwa kuliko mwanzo. Hata mimi siwaamini baadhi ya viongozi wa CCM hata kama M/kiti ana nia nzuri yaliotokea Bungeni baada ya Rais kukubaliana na Chadema na vyama vingine Wabunge wa CCM walikuja juu na kutaka kumgomea M/kiti wao.
   
 7. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwamadhaifu ya ccm sizani kama kina Mzee mtei watakubali huo ujinga. na kama activist ninaona chadema ikikubali hilo nadhani ndochadema kitakua kinachungulia kaburi kama c.u.f
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hilo haliwezi kutokea hata kidogo.... Tanzania bara hatujafikia hali iliyokuwepo Zanzibar.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CHADEMA haijafikia kuwa tishio kwa CCM kama ilivyokuwa kwa CUF, hata hivyo CUF imeangukia pua CHADEMA ndiyo itaweza wakati haijaweza hata kujitanua nchi nzima?
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Naomba kutofautiana na wewe. Kukubali kuingia mseto na CCM ni kama unamwongezea uhaki mgonjwa aliye mahututi. Kinachotakiwa sasa hivi ni kumzika mfu na si kumwongezea mashini ya kupumua.
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Naongezea kwa Mkandara kwamba serikali ya mseto ni pale kinapokosekana chama chenye wingi wa kutosha kuunda serikali pekee yake. Ikitokea vyama vimeshindwa kukubaliana basi unaitishwa uchaguzi mpya! Hii inayofanyika Afrika kama ambavyo tumeona Zimbabwe,Kenya na hata Zanzibar ni demokrasia ya viongozi wa vyama kugawana madaraka!
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe kwamba Tanzania kwasasa hatuko ktk hali ambayo CCM inalazimika kushirikiana na chama kingine kwasababu inao wingi wa kutosha kupitisha miswada yake bungeni. Hata hivyo hali hiyo haitaendelea milele,miaka michache ijayo tunaweza jikuta hatuna chama chenye wingi wa kutosha bungeni kuunda serikali pekee yake. Automatically lazima iundwe serikali ya mseto. Kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea vyama husika vinakutana na kukubaliana hata sera na serikali ya mseto itakavyoendeshwa. Mimi huwa nashangaa mseto wa Zanzibar ninaposikia sera ni za CCM,sasa CUF wanafanya nini ktk hiyo serikali?
   
Loading...