CHADEMA wanaiga style ya CUF ya miaka ya tisini!

CHADEMA wanaiga style ya CUF ya miaka ya tisini!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
38,534
Reaction score
31,199
Kwa wenye kumbukumbu mtakuwa mnalikumbuka sakata la IGP OMAR MAHITA(NGUNGURI) dhidi ya Chama Cha CUF(NGANGARI)

Hapa palitokea mikwara na ubishani kuhusu maandamano na mikutano ya hadhara na hatimaye CUF walichesea virungu kisawasawa na hadi leo hii wameufyata.

Sasa ninawashangaa washika UKuta wakitumia mbinu zile zile zilizoshindwa kwa kutarajia kupeleka kilio ICC.

Kupinga Utawala halali uliochaguliwa na raia wema ni uhaini uchwara na adhabu yake inajulikana.
 
Naona umeandika kimwwndokasi tu,huna hoja na zaidi unapotosha!Upinzani wanapinga uvunjwaji wa katiba unaofanywa na Serikali,wanatumia mikutano ya siasa kuuelezea umma juu ya ubakaji huo demokrasia!Mikutano iko kikatiba na ni haki ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
 
Iyo ilikuwa 90,hii ni 2016 pia iyo ilikuwa ni CUF peke yake ila hii ni UKAWA.(jishtukie)
 
Tatizo la chadema ni lipi kwani wao Kama chama cha siasa kutetea uhuru wao wa kufanya kazi Yao ya siasa ni kosa? Na hata huo mfano wako wa cuf na mahita je Nani alishinda? Mahita kastaafu lakini siasa inazidi kukua walitumia propaganda ya udini na vurugu lakini cuf ikazidi kukua na sasa ccm imepoteza mwelekeo wakati upinzan unazidi kuimarika huwezi kuzuia siasa kwani hapo ndipo watu hutoa Yao ya moyoni kuhusu serikali Yao na fahamu unapomzuia mtu kusema yaliyopo moyoni unatengeneza bomu kubwa ambapo baadae utajutia mfano mdogo ni Libya gadafi aliwanyima watu fursa ya kutoa ya moyoni nadhani uliona yaliyotokea ingawaje sasa wananchi wenyewe wanateseka
 
Kwani wanaopiga ivyo virungu nyie au sisi si mnatakiwa mfurahie mbona mnatufuatilia sana nyie
 
ingawaje sasa wananchi wenyewe wanateseka
Umejieleza vyema sana...pale libya watu waliamua kutumika na wazungu kama leo hii hizi NGOs za kisiasa zinavyotumika hapa Tanzania na madhara yake wanayaona!
 
Iyo ilikuwa 90,hii ni 2016 pia iyo ilikuwa ni CUF peke yake ila hii ni UKAWA.(jishtukie)
Ukawa ikawa iko wap, wewe kweli bado upo usingizini hiyo ni kushika ukuta, mbatia hayumo Maalimu na Duni Haji aka mzee wa chaliiii hawa more, ukawa ilikuwa ya kuivusha cdm kutoka kwenye matatixo ilokuwa nayo wakati huo, pole nenda kashikishwe ukuta
 
Naona umeandika kimwwndokasi tu,huna hoja na zaidi unapotosha!Upinzani wanapinga uvunjwaji wa katiba unaofanywa na Serikali,wanatumia mikutano ya siasa kuuelezea umma juu ya ubakaji huo demokrasia!Mikutano iko kikatiba na ni haki ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
Ibara ya ngapi ya katiba imevunjwa?
 
Tatizo la chadema ni lipi kwani wao Kama chama cha siasa kutetea uhuru wao wa kufanya kazi Yao ya siasa ni kosa? Na hata huo mfano wako wa cuf na mahita je Nani alishinda? Mahita kastaafu lakini siasa inazidi kukua walitumia propaganda ya udini na vurugu lakini cuf ikazidi kukua na sasa ccm imepoteza mwelekeo wakati upinzan unazidi kuimarika huwezi kuzuia siasa kwani hapo ndipo watu hutoa Yao ya moyoni kuhusu serikali Yao na fahamu unapomzuia mtu kusema yaliyopo moyoni unatengeneza bomu kubwa ambapo baadae utajutia mfano mdogo ni Libya gadafi aliwanyima watu fursa ya kutoa ya moyoni nadhani uliona yaliyotokea ingawaje sasa wananchi wenyewe wanateseka
Upinzani wa wapi umeimarika?
 
Screenshot_2016-07-31-12-09-55.png
Ibara ya ngapi ya katiba imevunjwa?
Kasome ibara ya 18 na 20,pia soma haki na wajibu wa vyama vya siasa!
 
style hii zunguka dunia nzima kama utakuta style hii iliweza kuzaa matunda zaidi ya kuzalisha walemavu na wakimbizi duniani wahasisi wa style hii hata wao wameicha ndo maana utakuta nw wanatafuta haki kwa style ya tofauti kabisa na naishangaa cku hzi chadema chama kilichoamika kuwa na hazina kubwa ya wasomi na maprof kuliko chama kingine chochote Tanzania wameshindwa kujua kuwa siasa za kiharakati cku hz hazina nafasi katika dunia ya kistarabu nataka kuwakumbusha kuwa kuna mihimili 3 kama wamekufunga mdomo bungeni na ikulu sehemu pekee inayoweza kukufungua ni mahakamani ni sehemu pekee ambapo serikari huwa inakubali kushindwa si bungeni au sehemu nyingine yeyote mahakamani ndio tafasili ya kile kinachotungwa bungeni hutafasiliwa mahakamani kama chama kinajinasibu kuwa na mwanasheria wazuri why kikafanye fujo na maandamano yasiyo ni manufaa au faida kwa jamii

kama wanakumbuka wakati kada wao geita kafariki serikali kupitia kwa police walikataa wasimzike lakini walipotumia mahakama mbona hao waliokataa wasimzike ndio walikuwa walinzi wao wakati wanamzika?????? je wangetumia nguvu au maandamano kupinga si wangewasababishia ulemavu watu huwezi hata cku moja kupambana na mtu mwenye police,jeshi,usalama,na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinavyo onekana na visivyo onekana vina report kwake na viko tayali kutekeleza order yake mda wowote ukashinda kwa njia ya violence ndo maana nawambia chadema waache siasa za harakati na kutaka sifa wafanye siasa za kisomi na siasa za ufahamu ndo maana siku hizi kuna siasa ya kisanyansi lakini enzi za siasa za kaharakati miaka 1960-1990 zimepitwa na wakati
 
Back
Top Bottom