CHADEMA wamshambulia Kilango jimboni kwake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wamshambulia Kilango jimboni kwake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Dec 27, 2009.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  na Asha Bani, Same
  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliongoza Operesheni Sangara katika Jimbo la Same Mashariki kwa kumrushia makombora mazito mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela (CCM).

  Wakizungumza kwa zamu katika Kijiji cha Usambara ilipo nyumba ya Kilango kwenye Kata ya Kihurio, viongozi hao wa CHADEMA walieleza kusikitishwa na hatua ya mbunge huyo aliye katika kundi la wabunge wa chama tawala waliojipambanua kupambana na ufisadi, kusafiri hadi Moshi Mjini na kumshambulia mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA).

  Akihitimisha hotuba katika eneo hilo la nyumbani kwa Kilango baada ya viongozi wengine kuzungumza, Mbowe aliwataka wananchi wa Same Mashariki kutambua kuwa tatizo la ufisadi ndani ya CCM limeathiri mfumo mzima wa utawala.

  Kutokana na hali hiyo, Mbowe alisema matokeo ya hali hiyo yameifanya CCM kuongozwa na mafisadi ambao wamekuwa wakitumia kila aina ya hila kushinda wakati wa uchaguzi unapofika.

  Akimgeukia Kilango, Mbowe alisema, mbunge huyo wa CCM amekuwa akijinadi kupambana na ufisadi huku akijua fika kwamba waasisi halisi wa vita hiyo ni CHADEMA ambao Septemba 15, mwaka 2007 walitaja orodha ya watuhumiwa wakubwa 11 wa ufisadi nchini.

  Kutokana na ukweli huo, Mbowe alisema hatua ya Kilango kumshambulia Ndesamburo katika jimbo lake, inaweza kuifanya CHADEMA ikalazimika ‘kumfungia kazi’ mama huyo kwa kumuangusha katika kinyang’anyiro cha ubunge mwakani na kumfanya alazimike kwenda likizo kuishi na mumewe huko Mtera mkoani Dodoma.

  Akizungumza katika Kijiji cha Bendera, Kata ya Bendera wilayani hapa, Mbowe alisema hakuna sababu ya Kilango kupiga kelele bungeni kuwa anapambana na mafisaidi huku wakazi wa jimboni kwake wakiwa wanakunywa maji yanayotiririka mtaroni na kunywa pamoja na wanyama.

  “Sina ugomvi na Mama Kilango, nilikuwa naye bungeni, ni rafiki yangu, lakini ugomvi wangu unaanzia pale ninapomuona akiwa anapiga kelele bungeni za kudai ufisadi huku wakazi wa jimboni kwake wakiwa hawana huduma za afya, maji safi na salama, na hata barabara kupita ni shida, hii ni hatari sana, lazima wakazi wa Same muache kuwakumbatia wabunge wa namna hii, kelele zote anazopiga zilitakiwa kupambana na serikali ili wakazi wa Same wapate huduma bora na zinazostahili,” alisema Mbowe.

  Kijiji cha Bendera kwa sasa kinakabiliwa na njaa kali, jambo lililosababisha mwenyekiti huyo kumtaka Kilango kutumia muda wake mwingi katika kuwatafutia njia mbadala, hata kuwaombea chakula cha msaada na kusimamia, ili kiweze kufika kwa wakati.

  Kutokana na matatizo hayo, aliwalaumu wakazi wa Bendera kwa kutokuwa na maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi wao kana kwamba wamefunga ndoa na wabunge wa CCM.

  Alisema Kilango hawezi kuwatetea wakazi wa Same wakati yeye mwenyewe anaishi mjini Dodoma na mumewe John Samuel Malecela aliyewahi kuwa waziri na ambaye pia ni mbunge kwa kipindi cha miaka mingi.

  Mwanasiasa huyo alisema hata siku moja mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi hawezi kukaa mbali kwa kipindi kirefu na wapiga kura wake na kuonekana katika kipindi cha uchaguzi kwa ajili ya kuwatumia katika kampeni na kupata ushindi.

  Awali akihutubia mkutano huo wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika, alisema historia inaonyesha wazi kwamba wakati Ndesamburo alianza kupambana na ufisadi wa CCM tangu mwaka 2000 ndani na nje ya Bunge, Kilango ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa viti maalum, alikuwa kimya akitetea chama chake.

  Alisema uamuzi wa Kilango kujivua gamba la CCM na kuanza kujitanabahisha kupiga vita ufisadi, ulikuja baada ya viongozi wa CHADEMA kutangaza rasmi kupambana na ufisadi ndani ya serikali ya chama hicho tawala.

  “Kama kweli Kilango ni mpambanaji wa kweli wa ufisadi, anapaswa kumuunga mkono mbunge mwenzake wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Ndesamburo na CHADEMA ambao tunafanya mapambano ya kweli ya ufisadi,” alisema Mnyika na kusababisha umati wa watu kumshangilia.

