CHADEMA wanani dissapoint kwa kweli



joining date yako ni baada ya ccm kujivua magamba na kipindi hicho jf ilishambuliwa sana na wavua magamba kwamba inatumiwa na cdm kuwapotosha wanachi. wana magamba wakakubaliana na wao watumie mitandao vizuri ili kujisafisha uozo wao. kuanzia hapo tumepata member kibao humu ndani and kitu cha kushangaza hao wageni wengi wao wana sera za kimagambamagamba!!!!!!!!! nina hofu tumeingiliwa humu jf.
 

Unakerwa na CDM NA RAIS WA MOYO WANGU DR SLAA kwa sababu unataka kuingia CDM while ujajivua gamba,nakushauri jivue gamba then mtafute mtumishi wa Mungu akuungamishe dhambi zako then uje CDM hakika hautajisikia vibaya tena.
 
watu wengi tu walishasema kuhusu chadema kujibadilisha kisera, kimtazamo na ki-organisation, naona ujumbe unazidi kuwaingia , tusubiri wamalize hii ngwe, tuone kinachofuata.

siku moja niliuliza, hivi ikitokea, jk akajifanya kichaa, awafunge akina mapacha watatu, je cdm itakuwa na hoja gani ya mvuto?
kujiimarisha kwa kutumia udhaifu wa mwenzio sio deal.
wakubwa eee, sikilizeni ushauri.

HONGERA SANA BOSS
 

Anayeweza kujibu vizuri swali lako kwa sasahivi wakati bado jk hajachukua hatua ni sheikh yahya pekee.

Lakini kama unataka kujua kwa uhakika kwamba chadema itakuwa na hoja gani ya mvuto mwambie jk afanye hicho unachotamani, ama vinginevyo kamuulize makamba chadema walikuja na hoja gani wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010. Nikukumbushe makamba alipokuwa akimtambulisha jk kwa wanaccm baada ya kuchukua fomu za kugombea uraisi aliwaambia wananchama wake kwamba Dr. Slaa asiwatishe kwakuwa wanaijua agenda yake, ni ya ufisadi na tayari ccm ina majibu ya agenda hiyo.

Sasa baada ya uchaguzi mkuu, ccm imejua kwamba chadema walikuwa na agenda gani wakati wa uchaguzi, na baada ya chadema kuendelea na moto wa maandamano ccm wameanza kulalamika na zaidi ya hapo wameamua kuvuana magamba na gamba la kwanza kuvuliwa amekuwa ni makamba aliyedhani amemaliza agenda ya chadema.Sasa na wewe angalia usije kuingia kwenye mtego wa makamba na ccm kama we si mmoja wao.
 


Ndugu yangu naona umeniwahi, kidogo!
Wabongo tuache uoga, naelewa kuwa siasa zinazopigwa na CDM ni ngeni sana miongoni mwa wa TZ wengi.
Mvutano wa kisiasa kati ya CCM na CDM saivi wengi wanauona kuwa ni "malumbano yaisyo na maana kwa watu"
Inawezekana ikawa kweli, ila kwa maoni yangu nadhani yanaumuhimu sana sababu mwisho wa siku haijalishi kwa mbinu gani (ilimradi ni kisiasa) KITAJULIKANA CHAMA MAKINI.
 
Mi nadhani hoja ya The Boss ni ya msingi, si kila kitu cha kujibujibu tu. Kwa nyakati zetu hizi ambazo watanzania wanakuwa katika kufikiri na kuchambua mambo ni vizuri kwa CDM kuendelea na kampeni yao ya kueleza matatizo ya nchi hii na kutuaminisha kwa sera na itikadi zao ni kwa kiasi gani zinaweza kutatulika. Sisi wananchi tutachambua pumba ni zipi na mchele ni upi. Mi nawasifu CDM ni watu makini wako tayari kuchukua ushauri na kuufanyia kazi. Sio siri yale ya Mpendazoe sidhani kama yanafaida sana kwa CDM
 
Utakuwa disapointedi sana tu, na bado. Makamanda endelezeni mapambano kwa kutumia silaha zote. Hawa wanaokuwa disapontedi wala wasiwashuhulishe sababu hawana msaada wowote: Zaidi ya kuwa disapointedi. Pipooooooooooz....
 
The Boss yuko sahihi though pia sikubaliani na Mr Mark,wanachofanya cdm c kufundisha wananchi kuichukia nchi/serikali yao bali kuwaelimisha juu ya mambo ya msingi na kutowajibika kwa serikali ya ccm. the only problem I see wit cdm ni ile kubase kwenye mada moja -ufisadi, kurushiana majibu as if hakuna mambo mangine tangible. otherwise move yao cdm ni nzuri waifanyie marekebisho/maboresho tu
 
Hii ni budget season!!!....mkulo ashatoa draft yake like 2months ago,zitto katoa yake like a week ago,wana jf bado tupo kwenye malumbano ya nani muhuni na nani mstaarabu.Hivi tunajua tunachokiface?.....Cdm now is like NCCR in the late 90s but on steroids!
 
Mleta mada, tutaanza kudoubt curiosity yako. Ni lini ulisikia mwana CCM anamsema live Dr fake, au Makamba au Lowasa laivu hapa jf?

Au unaleta ile tunaita positive criticism ili kushake after use vichwa vya wachangiaji?

Nakuacha na maneno ya Achebe: "we should first chase the fox into the forest,then we come back to warn our hen of wondering in the forest".

Mchangiaji kashasema, hatutakubali kumuacha adui mwenye panga vitani, eti kwa kuwa amiri jeshi kasema tumsake adui mwenye bunduki.

