Cuf waicharukia chadema, wasema inawafuata fuata kwenye mikutano yao ya kampeni


jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
1,861
Likes
408
Points
180
jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
1,861 408 180
CHAMA cha CUF kimekicharukia CHADEMA na kukitaka kuacha siasa za vurugu na kuwafuata fuata kwenye mikutano yao ya kampeni.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Ntatilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Igunga.
Alisema CHADEMA wamekuwa wa wakiwafuata fuata CUF kwenye mikutano yao mbalimbali ya kampeni jambo ambalo amesema linakera mno na ni ishaara ya kutafuta maafa.
"Ipo mifano ya wazi kwa hawa CHADEMA kutufutana fuata, kila tunakokuwa na mikutano wanakwenda na gari lao na kuliegesha karibu kabisa na mahali tulipo, haya yalitokea pale Itumba, Nanga na mahali pengi zaidi ya mara nne", alisema Ntatilo.
"Juzi nikiwa na mkutano pale Nanga , watu wawili wakiwa na magwanda ya CHADEMA walikuja na kuingia kabisa kwenye mkutano wetu, eti wakajidai kunisalimia. Hebu niambieni watu wakivaa sare za chama kingine kama CUF au CCM wakiingia mkutano wa CHADEMA wanaweza kusalimika?" aliuliza Ntatilo
Alisema, baada ya kujidai kumsalimia kwenye mkutano huo, Ntatilo aliwafukuza kistaarabu na kuwataka wasirudie tena utaratibu wao huo mbaya na wa kichokozi.
"Naomba sana katika siku hizi chache zilizobaki CHADEMA wajaribu kuwa wastaarabu ingawa naamini hawawezi, , wananchi wa Igunga wanachotaka ni uchaguzi wa amani na utulivu siyo magomvi", alisema Mtatilo.
Alisema, vyama vitakavyoendeleza vurugu wakati wa uchaguzi vitakuwa vimechuma dhambi kubwa, kwa sababu baada ya uchaguzi inatakiwa abaki mbunge siyo kuwaachia vifo wananchi wa Igunga.
Kuhusu CHADEMA kuwaita CUF CCM B, Ntatilo alisema, tuhuma hizo ni za kitoto na dalili kwamba CHADEMA hawajui siasa za kistaarabu.
" Sisi tulikuwa chama cha vurugu hakuna asiyejua, lakini imefika mahali tukaona kwamba hatuwezi kuendelea kuwa chama cha upinzani tu, lakini lazima tushike dola, sasa tumepata fursa tumepata pale Zanzibar, badala ya kutupongeza hawa CHADEMA wanatukejeli, hawa wanaakili kweli?" alisena Ntatilo.
"Yaani walitaka hata baada ya kufikia maelewano kwamba kuwepo na serikali ya Kitaifa, basi tukatae kila kitu na kuendelea kuwa ngangari tuuuu' ahhh' haiwezekani hicho kitakuwa ni chama kilichokuwa na lengo baya kwa nchi si CUF", alisema.
Katika hatua nyingine Ntatilo ameshusha tuhuma kwa CCM kwamba imeingiza 'janjawidi' kwa ajili ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii.
Hata hivyo CCM imekanusha vikali na kusema kwamba, haiwezi kufanya hivyo, na kwaamba vijana waliopo ni kwa ajili ya kulinda usalama wa viongozi na wanachama wa CCM na vijana hao siyo siri wanajulikana.
Mratibu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba alisema, ili kujiweka tayari na kuhakikisha inao vijana wa kutosha katika kusimamia baadhi ya shughuli kama za uwakala wakati wa uchaguzi imewap[a mafunzo ya kikakamavu na ya kujenga akili na siyo ya kijeshi kama inavyopotoshwa.
Wakati huohuo, Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Asha Abdallah Juma, amewataka viongozi wote wa CCM kuhakikisha kila mwana-CCM anajitokeza kupiga kura Jumapili.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za CCM kwenye kijiji cha Ipumbulya,Kata ya Bukoko jimboni hapa, Asha alisema, kimsingi CCM inao wanachama wengi na hata mikutano ya kampeni imedhihirisha hilo kwa hiyo hakuna sababu itakayoifanya CCM ishindwe wanachana, wapenzi na wakereketwa wote watajitokeza kupiga kura.
Asha alisema, serikali ya Chama Cha Mapinduzi itahakikisha unakuwepo usalama wa kutosha katika maeneo yote tangu majumbani, njiani na kwenye vituo vya kupiga kura hivyo mtu yeyote asihofu kutoka akidhani yupo atakayemdhuru.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira amesema hakuna chama chochote cha Siasa ambacho kimeweza kuonyesha hadi sasa kuwa kinaweza kuwa mbadala kwa CCM.
Akimnadi mgombea ubunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu, Wasira ambaye ni Mbunge wa Bunda alisema, ni kosa kwa sasa mtu yeyote kudhani kuwa kipo chama chenye uwezo kama CCM katika kuongoza wananchi kwa kuwa havijawa na sera makini.
"Vyama hivi vikija hapa mwanzo wa mkutano hadi mwisho ni matusi weee mpaka basi, na wakijaribu kutoa sera wanakopi zile zile za CCM ambazo wao hawawezi kuzitekeleza kwa kuwa haziwahusu" alisema Wasira.
1859130880412241953-4511551694622061183?l=fullshangwe.blogspot.com
 
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,426
Likes
3,481
Points
280
Mzee

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,426 3,481 280
Tar 2 si mbali, mbichi na mbivu zitajulikana.
 
Mchaka Mchaka

Mchaka Mchaka

JF Bronze Member
Joined
Jul 20, 2010
Messages
4,528
Likes
49
Points
0
Mchaka Mchaka

Mchaka Mchaka

JF Bronze Member
Joined Jul 20, 2010
4,528 49 0
Kama sikosei source ni habari leo.
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,602
Likes
1,644
Points
280
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,602 1,644 280
Udhaifu wako ni kuogopa kuandika majibu ya chadema kupitia kwa katibu mkuu wake Dr Slaa kuhusu madai ya CUF kwa chadema ila sishangai kwa nini umeposti hii thread kikuda hivi kwa sababu huna references mbalimbali za sources
 
Mshume Kiyate

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2011
Messages
6,773
Likes
30
Points
135
Mshume Kiyate

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2011
6,773 30 135
Ngoja Jumapili ifike hii habari ya Igunga tuimalize
 

Forum statistics

Threads 1,236,629
Members 475,218
Posts 29,264,875