CHADEMA wamtangazia vita Spika Makinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wamtangazia vita Spika Makinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Apr 20, 2013.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,265
  Likes Received: 1,215
  Trophy Points: 280
  [h=1][/h]


  [​IMG]
  Spika wa Bunge, Anna Makinda


  Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema kuwa watakata rufaa katika Kamati ya Kanuni ya Bunge dhidi ya mwongozo wa Spika uliobariki adhabu ya kuwatimua kwa siku tano wabunge sita wa Chadema kwa kudharau mamlaka ya Spika.


  Akitoa mwongozo wake jana, Spika Anne Makinda alibariki wabunge hao kutimuliwa akisema kuwa Kanuni za Bunge zilikiukwa.

  Wabunge waliofukuzwa na Naibu Spika, Job Ndugai juzi ni pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

  Juzi Mbowe aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya 68 (7), akimtaka Spika aeleze naibu wake (Ndugai) alitumia kanuni gani ya Bunge, kuwasimamisha siku tano wabunge sita wa Chadema wasihudhurie vikao vya Bunge vinavyoendelea.

  Mwongozo wa Makinda
  Akitoa mwongozo huo jana, Spika Anne Makinda alisema kuwa kitendo kilichotokea hakiwezi kupuuzwa na wala kuvumiliwa na Bunge, pamoja na wananchi kwa kuwa ni utovu wa nidhamu ya Bunge na wananchi kwa jumla.

  Alisema: “Kanuni ya 2(2) na 5(1), inampa mamlaka Spika ya kuleta amani bungeni.

  Kanuni ya 2(2) inaeleza: “Iwapo jambo au shughuli yoyote haikuwekewa masharti katika kanuni hizi, Spika ataamua utaratibu wa kufuata katika jambo au shughuli hiyo, kwa kuzingatia Katiba, Sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge na mila na desturi za uendeshaji bora wa shughuli za Bunge na uamuzi huo utaingizwa katika kitabu cha maamuzi ili kuongoza mwenendo wa baadaye wa uendeshaji wa shughuli za Bunge.”


  Kanuni ya 5(1) inaeleza: “Katika kutekeleza majukumu yake yaliyotajwa katika Ibara ya 84 ya Katiba, Spika ataongozwa na kanuni hizi na pale ambapo kanuni hazikutoa mwongozo, basi Spika atafanya kazi kwa kuzingatia Katiba, Sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa bunge la Tanzania.”

  Makinda alisema kwa kutumia kanuni hizo mbili anakubaliana na uamuzi uliotolewa na Ndugai na kwamba suala hilo litaingizwa kwenye kitabu cha uamuzi wa Spika.

  “Natumia Kanuni ya 2(2) na 5(1) kusema kuwa uamuzi uliofanywa na Ndugai ni halali na itaingizwa kwenye kitabu cha maamuzi ya Spika,” alisema Spika Makinda.

  Kauli ya Mbowe
  Mbowe jana alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi wa Spika ulijielekeza katika jambo lisilo na kanuni inayolisimamia, tofauti na lile la kudharau mamlaka ya kiti cha Spika, lililotolewa maelekezo na Kanuni ya 74 (1).

  Kanuni hiyo inasema: “Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge; ikiwa kwa maneno au vitendo mbunge huyo anaonyesha dharau kwa mamlaka ya Spika; au Mbunge huyo atafanya kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.”
   
 2. l

  lupe JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 1, 2013
  Messages: 5,659
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo spika makinda sura mbaya kama msaga sumu, kanuni na sheria za bunge hajui yeye ni bora liende...hatumtaki makinda na ndungai ni mzigo kwa taifa!!!
   
 3. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2013
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,211
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Haya nenda wewe unaejua kanuni,tatizo lenu.kufuata mkumbo,haya sasa vikao 5 nje,nini faida yakujifanya unajua sana,lissu sini mwanasheria akate rufaa,
   
 4. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2013
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 60
  Makinda ni kama bata wa kienyeji anayeharisha bila kujua hapa ni wapi,,,hajui alitendalo bungeni,nakili kuwa uadilifu wa bunge umepungua kutokana na aina mbovu ya uongozi wa spika bungeni,,,baba asiye na mke au mama asiye na mume ni vigumu kujua matatizo ya familia ndo anachokifanya bibi Makinda maana hata nikimuita mheshimiwa hastaili,nikimuita mama hana sifa kama wanawake wenzake
   
 5. Kifai

  Kifai JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2013
  Joined: Jan 18, 2013
  Messages: 819
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  umetumwa na basha wako mwigulu?
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,503
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  mkuu sitakosea kama nikikufananisha na yule aliyetukana F.U.C.K U bungeni na hakuna kifungu kinachoweza kumtia hatiani il kwa yule aliyenyimwa haki yake ya msingi ya kutoa taarifa akawa na kifungu cha kumwadhibu ila uzuri wake mahakimu wa kila miaka mi5 tunaona na la kufunya tushaamua
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,503
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kweli kwa7bu mengi anayoyafanya wanaoumia ni mama zetu na wanawake kwa ujumla maana wanawake hawa wamekuwa wakitetea masuala kama maji ila bi kiroboto na ccm kwa ujumla wameona halifai
   
 8. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,265
  Likes Received: 1,215
  Trophy Points: 280
  maneno kama ya Sugu
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,318
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180

  Mbowe anatishia nyauhuyo, kanuni hazijui.
   