Wote ni hatari mkuu,

Tafakari, chukua hatua.
 
Mkuu pia umesema umekuwa disappointed ,lakini hukueleza ni lini ulikuwa umekuwa appointed! Lugha mchanyato utachanyata hata hoja za wachangiaji! Tulia ueleze dukuduku vizuri,pia soma michango ya wanahoja ndugu!
 

Panga kwa panga au siyo!..Usinikumbushe makamba alivyofyata! he he
 





hizo point 3 ulizoziainisha kwanza zitoe...kwa sababu zifuatazo
1...CDM kama chama cha upinzan tanzania kinatakiwa kieleze mabaya na mema kidogo dhidi ya chama kilicho na dola kwa hiyo hizo habari ya kwanin kinaongea cna mambo ya ccm ni wajibu.

2.kwa kua kina uchungu na hali ya maisha kwa wananchi kwa ujumla lzma kisema hali iliopa kta misingi ya gharama za maisha kulinganisha na kipato cha mtu ili jamii ielewe,kwa kuwaambia watu hali ni tete ni moja ya msaada kwetu

3.kuhusu swala la media acha kama lilivyo koz ushasema media inasema wanatumiwa...
 
Naona mwanzishaji wa hii thread alishakata tamaa kabisa hata kama ukifanya lolote jema. Mimi binafsi nafikiri hiyo strategy wanayotumia CHADEMA ku-REBUT uongo unaoenezwa na CCM ni nzuri. Hata Jaluo wa Marekani (Obama) alitumia the same strategy ku-shut down uongo uliokuwa unaelekezwa kwake na Republican na Talk Radio hosts wa ki-conservative wakati wa uchaguzi mkuu US. Matokeo yake conservatives waliumbuka.

Huwezi kunyamaza wakati uongo unaundwa kuwa ukweli. JK alitajwa kuwa ni fisadi, hajawahi hata siku moja kukanusha hilo wala kwenda mahakamani kwa kuchafuliwa jina. That means anakubaliana na hao waliomtuhumu kwa ni fisadi. Na hakuna Ubishi katika hilo, JK is FISADI.

Ni vema CHADEMA wakaendelea ku-rebut uongo wa CCM kwa uthibitisho.
Kudo CHADEMA.
 

Kwa maoni yangu, kukosa focus ndiko kunakosababisha kuingia kwenye mitego ya kuingia kwenye malumbano ambayo kwa bahati mbaya hayana tija yoyote kwa mwananchi wa kawaida.

Mimi nitaelewa kama chama kitafanya hivyo kinapokuwa under attack na hasa inapohusiana na viongozi wake, lakini hiyo haiwezi kuwa ni mpambano wa kudumu kama inavyoonekana kuwa sasa hivi.

Hali hii itawafanya wafuasi wao na most importantly, watanzania wataona wazi kabisa kwamba pengine chama hiki hakiko issue driven bali ni mkusanyiko ambao unasubiri kuona kuna mabishano gani na wao wajiingizeje ili kuendesha vita vya maneno na kuibuka washindi.

Kuna mambo kadhaa yanayohitaji kutengeneza a legislative agenda ambayo itawasaidia kulisukuma bunge kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi ulio huru zaidi na pia kuandaa mazingira mazuri ya namna nzuri ya kulinda rasilimali zetu na kuwafanya wanachi kufaidika zaidi.

Mikutano ya hadhara, pamoja na uzuri wake, haitoshi kukiweka chama kuwa karibu na wananchi kama hakuna juhudi za makusudi za kujenga mazingira ya kujenga kuaminiwa.

Miaka mitano ni kipindi kifupi na kama wasipojijengea mazingira ya kupigania mageuzi, wasikae kuja kupiga kelele wakati wa uchaguzi na kuchochea wananchi kufanya machafuko kwa mambo ambayo wana fursa ya kuyabadilisha leo lakini wako busy kulumbana na kulia lia.
 

That is completely a wrong approach coz siyo kila wakati unaweza kujibu kila tuhuma inayokuja kwako na hiyo tafsiri yako kwamba kila ukikaa kimya basi unakiri ni potofu. Watu wanaoamini kwamba JK anahusika na ufisadi kwa sababu tu hakujibu hoja au matamko ya jukwaani na ambayo ni ya kutunga na matokeo ya conspiracy kati ya mafisadi na baadhi ya mawakala wao.

Kama CDM wanadhani wataweza kujibu kila hoja, tunawatakia kila la heri na tunasubiri kuona watakachokuwa wamevuna baada ya muda wa malumbano na hatutaki kusikia wakilalamika, na wewe advisor wao usiwakimbie baadae.
 
kweli kabisa chadema inabidi ishughulike na mambo ya wananchi kuendelea kujibizana na ccm ni kupoteza attention ya mambo ya msingi nakuunga mkono mkuu the boss

who is the duty bearer? Is it cdm or the govt of ccm?
The right holders are the tz communities the role of cdm is not to provide the services/rights to tz communities but to hold the duty bearers accountable to tz communities' rights.
 
who is the duty bearer? Is it cdm or the govt of ccm?
The right holders are the tz communities the role of cdm is not to provide the services/rights to tz communities but to hold the duty bearers accountable to tz communities' rights.
And how the f**k you gonna go about it?

 
Ma agent wa CCM ndani ya JF wala hawajifichi.

Kwani wa chama gani wanajificha, na kwanini wajifiche? Kwa dhambi ipi? Hili ni jukwaa la mijadala na kinachoshinda ni hoja na siyo chama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…