  Wakizungumza kabla na baada ya mikutano hiyo ya hadhara, wananchi wa kata anayotoka Kilango walieleza kusikitishwa na hatua ya mbunge wao kupata muda wa kuitisha mikutano ya hadhara nje ya eneo lao wakati hajapata kufanya hivyo kwao.

  Walisema badala yake mbunge wao huyo amekuwa na desturi ya kuitisha mikutano ya ndani na wana CCM wenzake ambayo pamoja na kuzungumzia masuala yanayohusu jimbo lao, ameshindwa kupambana na mtandao wa udikteta na ufisadi unaoongozwa na viongozi wa kata yao.

  Wakitoa mfano wananchi hao waliwaeleza akina Mbowe kuwa, uamuzi wa kijiji kujenga lambo la kuhifadhi maji kwa lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji uliofanikisha kupatikana kwa sh milioni 28 umebatilishwa na kikundi cha wana CCM wachache na badala yake fedha hizo zimeamriwa zitumike kujengea maghala ya kuhifadhia chakula.

  Katika malalamiko yao, wananchi hao walisema, uamuzi wa kujenga maghala badala ya lambo la maji wanalolihitaji kwa kiasi kikubwa hivi sasa, umewasononesha ikizingatiwa kuwa, hadi hivi sasa kuna maghala mawili zaidi ya kuhifadhia chakula ambayo hayana hifadhi yoyote ya chakula kutokana na ukame ulioharibu mazao.

  Mbali ya hayo wananchi hao, waliwalaumu viongozi wa CCM na mbunge wao kwa kukaa kimya wakati wakazi wa Kata ya Kihurio anakotoka Kilango wakiporwa ardhi yao kwa kisingizio kuwa ni eneo la misitu.

  Walisema hatua ya ardhi yao hiyo kuporwa, imesababisha akina mama wengi kulazimika kwenda maeneo ya mbali kuchota maji na hivyo kuwaongezea matatizo mengi.

  Naye Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo Taifa wa CHADEMA, Benson Kigaila, alisema kuwa mbunge huyo hana hoja kutokana na kupiga kelele anapambana na ufisadi huku akishindwa kuwataja mafisadi wanaotuhumiwa.

  Alisema kuwa kama Kilango ni mpambanaji wa kweli wa ufisaidi, anatakiwa kutoka katika chama hicho na kutafuta chama mbadala kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya CCM wanaoongoza katika ufisadi nchini.
   
 2. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Daniel Mjema,Moshi


  MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametangaza rasmi kupiga kambi Moshi Mjini hadi mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa CCM inanyakua jimbo hilo, uamuzi ambao unamuingiza kwenye vita kali na mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo.

  Katika kuonyesha kuwa Ndesamburo hana nguvu kwenye jimbo hilo, Kilango aliwaambia wanachama na viongozi wa CCM kuwa mbunge huyo kutoka Chadema ameshinda mara mbili mfululizo kutokana na matatizo ya wanaCCM wenyewe na kuwataka wajisafishe.

  Kilango, ambaye amekuwa akilalamika kuwa mafisadi wanataka kuchukua jimbo lake la Same Mashariki, alitangaza mkakati huo jana wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi, ikiwa dalili za wazi kwamba, CCM sasa imeanza kujipanga kufanya mashambulizi mkoani hapa ambako vyama vya upinzani vinaonekana kuwa na nguvu kubwa.

  “Nitapiga kambi hapa... kwanini tupate madiwani 12 na Chadema watatu halafu tushindwe ubunge,” alihoji Kilango. “Nitakaa hapa mpaka nimfahamu mchawi ili nimshike mkono nimwambie Rais (Jakaya) Kikwete huyu ndiye anayetufanya tushindwe na Ndesamburo.”

  Mbunge huyo aliongeza kusema:”Hatuwezi kukubali kuwa na wanaCCM ambao mchana wamevaa kijani, lakini usiku wamevaa nguo nyingine…nimeongea na Ndesamburo ananiambia wanaompa ubunge ni wanaCCM wenyewe… hili halikubaliki”.

  Alisema kuwa suala la Jimbo la Moshi Mjini kuwa chini ya upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 linampa tabu sana na hilo ndilo lililomsukuma kupiga kambi katika jimbo hilo hadi uchaguzi mkuu wa 2010.

  “Leo nimebisha hodi hapa tutakuwa wote mpaka Oktoba 2010 na kama tunakosa naomba wananchi mtuambie mapema nini na ndio maana nitakuja kila siku hapa, lakini na nyinyi viongozi na wanaCCM mjitazame inakuwaje tuna madiwani 12 tukose mbunge,” alisema mbunge huyo wa Same.

  Hata hivyo, alisema katika kipindi cha siku mbili tu alizokaa Moshi Mjini ameambiwa kuwa moja ya kero inayoinyima CCM ushindi ni vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga.

  Kilango alifafanua kuwa hakuna mtu muhimu kama anayejitafutia riziki yake, lakini ni jambo baya kama mtu huyo anakwamishwa na kuapa kuwa kwa suala hilo la machinga, ikibidi kulifikisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, basi atafanya hivyo.

  “Sisi tuna njia zetu pale bungeni unaweza kuuliza maswali ya kawaida au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na ikibidi kumuuliza, nitamuuliza,” alisema Kilango.

  Katika hali iliyodhihirisha kuwa suala hilo la machinga linagusa mioyo ya wananchi wengi wa mji wa Moshi, mara tu baada ya Kilango kulitaja, umati wa wananchi na wafuasi wa CCM ulilipuka kwa furaha.

  Mbunge huyo aliamua kumsimamisha katika hadhara hiyo mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi Kuu ya Moshi, Vicent Asenga kuelezea kile kinachowakwaza hadi waamue kutoipa CCM kura katika vipindi vitatu mfululizo.

  Asenga alisema waliingia makubaliano na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwamba kama wanataka kutoa huduma ya biashara kwenye stendi hiyo, wawe na vitambulisho na sare jambo ambalo walilitekeleza kikamilifu.

  Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema walishangaa siku moja wakivamiwa na kukamatwa na kupelekwa ofisi ya kikosi cha usalama barabarani na kutozwa faini ya kati ya Sh20,000 hadi Sh40,000 kana kwamba wao wamefanya makosa yanayohusiana na usalama barabarani.

  “Sisi hatuna upinzani na CCM lakini tuna upinzani na wanaotukwamisha,” alisema Asenga huku akishangiliwa na wananchi waliofurika katika mkutano huo na kuhoji kama makosa ya kufanya biashara yana uhusiano wowote na kikosi cha polisi wa usalama barabarani.

  Kutokana na maelezo hayo na kuwepo wafanyabiashara wengine waliojitokeza kutaka kuzungumza, Mama Kilango aliwataka wafanyabiashara hao kuteua wawakilishi watano ambao angekutana nao jana jioni kupata picha halisi ya kero hiyo.

  Suala la Machinga limekuwa kete ya kisiasa na Ndesamburo aliwahi kununua eneo kwa ajili ya kuanzisha soko la wafanyabiashara hao wadogo, lakini inadaiwa kuwa aliwekewa vizingiti na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, uamuzi ambao unadaiwa kuzidisha hasira ya wafanyabiashara dhidi ya CCM.

  Jimbo la Moshi Mjini limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 1995 likianzia kwa Joseph Mtui wa NCCR (1995-2000) na Philemon Ndesamburo wa Chadema ambaye ameshikilia Jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo (2000-2005 na 2005 hadi 2010).

  Mwaka 1995, CCM ilimsimamisha mkuu wa Itifaki, kapteni mstaafu, Abubakar Nkya ambaye alishindwa vibaya na Mtu wa NCCR kabla ya kumsimamisha wakili Elizabeth Minde 2000 na 2005 ambaye hata hivyo hakufua dafu kwa Ndesamburo.
  Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika mwezi uliopita, CCM iliibuka na ushindi wa asimia 65 ikinyakua mitaa 39 huku CHADEMA ikichukua mitaa 21.

  ......ndiyohiyo
   
 3. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Moderator

  Naona mmebadili kichwa cha habari na reason umeandika 'upotoshaji wa makusudi wa kichwa cha habari'.

  Hakuna upotoshaji, kichwa hicho "CHADEMA yamshambulia anna kilango nyumbani kwao' ndio kimetumiwa na chanzo cha habari.

  Tazama website ya Tanzania Daima: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=11502
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Ahsante sana kwa hizi taarifa ambazo zinajisema zenyewe what is what, wala hakuna cha kuongezea.

  Respect.


  FMEs!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Duh!!!!!!!!!!!!
   
 6. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Duh!!!!!!!!!!!!
   
 7. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaaazi kweli kweli

  Kama upinzani haihitaji kusubiri mpaka mmoja wenu ashambuliwe ndo mujipange kulichukua jimbo toka mikononi mwa chama tawala. Naimani ni majukumu yenu ku hakikisha mnakamata majimbo mengi kadri iwezekananvyo na hakuna sababu ya kutishana kufungiana kambi.

  Kama mna nguvu lichukueni hilo jimbo na majimbo mengine yote. Tukianza zungumzia kufungiana kambi sijui kwa kipindi cha kampeni cha mwezi mmoja tutafunga kambi majimbo mangapi na sijui tutaambulia nini kwenye huo uchaguzi.

  Jipangeni wakuu
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nafikiri tukisoma kwa makini zaidi hawa viongozi wa Chadema wamechukizwa na kauli ya Mama Kilango ya kutia kambi Moshi mjini kupambana na sharehlder mkubwa a Chadema Mzee Ndesamburo.

  Ni vizuri vyama vya siasa huko Tanzania kujikita katika kuzungumzia matatizo ya wananchi na kutoa suluhisho lake kuliko kum defend mtu kwa kumkashifu mwingine.

  Chadema mnatumia pesa nyingi sana sasa jifunzeni kupambanua miongoni mwa mambo binafsi na mambo ya kijamii.

  msitumie majukwaa yenu kumzungumzia Kilango bali zungumzieni matatizo ya sehemu husika na kunadi sera zenu.
   
Loading...