 10. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2013
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,903
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Kama uwezi kuona uonevu wa maspika bungeni dhidi ya wabunge wa cdm si muda mlefu utajiunga na kundi la 'interahamwe'.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,318
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Mkuu ndo wale wale, unafikiri kwa nini bunge limekuwa uchochoro? Sababu ya kujaza vilaza kama akina sugu
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,318
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Haizekani Spika aache kufuata kanuni kisa Chadema watasema wameonewa, mimi naona bora ijulikane hivyo kuliko kubadilisha bunge kuwa kijiwe
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,318
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  ---- linaonekana tusi kubwa sababu ni neno la kiingereza nini? Mbona yametplewa matusi mengi tu tena yanaelekezwa kwa mtu moja kwa moja.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,318
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  mtu yeyote aliyezaliwa uwanja wa fisi kama wewe lazima atoe matusi ya nguoni kwa sababu anamuona mama yake kama CD, mlaumu mama yako mkuu, hata hivyo hayo sidhani kama yanaweza kumzuia kiongozi shupavu kufanya kazi.
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2013
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Jina lako na akili zako vinawndana sana...kikwetu ngongoseke ni mavi
   
 16. m

  magohe JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2013
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ajabu!!
  bungeni kuna kilaza zaidi ya spika na naibu wake?
   
 17. NullPointer

  NullPointer JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2013
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 3,482
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  Unajua ushabiki mkubwa wa wananchi ndio unaoleta ujinga wa namna hii Tanzania,
  Hivi Tanzania ndiyo imekua hivyo? Akili yote na nguvu yote imehamishiwa kwenye kutafuta kura 2015 kwa kuonyeshana ubabe kwa pande zote mbili huku hakuna inayobaki katika kuleta maendeleo. Iwe CCM au CHADEMA mi kwangu naona wote ni vita tu wamekalia na tamaa zimewajaa za kupata uongozi.. Hahaha blessed poor country with large number of dumbheads ambazo hazitaki kubadilika...
  Na hii nayo inachangiwa na wananchi kwa asilimia kubwa, badala ya kusimamana kuiambia serikali ikae ifanye kazi wananchi mnakaa mnashabikia hizi vita za kila siku.. We una chama nani alisema? Ujinga huu, mwananchi hatakiwi kukaa kwenye chama flani kama kweli ana upendo na nchi yake bali anatakiwa kuangalia mtu moja moja na kusema ingekua yeye kapewa uongozi wa kuchagua basi achague hao bora hata kama baadhi watatoka CHADEMA na baadhi CCM na sio kusema wote watatoka chama flani sababu ndiyo anachokipenda yeye.
  Tusichanganye mapenzi yetu na kazi, hili ni taifa 40M+ kuwaweka kwenye mgongo wako na kuwaongoza suo kiovyovyo hivyo, na watanzania muanze kubadilisha akili zenu zikaw kwenye kuleta maendeleo na sio kushabikia ugomvi kila siku, onyesha serikali wapi inatakiwa kufix na pangeni strategy za kuifanya ifanye hivo ila hata siku moja msikae mkaukubali huu ujinga unaoendelea na mnaufurahia, haha wanafunzi wa sekondari kweli nyie tena wale watumiaji wa facebook tu kila siku mnaweka picha za ajabu na kujiunga page za kijinga afu mnalaumu 95% ya waliofeli wote serikal ndiyo imesababisha huku hata hamjioni kwanza.. Mungu ibariki Tanzania, hii verse tuikumbuke na tuombe kila siku
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2013
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,387
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Hayo madudu yote wanayofanya ni mtaji mkubwa sana sana kwa majukwaa ya kuombea kura!CDM wajitahidi kulinda kura zao,pia wajiandikishe kwenye daftari jipya la kupiga kura maana najua itakuwa vita kubwa kupoteza majina ya vijana wengi hasa wa kiume ili wapate wasichana na wanawake watu wazima wawapigie kura waendelee kuiba!watanzania waamke,hasa vijana ujinga umetosha sasa twahitaji mabadiliko anzia kwa diwani,mbunge ndio tupande kwa Rais.....anza mkakati sasa
   
 19. delusions

  delusions JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2013
  Joined: Jan 11, 2013
  Messages: 4,955
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Spika siyo saizi yao cdm wataumbuka mwigulu tu wamemshindwa hadi sasa qmekuwa agenda sembuse spika
   
 20. j

  jigoku JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2013
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,383
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160
  Serukamba
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...