binafsi sioni kama ni kosa kwa Chadema wanachofanya sasa. ila inabidi waende mbali zaidi na kuongezea strategies zaidi,. ,mfano wanapofanya maandamano katika kila mkutano ingependeza zaidi ikaambatana na kufungua matawi na kufanya survey ya watu gani strong katika kila mkoa ambao wanaweza kuweka uhai wa chama (hapa inabidi kuwa makini wasije wakawawaweka mamluki). On top of that wanatakiwa wawawekee mpango mkakati wabunge wote (including performance indicators) ili waweze kutekekeleza yale ambayo yameshindwa na chama tawala. in fact i was put off kusikia kuwa kuna baadhi ya wabunge wa chadema wanashinda kwenye baa huko kanda ya ziwa badala ya kuchapa kazi kusaidiana na wananchi kuleta maendeleo (katika hili Chadema inabidi kutengeneza code of ethics).
Aidha, kama Chadema wanataka kufanikiwa zaidi katika uchaguzi wa 2015 inabidi kujizatiti zaidi katika level za chini, hasa vijijjini na maeneo ambayo walipata kura chache mfano Lindi, Tanga, Mtwara, Zanzibar, Singida, Tabora, Manyara.
suala la kupambana na ufisadi waongeze nguvu lakini liende hand in hand na mambo mengine yatakayowasaidia watanzania kunyanyuka angalau hatua moja mbele.
swali ninalotaka kuwauliza chadema: Je mlishawahi kufanya POSTMORTEM ya uchaguzi? inawezekana suala la hitilafu za uchaguzi isiwe sababu tosha ya nyie kushindwa, kuna sababu nyingine zinatotakiwa kuibuliwa na kufanyiwa kazi.. CCM ikiwapiga bao 2015 msishangae!!