Siasa zinazofanywa na CHADEMA zilifanywa na Prof. Lipumba na CUF wakati wa IGP Mahita zikafeli. Je, mwamba Mbowe atafaulu?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,198
2,000
Hizi siasa zinazofanywa na Chadema leo wakiongozwa na Mbowe zilishafanywa na CUF ya Lipumba na Maalim Seif enzi za IGP Omar Mahita lakini zilifeli.

Wakati ule CUF walijiita Ngangari na Mahita akawabatiza vijana wake jina la "Ngunguri" na kilichofuatia tunakijua CUF walihamia uhamishoni Mombasa kwa muda.

Siasa za zama hizi ni za kutumia akili zaidi kuliko nguvu.

Kama Chadema wataendelea na aina hii ya siasa wahesabu maumivu kwani hawatafika popote; wanaweza kuporomoka zaidi ya pale walipo CUF kwa sasa.

Urafiki wa CCM na upinzani katika awamu hii ya 5 hautofautiani sana na ule wa awamu ya 3 enzi za Mzee Mkapa.

Maendeleo hayana vyama!
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,506
2,000
Na Chadema inaelekea kuwa kama Cuf!

..unaweza kuia CHADEMAM an institution, lakini huwezi kuua matamanio ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

..CHADEMA inaweza kusambaratishwa lakini wafuasi wake watahamia kwenye chama kingine kitakachopata upenyo wa kuibuka.

..watu wenye umri wa makamo wanaoshabikia CHADEMA leo hii zamani walikuwa NCCR. Wengeni walikuwa radicals wakimuunga mkono Mtikila na dp.

..sasa hao wa umri wa makamo wamechanganyika na vijana ambao hawakukuzwa ktk mfumo wa chama kimoja.

..inabidi ufikirie vijana wenye miaka 30 kwenda chini kama fikra na mitizamo yao itaweza kuwa accomodated ndani ya mfumo wa vyama vingi / CCM.

..kwa maoni yangu hilo haliwezekani.
 
Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,376
2,000
sasa hivi mazingira yamebadilika sana tofauti na enzi za mr.clean
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
98,042
2,000
Tulieni dawa iwaingie vema
Hizi siasa zinazofanywa na Chadema leo wakiongozwa na Mbowe zilishafanywa na CUF ya Lipumba na Maalim Seif enzi za IGP Omar Mahita lakini zilifeli.

Wakati ule CUF walijiita Ngangari na Mahita akawabatiza vijana wake jina la "Ngunguri" na kilichofuatia tunakijua CUF walihamia uhamishoni Mombasa kwa muda.

Siasa za zama hizi ni za kutumia akili zaidi kuliko nguvu.

Kama Chadema wataendelea na aina hii ya siasa wahesabu maumivu kwani hawatafika popote; wanaweza kuporomoka zaidi ya pale walipo CUF kwa sasa.

Urafiki wa CCM na upinzani katika awamu hii ya 5 hautofautiani sana na ule wa awamu ya 3 enzi za Mzee Mkapa.

Maendeleo hayana vyama!

In God we Trust
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,506
2,000
sasa hivi mazingira yamebadilika sana tofauti na enzi za mr.clean

..wanachofanya ccm ni sawa na mzee anayelazimisha vijana wa kileo wasikilize muziki wa mwaka 70, wakati madogo hisia zao ziko ktk muziki wa kileo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom