Chadema wamshambulia Edward Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wamshambulia Edward Lowassa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 24, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Na Sharon Sauwa
  24th March 2010

  [​IMG]
  Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

  Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ameshambuliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiwahoji watu wa jamii ya Kimasai kuamua kutoa cheo cha kimila kwa mtu ambaye amekuwa akikaa kimya wakati wanagombania ardhi...Mashambulizi hayo yalitolewa jana na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri Kuu ya Chadema, John Mrema, wakati akihutubua mkutano wa operesheni Sangara katika kijiji cha Mbeli wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara.

  Mrema alisema Wamasai wilayani Kiteto wamekuwa wakijeruhiwa na kuuawa katika mapigano ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

  Alisema kuwa ugomvi huo ungeweza kutatuliwa kwa kutenga ardhi kwa ajili ya wakulima na wafugaji, lakini hadi sasa serikali ya CCM haijachukua hatua.

  Mrema alisema nchi nyingi ambazo zimekuwa na mapigano sababu kubwa ni ugomvi wa ardhi na kutahadharisha kuwa kama matatizo hayo hayatarekebishwa, nchi itaingia katika matatizo makubwa.

  Alitolea mfano kwa Sudan ambayo alisema vita ilisababishwa na mafuta pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuingia katiika mapigano kutokana na kugombania madini. "Nyie Wamasai mmetoa cheo kwa Lowassa ni vipi mnampa cheo cha kimila mtu ambaye amekuwa hawatetei, anakaa kimya bungeni?" alihoji Mrema.

  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kukaa pembeni wakati wa uchaguzi mkuu na kukiacha chama chake kipambane na CCM kwa uhuru. Alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mkutano wa operesheni Sangara uliofanyika katika viwanja vya Kata ya Kitelesa, wilayani Kondoa."Tuacheni tupambane na CCM wenyewe, msiingilie," alisema Mbowe.

  Alisema wakati wa uchaguzi, polisi wamekuwa wakiwaandama wananchi na vyama vya siasa.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiki chama matatizo ona majina yote ya viongozi wao ni akina 'MEKU'
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hakuna aliposhambuliwa , ila wameeleza ukweli kuwa Lowassa hashughulikii matatizo ya waliompeleka kule Bungeni, yeye kutwa kwenye vikao na kina RA na mafisadi wa kariba hiyo.
   
Loading...